Maaskofu na Wachungaji zaidi ya 1200 wa Kanisa la Askofu Gwajima watinga Mahakamani Dodoma

Maaskofu na Wachungaji zaidi ya 1200 wa Kanisa la Askofu Gwajima watinga Mahakamani Dodoma

Wewe ndo umehusika kufungia kwa kutumia akili ndogo

Kosa la mchungaji mmoja haliwezi kusababisha watu zaidi ya milioni wawe kwenye kosa hilo hilo

Kamata Gwajima weka ndani, kanisa liendelee

Sielewi nyinyi ccm ni hadi zipite karine ngapi ndio mpate walau akili kidooogo kabisa
Mimi sihusiki natoa yangu

Maamuzi kuhusu Gwajima yalitakiwa kutolewa na uongozi wa kanisa

Ndio maana kuna bodi hadi ya wadhamini kusimamia katiba yao ya taasisi na mali zake sio kazi ya serikali

Hawakufanya hivyo wakaacha tu taasisi kutumika kisiasa tena za hovyo

Msajili akaamua afunge taasisi
 
Aliyetoa uamuzi wa kufungia kanisa kwasababu mtu mmoja ametoa kauli gani sijui ni zaidi ya MPUMBAVU! Yaani wanaiabisha serikali hawa watu. Unakosaje akili kiasi hicho?
Ni mpumbavu kama alivyo Mchungaji wa mchongo Richard Hananja aliyekubali kuuza utu wake kwa vipande 30 vya fedha.
 
Mimi sihusiki natoa yangu

Maamuzi kuhusu Gwajima yalitakiwa kutolewa na uongozi wa kanisa

Ndio maana kuna bodi hadi ya wadhamini kusimamia katiba yao ya taasisi na mali zake sio kazi ya serikali

Hawakufanya hivyo wakaacha tu taasisi kutumika kisiasa tena za hovyo

Msajili akaamua afunge taasisi
Ukiondoa kile kisicho sheria kwamba, kiongozi wa dini ama taasisi za dini hazipaswi kuzumgumzia masuala ya kisiasa

Unauhakika alichokuwa akisema Gwajima ni cha hovyo?

Kama ndivyo, hauko timamu, licha kwamba unachotetea ni chama chako

Gwajima, hakumtukana yeyote, alichosema ni kuwepo idadi kubwa ya watu kupotea/kupotezwa na mamlaka kama hazichuki hatua

Akatolea mfano ambao huo ndilo kosa lake, ikitokea mtoto wa kiongozi kapotea/kupotezwa, hakutachangamka?

Kama ndivyo je, ni halali kupotea mtu baki kwa kuwa umaana wake ni mdogo kuliko viongozi?

Hayo ni makosa kweli au ni chuki dhidi ya ukweli?

Maoni yangu, Yaweza kuwa Gwajima alitoa mfano usio faa, lakini kwa nini isingetosha kutufanya kama nchi tukae pamoja tuzungumze jambo hili?

Kulikuwa na kosa gani hapo?
 
Huelewi kitu
Taasisi za din haziruhusiwii kuendesha siasa

Iliyosajiliwa ni taasisi sio Gwajima

Kwa hiyo Gwajima kutumia taasisi kuendesha siasa mhalifu anakuwa taasisi waliompa platform kuwa imekiuka masharti ya usajili

Msajili hakumsajili Gwajima.Gwajima aweza hama kanisa au acha taasisi itaendelea

Taasisi ndio inawajibika kwa kukiuka masharti ya usajili sio mtu
Kwa kuwa ndani ya CCM kuna watu ni mafisadi na majizi ya mali yauma hivyo tuseme CCM ni Chama Cha Mafisadi na majizi? Hivi ni lazima ukiwa mwanaccm ujitotoe ufahamu kiasi hiki?
 
Familia haisajiwi kwa msajili baba wala watoto

Msajili mkataba wa usajili wa taasisi hiyo ni kati yake na taasisi sio kati yake na Gwajima au Mwanamapinduzi au yeyote au mke au mtoto au muumini wa hilo kanisa

Viongozi waliopo na waumini waliopo waweza ondoka hata leo msajili atabaki kuangalia taasisi kama inazingatia maadili na masharti ya usajili tu si vinginevyo

Msajili kafunga sababu ya taasisi kukiuka masharti ya usajili.Hapo hahangaiki na hayo mavazi ya kiaskofu na kichungaji mliyoingia nayo mahakamani hayo hayamtishi msajili wala hakimu ni sheria tu
Crap from low brain.
 
Maaskofu na Wachungaji wanaohudumu kupitia Kanisa la Glory Of Christ Tanzania Church(Ufufuo na Uzima) 'kanisa la Gwajima' wakiingia na kukaa katika chumba cha mahakama hapa katika Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dodoma kwa ajili ya kufuatilia shauri la kanisa wanalohudumu ambalo limezuiwa kutoa huduma kuanzia juni 02, 2025.

Pia, Soma: Kesi ya Kanisa la Gwajima kufungiwa kunguruma leo Dodoma

Viongozi hawa wametoka maeneo mbalimbali nchini na kuja hapa Dodoma ili kujua hatma ya kanisa hilo lililopo chini ya Askofu Dkt. Josephat Gwajima ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaam.

Kesi hiyo inalenga kulinda hadhi ya usajili wa kanisa hilo huku rufaa dhidi ya zuio hilo ikiendelea kusikilizwa. Kanisa hilo linaongozwa na Askofu Josephat Gwajima, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe kupitia CCM.

Hivi karibuni, mamlaka za Serikali zilifunga kanisa hilo kwa madai kwamba linaendesha shughuli kinyume na masharti ya leseni ya usajili wake.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mamlaka, baadhi ya shughuli zinazofanyika ndani ya kanisa hilo zimeelezwa kuwa ni za ‘kisasa kupita kiasi’, na hazilingani na malengo ya asili ya taasisi hiyo kama ilivyosajiliwa.

Kupitia kwa wakili wake, Peter Kibatala, kanisa hilo limewasilisha shauri namba 13189 la mwaka 2025 dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na Msajili wa Taasisi za Kiraia.

Katika shauri hilo, Glory of Christ Tanzania Church inaiomba mahakama kutoa amri ya muda itakayoruhusu kuendelea kwa ibada na shughuli nyingine za kidini, hadi pale rufaa iliyowasilishwa kupinga hatua ya serikali kufungia kanisa hilo itakaposikilizwa na kuamuliwa rasmi.

Wangekuwa chadema tayari ungekuta polisi wamekasirika kwanini wanajaa mahakamani
 
Ukiondoa kile kisicho sheria kwamba, kiongozi wa dini ama taasisi za dini hazipaswi kuzumgumzia masuala ya kisiasa

Unauhakika alichokuwa akisema Gwajima ni cha hovyo?

Kama ndivyo, hauko timamu, licha kwamba unachotetea ni chama chako

Gwajima, hakumtukana yeyote, alichosema ni kuwepo idadi kubwa ya watu kupotea/kupotezwa na mamlaka kama hazichuki hatua

Akatolea mfano ambao huo ndilo kosa lake, ikitokea mtoto wa kiongozi kapotea/kupotezwa, hakutachangamka?

Kama ndivyo je, ni halali kupotea mtu baki kwa kuwa umaana wake ni mdogo kuliko viongozi?

Hayo ni makosa kweli au ni chuki dhidi ya ukweli?

Maoni yangu, Yaweza kuwa Gwajima alitoa mfano usio faa, lakini kwa nini isingetosha kutufanya kama nchi tukae pamoja tuzungumze jambo hili?

Kulikuwa na kosa gani hapo?
Wanasema et aliyekuwa akiyaongea Gwajima ni siasa hivyo kafanya siasa kanisani.
 
Huelewi kitu
Taasisi za din haziruhusiwii kuendesha siasa

Iliyosajiliwa ni taasisi sio Gwajima

Kwa hiyo Gwajima kutumia taasisi kuendesha siasa mhalifu anakuwa taasisi waliompa platform kuwa imekiuka masharti ya usajili

Msajili hakumsajili Gwajima.Gwajima aweza hama kanisa au acha taasisi itaendelea

Taasisi ndio inawajibika kwa kukiuka masharti ya usajili sio mtu
Lakini Mwandishi wa habari akizingua anawajbika yeye na sio media husika? Ujinga ni mzigo wa mavi kichwani
 
Inategemea hujawahi ona vyombo vya habari vikifungiwa?

Wewe ndio hujui
Ni Kwa sababu wewe umeamua upande wa kutokuongeza ufahamu, labda nikusaudie tu kwamba swala la kufungiwa vyombo vya habari Kwa kile kilichoitwa makosa ya waandishi wa habari lilipigiwa kelele na wamiliki na wahariri na serikali ukabadili kanuni hiyo na kufanya mzigo huo abebe Mwandishi peke yake. Ni hayo tu.
 
Sio kweli mfano mimi nikidhalilishwa na chombo cha habari siwezi mshtaki mwandishi binafsi nitakiburuza mahakamani chombo cha habari
 
Back
Top Bottom