Hivi karibuni liliotolewa tamko la jukwaa la kikristo, na kusainiwa na viongozi wahusika, wakiwakilisha TEC, ELCT, PCT.
Baada ya hilo tamko tunasikia maaskofu wengine moja moja wakitoa matamko yao kupingana na hilo tamko.
Huo ni unafiki mkubwa, na ni aibu kwa viongozi wa dini kuwa mnafiki. Tunaamini tamko lililoletwa kwetu na viongozi wao ni tamko lao sote, kama walikuwa na maoni yao binafsi walipaswa kuyatolea kwenye vikao vyao. Sio busara hata kidogo tamko ambalo sisi tunalichukulia la kikundi, hata kama wote hawakuliafiki kati yao, kwa vyovyote wengi wao waliliafiki, ndiyo maana imeletewa mbele yetu kama tamko la pamoja.
Ajabu askofu anajitoa kutohusika eti kwa kusema alikuwa sijui sherehe, au matibabu.
Ni ajabu kwani hata kama hakuweza kuhudhuria kikao hicho kilichotoa maamuzi, kwa vyovyote alipata nakala, na hata kama hakupewa nakala, anajua mawasiliano ya bosi wake, yaani mwenyekiti wa baraza, sasa iweje aende mimbarini badala ya kuhubiri neno la Mungu anaanza kupingana na tamko, ambalo kimsingi ni halali.
Kama ni halali mwingine kumfundisha mtu kusema "ndiyo" kwanini isiwe halali mwingine kumwambia ajibu "hapana"?
Nasema tu maaskofu muache kutuchanganya, mkitaka kutoa tamko tofuati mkae tena na mlete kupitia viongozi wenu halali kama mlivyofanya siku zote.