Maaskofu na Wachungaji zaidi ya 1200 wa Kanisa la Askofu Gwajima watinga Mahakamani Dodoma

Sio kweli mfano mimi nikidhalilishwa na chombo cha habari siwezi mshtaki mwandishi binafsi nitakiburuza mahakamani chombo cha habari
Hayo ni mawazo Yako lakini Kuna Sheria na Kanuni sasa ambazo zinaelekeza aliyekosea kuwajibika

Kwa mujibu wa Kifungu cha 50 cha Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016, mwandishi au mchapishaji yeyote ambaye anachapisha au kutangaza taarifa ya uongo au upotoshaji kwa makusudi au kwa uzembe mkubwa, atakuwa ametenda kosa la jinai. Sheria inaeleza wazi kuwa mtu huyo ni yule ambaye “anachapisha au kutangaza taarifa ambayo anajua au angepaswa kujua kuwa ni ya uongo au ina lengo la kupotosha umma.” Adhabu kwa kosa hili ni faini isiyopungua shilingi milioni tano (TSh 5,000,000) au kifungo kisichozidi miaka mitatu (3) au vyote kwa pamoja. Hili linaonesha dhamira ya sheria kuhakikisha kuwa waandishi wanatimiza wajibu wao kwa weledi na uaminifu wa hali ya juu.

Aidha, Kifungu cha 52(1) kinazungumzia kuchapisha taarifa za uchochezi (seditious publication). Kwa mujibu wa kifungu hiki, taarifa yoyote inayochapishwa kwa lengo la kuleta chuki dhidi ya serikali, au kuchochea wananchi kuasi mamlaka halali, au kuvuruga amani na mshikamano wa kijamii, inachukuliwa kuwa ni ya uchochezi. Hata kama taarifa hiyo inaonekana kuwa ni maoni ya mtu binafsi, ikiwa ina athari za kuvuruga utulivu wa jamii, basi mwandishi au mchapishaji wake anawajibika kisheria.

Kwa upande mwingine, Kifungu cha 52(2) kinaweka wazi kuwa hata kama mtu hakuwa na nia ya kuchochea, lakini alichapisha au kutangaza taarifa ya aina hiyo kwa uzembe au bila kufanya uchunguzi wa kutosha, bado atawajibika kwa mujibu wa sheria. Hii inamaanisha kwamba mwandishi hawezi kujitetea kwamba hakujua, kwani sheria inamtaka awe makini na kufanya utafiti wa kina kabla ya kuchapisha taarifa yoyote yenye uzito kwa jamii au nchi.

Hatimaye, Kifungu cha 54(1) kimeweka bayana adhabu kwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia ya kuchapisha au kutangaza taarifa ya uchochezi. Adhabu hiyo ni pamoja na kutozwa faini isiyopungua shilingi milioni tano (TSh 5,000,000), au kifungo kisichozidi miaka mitano (5), au vyote viwili. Adhabu hizi ni nzito kwa makusudi ya kuzuia matumizi mabaya ya vyombo vya habari kwa manufaa binafsi au kisiasa, na kulinda utulivu wa taifa.
 
The TZ government is full of idiots! Yaani hawa bastards wanafunga kanisa lenye maelfu ya watumishi wa Mungu na makumi ya maelfu ya waumini kwasababu ya tuhuma dhidi ya muumini kiongozi mmoja?
 
Katoliki ina makanisa kila kona,ila ina maaskofu hawafiki hata thelathini hapa Tanzania.Ila kanisa la Gwajima linatisha kwa wingi wa maaskof.Haya bhana tutafakari tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…