Maaskofu waache kutuchanganya

Dopas

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2010
Posts
1,151
Reaction score
392
Hivi karibuni liliotolewa tamko la jukwaa la kikristo, na kusainiwa na viongozi wahusika, wakiwakilisha TEC, ELCT, PCT.
Baada ya hilo tamko tunasikia maaskofu wengine moja moja wakitoa matamko yao kupingana na hilo tamko.

Huo ni unafiki mkubwa, na ni aibu kwa viongozi wa dini kuwa mnafiki. Tunaamini tamko lililoletwa kwetu na viongozi wao ni tamko lao sote, kama walikuwa na maoni yao binafsi walipaswa kuyatolea kwenye vikao vyao. Sio busara hata kidogo tamko ambalo sisi tunalichukulia la kikundi, hata kama wote hawakuliafiki kati yao, kwa vyovyote wengi wao waliliafiki, ndiyo maana imeletewa mbele yetu kama tamko la pamoja.

Ajabu askofu anajitoa kutohusika eti kwa kusema alikuwa sijui sherehe, au matibabu.

Ni ajabu kwani hata kama hakuweza kuhudhuria kikao hicho kilichotoa maamuzi, kwa vyovyote alipata nakala, na hata kama hakupewa nakala, anajua mawasiliano ya bosi wake, yaani mwenyekiti wa baraza, sasa iweje aende mimbarini badala ya kuhubiri neno la Mungu anaanza kupingana na tamko, ambalo kimsingi ni halali.

Kama ni halali mwingine kumfundisha mtu kusema "ndiyo" kwanini isiwe halali mwingine kumwambia ajibu "hapana"?
Nasema tu maaskofu muache kutuchanganya, mkitaka kutoa tamko tofuati mkae tena na mlete kupitia viongozi wenu halali kama mlivyofanya siku zote.
 

Maaskofu gani unawasema waliopinga. Hao kawaulize wamechaguliwa na mamlaka gani-self proclaimed bishops!
 
pengo hajapinga katoa maoni yake...........
 
pengo hajapinga katoa maoni yake...........
Maoni yake hayo akatolee kwenye vikwao vyao, amepingana na tamko kwa maana ya kupinga lililowakilishwa na viongozi wao
 
Wanaopingana na tamko la Jukwaa, wakiongozwa na Pengo

Pengo hakuwapinga ametoa maoni tu. Lakini naye Pengo anasahau kuwa anahubiri madhabahuni tufanye mambo fulani. Si atuache tuamue wenyewe? Kwa nini huwa anapoteza muda wake kutoa mahubiri. Si aache tusome wenyewe biblia?
 
Mkuu maaskofu walisha maliza kazi yao na anayepinga angepinga kwenye kikao sio nje coz lazima kabla ya uamuzi kilikalika kikao chao maaskofu.....
 

Mkuu wewe si unaakili zako mpaka usikilize matamko ndio ujue nini cha kupigia kura? Kama mimi hata bila tamko kwa nilivyouona mchakato tangu mwanzoni ukikosa uhalali wa kisiasa, na mambo muhimu kuenguliwa kura yangu ni ya HAPANA
 

Usiachanganyikiwe hawa maaskofu wengine ni waganga njaa tu tamko tunalolitambua nilile lililosainiwa na viongozi wetu nakusomewa makanisani.
 
Mkuu wewe si unaakili zako mpaka usikilize matamko ndio ujue nini cha kupigia kura? Kama mimi hata bila tamko kwa nilivyouona mchakato tangu mwanzoni ukikosa uhalali wa kisiasa, na mambo muhimu kuenguliwa kura yangu ni ya HAPANA
Ni kweli ila kwa katiba hiyo yenye mkanganyiko mwingi, ukizingatia kuwa sio wote watakaoweza kuisoma na kuielewa, tamko la viongozi wetu, ambalo kimsingi tunaamini wanatoa kwa manufaa yetu, inasaidia.

Kiongozi yeye ambaye amewakilishwa na wale wenyeviti watatu, akizungumza pembeni, eti ni maoni yake tu mi namwona mnafiki. Maoni yake tu atolee kwenye vikao vyao yawakilishwe kwetu na tamko lao. Kama kusingekuwa na tamko lolote, au wangotoa maoni yao kabla ya tamko, hapo sawa
 
Maaskofu nao ni wachungaji Wa watu kama wanaona jambo linaenda mrama kwanini wasikemee,wew unafikiri wasipoongea mfano watu toka mikoa ya Tanga,lindi,Dar ,pwani,Dodoma na singida na monduli kwao Lowassa na jamii nzima ya kimasai,watapiga Kura ya ndiyo kwenye katiba make elimu Yao na kupenda ccm walishatambikiwa watatupoteza kwenye ktiba
 
Hawa vijiaskofu wengine wanaopinga tamko hilo ni wale ambao walishapewa BAHASHA ZA KAKI, na ukiwafuatilia sana sio hata maaskofu wanaoeleweka, ni wa kujipachika. Tamko la Maaskofu ni halali kabisa, na ningeomba waendelee kuwaelimisha waumini wao dhidi ya mashwetani hawa wa CCM wanaofanya upotoshaji katika katiba yao walioitunga wenyewe kwa maslahi yao binafsi..
 
Viongozi wa ccm pamoja na Pengo mnatakiwa kuacha kuwapotosha wananchi tamko la maaskofu lilipata Baraka zote za maaskofu ni tamko lenye nia njema kwa watanzania kuhusu kuipigia kura ya HAPANA katiba ya ccm.
 
Pengo anatumiwa na ccm kuwapotosha wananchi.
 
Hakuna wanaopingana,hao wanaoropoka wametengenezwa na seriakli ya ccm,lakini wakae wakijua tamko la tasisi kama tec,cct,pcf n.k hivyo,hao wanaobwabwaja wanapoteza muda pengo hayumpo juu ya tec ni maaskofu kama maaaskofu wengine,seriakloi iendelee kutengeneza propaganda lakini waraka ndio utakao somwa kanisani.
 
umenena vyema sana mkuu elimu inahitajika sana.
 

Epuka kuhusisha siasa na mambo ya dini wewe.
 
Asante Maaskofu kwa kuhimiza waumini wenu kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kupata civic education. Pia nikushukuru binafsi Mwadhama P.C Pengo kwa kuwafungua macho maaskofu wenzako kuwa hamna mamlaka ya kuwalazimisha waumini kufanya au kutokufanya jambo. Kweli Pengo umesoma na ukaelimika. Ndio maana umechambua waraka wenu kiusomi. Na Mashekh wenzangu tuige mfano wa Pengo kuwahimiza ndugu Waislam kuisoma Katiba Inayopendekezwa na hatimaye kuipigia kura kadri ulivyoielewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…