Maaskofu, Mapadre, Hawatayumbishwa na Waumini Kama Ludovivk, Walioamua Kumtumikia Shetani

Maaskofu, Mapadre, Hawatayumbishwa na Waumini Kama Ludovivk, Walioamua Kumtumikia Shetani

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Jambo lililo dhahiri, na kwa mafundisho ya kiimani, shetani huwatumia wanadamu kufanikidha malengo yake. Sio wote waliopo makanisani au waimbao Bwana Bwana, au wenye majina ya Kikristo, ni waumini na wafuasi wa Kristo na Kanisa. Wengine wapo makanisani kwaajili ya kulivuruga na hata kuliangamiza Kanisa la Kristo. Japo kwa uhakika hawatafanikiwa kamwe, maana msingi mkuu wa Kanisa ni Kristo mwenyewe.

Siku za karibuni wameibuka matapeli wa imani wakijitambulisha kuwa ni wakatoliki, kulishambulia Kanisa la Kristo. Nawaita hawa ni matapeli, kwani wanawatapeli hao wanaowatuma, kuwa wao ni wakatoliki. Ukristo na ukatoliki siyo kuingia ndani ya kanisa Katoliki au kuitwa Ludovick, bali ni kuyaishi mafundisho ya Kristo na Kanisa.

Kwa wasiofahamu, Kanisa katoliki lina taratibu zilizo wazi kabisa zisizo na shaka kwa muumini yeyote halisia, achana na hao matapeli akina Ludovick. Matapeli kwaajili ya kutumika dhidi ya Kanisa wamekuwa wakitapatapa, na kurukia hili na lile, mara maaskofu hawatoi taarifa za pesa, mara maaskofu wanahubiri siasa, mara Maaskofu wanatoa matusi. Mkatoliki yeyote anajua yafuatayo:

1. Masuala yote ya fedha ndani ya kanisa Katoliki yanasimamiwa na mabaraza ya walei, hayasimamiwi na paroko au Askofu. Pesa ambayo ni haki ya padre/askofu (kuhani), ni sadaka. Na hii ni kwa mujibu wa maandiko. Sadaka zote zitolewazo kwa Mungu, tangu kale, zilikuwa ni kwaajili ya walawi ambao walikuwa makuhani. Zaka na michango mingine ambayo ni kwaajili ya maendeleo ya Kanisa, matumizi yake husimamiwa na baraza la walei. Kama una ushauri, maoni au maswali, kuna vikao mbalimbali, kuanzia kwenye jumuia ndogo ndogo, parokia mpaka jimbo ambako utapewa ufafanuzi au majibu.

2. Mapadre na Maaskofu ni viongozi wakuu wa kiroho, na katika masuala mengine yote hubakia kuwa washauri. Kwenye masuala yote ya kiroho na kichungaji, Padre au Askofu, ndiye mwenye maamuzi ya mwisho, akipenda anaweza kutoa nafasi ya kupokea ushauri na maoni, lakini halazimiki kufuata huo ushauri kwani ushauri huo hauwi maamuzi au maazimio. Hakuna muumini au mtu mwingine yeyote anayeweza kumwelekeza padre au Askofu aseme nini awapo kwenye mahubiri. Kama ingekuwa ni waumini wanaoamua padre au Askofu ahubiri nini, matapeli kama akina Ludovick wangesema padre asihubiri dhidi ya utapeli, ukahaba, dhuluma au mapato yasiyo halali. Lugha kali katika mahubiri siyo matusi, na mahubiri makali yameruhusiwa katika Kanisa.

2 Tim 4:2
Lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.

Tit2:15
Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote.
Mtume Paulo alipoona waumini wa kule Galatia wamekengeuka na kurudia kwenye maisha yao ya kale, aliwaonya kwa ukali, akawaambia hawana akili:

Gal 3:1
Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga.
Maneno makali ya Baba Askofu Ruwaichi dhidi ya yule lofa tapeli, hayakuwa tusi bali ni karipio dhidi ya uovu wake na waliomtuma.

Hata Ludovick, kama ni muumini kweli wa Kanisa Katoliki, halafu hajui utaratibu huu wa Kanisa ulio wazi, halafu anataka awafundishe nini maaskofu na mapadre wahubiri wanapokuwa kwenye ibada, basi huyu ni mwehu, anayetakiwa kuonywa kwa lugha kali au kuchukuliwa hatua kali.

Kwa kufuata kanuni za Kanisa, na kadiri Roho wa Mungu atakavyomwongoza, ni vema maparoko wa hawa matapeli wakawafungia wahusika kupata huduma zote za kuroho zinazotolewa na Kanisa mpaka watakapotubu.

Tangu kale, watawala na waovu wenye kiburi, hawakuyapenda mafundisho ya Kristo, wala ya mitume wake, na hao ndio wengine walifanya kila njia kuyafifisha mafundisho ya Kristo au kuyatafutia dosari, na hata kufanya mioango ya kuwaua ili tu kuulinda uovu wao, sawa na haya wanayoyafanya hawa akina Ludovick na wengine ambao bado wanaandaliwa. Haya yanayotokea, yenye msukumo wa watawala wadhulumu haki za watanzania wote, hayawezi kutetemesha, kulililegeza wala kulitisha Kanisa la Mungu. Yote haya ni utimilifu tu wa yale yaliyonenwa na Kristo. Kama Yuda Iskariote, tena akiwa mtume wake alitenda uovu ule, ni nini kitashangaza akina Ludovick and the like kuyafanya haya wanayofanya dhidi ya Kristo na Kanisa lake, na watumishi wake.

Mababa zetu katika imani, maneno na matendo ya ibilisi akitumia maneno na vitendo kupitia miili ya wanadamu, nina imani hayatawalegeza bali yatawaimarisha zaidi na kuonesha ukuu wa Mungu dhidi ya shetani na mawakala wake, bila ya kujali mawakala hao wataibukia nje au ndani ya Kanisa, ukweli unaosimama kwenye misingi ya upendo wa Kristo, lazima unenwe na Kanisa wakati wote kama walivyofanya mababa zetu tangu Kale.

Sauti za shetani zilizomo ndani ya Kanisa, Roho wa Mungu awaongoze katika kuyatumia maagizo haya ya Bwana wetu Yesu Kristo: "Lolote mtakalolifungia Duniani na mbinguni limefungiwa, na lolote litakalofunguliwa Duniani na mbinguni limefunguliwa".

Tukumbuke haya yanayotokea sasa ni madogo sana kuliko yale waliyoyapitia mababu zetu wa imani.
Daima maneno haya ya mashahidi wa imani yatuongoze sote:
INATUPASA KUMTII MUNGU KULIKO WANADAMU.​
 
Back
Top Bottom