Maaskofu 500 wa Kanisa la Ufufuo na Uzima watinga Mahakamani kufuatilia kesi ya Kanisa kufungiwa

Maaskofu 500 wa Kanisa la Ufufuo na Uzima watinga Mahakamani kufuatilia kesi ya Kanisa kufungiwa

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mawakili wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania, Peter Kibatala na Gloria Ulomi wakiwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kwenye kesi ya kupinga kufutwa kwa kanisa hilo. Wengine ni viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo wa kanisa hilo waliofika kusikiliza shauri hilo.

Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa alitangaza kulifuta kanisa hilo linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima kwa kile alichoeleza limekiuka Sheria ya Jumuiya Sura ya 337, kwa kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa na nia ya kuichonganisha Serikali na wananchi.

1749809347807.jpeg


===========================​

Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church, maarufu kama Kanisa la Ufufuo na Uzima, limefungua kesi Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, likiomba amri ya muda ya kuondoa zuio lililowekwa na Serikali dhidi ya kuendelea kwa shughuli zake za kidini, huku ikiripotiwa takribani maaskofu 500 wamefika kusikiliza kesi hiyo.

Kesi hiyo inalenga kulinda hadhi ya usajili wa kanisa hilo huku rufaa dhidi ya zuio hilo ikiendelea kusikilizwa.
Kanisa hilo linaongozwa na Askofu Josephat Gwajima, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe kupitia CCM.

Hivi karibuni, mamlaka za Serikali zilifunga kanisa hilo kwa madai kwamba linaendesha shughuli kinyume na masharti ya leseni ya usajili wake.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mamlaka, baadhi ya shughuli zinazofanyika ndani ya kanisa hilo zimeelezwa kuwa ni za ‘kisasa kupita kiasi’, na hazilingani na malengo ya asili ya taasisi hiyo kama ilivyosajiliwa.

Kupitia kwa wakili wake, Peter Kibatala, kanisa hilo limewasilisha shauri namba 13189 la mwaka 2025 dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na Msajili wa Taasisi za Kiraia.

Katika shauri hilo, Glory of Christ Tanzania Church inaiomba mahakama kutoa amri ya muda itakayoruhusu kuendelea kwa ibada na shughuli nyingine za kidini, hadi pale rufaa iliyowasilishwa kupinga hatua ya serikali kufungia kanisa hilo itakaposikilizwa na kuamuliwa rasmi.


Source: Mwananchi
 
Mawakili wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania, Peter Kibatala na Gloria Ulomi wakiwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kwenye kesi ya kupinga kufutwa kwa kanisa hilo. Wengine ni viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo wa kanisa hilo waliofika kusikiliza shauri hilo.

Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa alitangaza kulifuta kanisa hilo linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima kwa kile alichoeleza limekiuka Sheria ya Jumuiya Sura ya 337, kwa kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa na nia ya kuichonganisha Serikali na wananchi.
Kuna habari zaidi ya hii, au ndiyo umemaliza?
 
Wateja wengi wa kibataba ni mission town, cheki wanavyozuga kwamba ni wachungaji na church attire zao
 
d664f62d-dddb-4d8f-bf64-d162ea61f00e.jpg


Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma leo Juni 13 inaendelea kusikiliza kesi ya kupinga kufutwa kwa Kanisa la Glory of Christ Tanzania (Nyumba ya Ufufuo na Uzima).

Juni 2 Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa alitangaza kulifuta kanisa hilo linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima kwa kile alichoeleza limekiuka Sheria ya Jumuiya Sura ya 337, kwa kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa na nia ya kuichonganisha Serikali na wananchi.

Upande wa walalamikaji (Kanisa la Glory of Christ Tanzania) unaongozwa na mawakili wa, Peter Kibatala na Gloria Ulomi umefika mahakamani hapo tayari kwa kesi hiyo, wakiambatana na viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo wa kanisa hilo waliofika kusikiliza shauri hilo.
 
Mawakili wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania, Peter Kibatala na Gloria Ulomi wakiwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kwenye kesi ya kupinga kufutwa kwa kanisa hilo. Wengine ni viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo wa kanisa hilo waliofika kusikiliza shauri hilo.

Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa alitangaza kulifuta kanisa hilo linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima kwa kile alichoeleza limekiuka Sheria ya Jumuiya Sura ya 337, kwa kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa na nia ya kuichonganisha Serikali na wananchi.



Source: Mwananchi
Aisee kuna mauzauza mengi sana hii TZ 🤣
 
Wateja wengi wa kibataba ni mission town, cheki wanavyozuga kwamba ni wachungaji na church attire zao
Aiseee wewe ulizaliwa kama binadamu wengine au ULITAPIKWA kama matapishi?
 
Sasa kuna ubaya Gani kutoka mahubiri ya kisiasa ikiwa Gwajima ni mwanasiasa? Je kuna Sheria inayomzuia kiongozi wa kidini na pia mwanasiasa kuzungumzia habari za siasa? Au anashtakiwa kwa kifungu Gani Cha Sheria?
 
Back
Top Bottom