Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Ukumbi wa Kimataifa Wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC)- Dar es Salaam
AZIMIO LA JUMLA
Kongamano limeazimia kuipongeza serikali ya awamu ya sita kwa hatua kubwa iliyochukuliwa kupanua uhuru wa vyombo vya habari na kufungua milango ya mazungumzo na wadau wa habari kuhusu ukuaji wa sekta ya habari
Kongamano limeazimia kumpongeza Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh Nape Nauye kwa kuwa karibu na sekta ya habari na kufanya kazi usiku na mchana kulinda na kutetea uhuru wa habari na maslahi ya waandishi wa habari na sekta nzima ya habari.
MAAZIMIO YA SERIKALI
Katika kulipa sura mpya kongamano la maendeleo ya sekta ya habari serikali imeazimia kulipa hadhi ya kimataifa na kuliita‘KONGAMANO LA KITAMATAIFA LA MAENDELEO YA SEKTA YA HABARI’ na litakuwa linafanyika kila mwisho mwa mwaka kuanzia 2023.
Kuhusu kulinda uhuru wa vyombo vya habari nchini, serikali imeazimia kuendelea kusimamia uhuru wa vyombo vya habari ikiamini katika falsafa ya mambo makuu matatu kuwa hakuna maendeleo, furaha na amani bila uhuru.
Suala la maslahi na mikataba bora kwa waandishi wa habari limekuwa tatizo sugu kwa miaka mingi. Kutokana na kilio hiki cha muda mrefu serikali imeahidi kuanzia mwaka 2023 itaweka nguvu kubwa kushughulikia suala hili ili kulinda haki na maslahi ya waandishi wa habari kwa kuwawezesha kupata mikataba bora ya kazi.
Katika kulinda tunu za taifa, serikali imeazimia kuendelea kufanya kazi na vyombo vya habari kwa kuviasa kufuata miiko, maadili, tamaduni taifa letu.
Serikali imeazimia kuupeleka Bungeni Mswada wa Huduma za Vyombo vya Habari Januari 2023. Serikali pia imeazimia kuendelea kufanyia mabadiliko ya sheria na sera nyingine mfano Sera ya Utangazaji 2003 ili kuona uwezekano wa kuwa na sheria moja inayosimamia sekta habari
Serikali imeazimia kuboresha mazingira ya upatikanaji wa taarifa ili kuhakikisha wakati huu wa TEHAMA taarifa zinawafikia wananchi kwa wakati.
MAAZIMIO YA KONGAMANO
Kongamano limekubali azimio la serikali la kulifanya kongamano la maendeleo ya sekta ya habari kuwa la kimataifa kuanzia mwakani ( 2023)
Katika kutetea maslahi ya waandishi wa habari kongamano limeazimia kuhamasisha waandishi wengi kujiunga na vyama vya wafanyakazi kwa mfano Chama cha Wafanyakazi Wanahabari Tanzania (JOWUTA) ili kuvipa nguvu za kuwatetea pale wanapopata matatizo wakiwa kazini.
Kongamano limeazimia kuundwa kwa Bodi ya Wanataaluma wa Habari ili kulinda maadili ya sekta ya habari na mawasiliano.
Kongamano limiazimia kuwa serikali isaidie kuondoa gharama za kutandaza masafa ya mkongo wa taifa ili kupunguza gharama za mawasiliano kwa vyombo vya habari.
Kongamano limeazimia serikali iendelee kushughulikia kulipwa kwa deni la matangazo kwa vyombo vya habari
Kongamano limekubaliana kuwa uhuru wa vyombo vya habari utalindwa kupitia mabadiliko ya sheria yanayoendelezwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mh Rais Dr. Samia Hassan Suluhu.
Kongamano limeazimia kuwepo kwa mafunzo ya ndani na nje ya vyombo vya habari ya umahiri wa lugha ili kuboresha ubora wa maudhui yanayozalishwa na kuongeza wigo wa ajira kwa wandishi katika soko na la ndani na kimataifa.
Kongamano limeazimia kuwepo majadiliano endelevu kati ya wadau na taasisi/idara za serikali kuboresha mazingira ya utendaji kazi wa waandishi
Kongamanio limeazimia TCRA kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za ubora wa viwango isimamie ubora wa vifaa vya urushwaji wa matangazo vinavyonunuliwa na wamiliki wa vyombo vya habari ili kuboresha usikivu wa habari.
Kongamano pia limezimia kutumia fursa za mitandao ya kijamii ili kukuza taaluma na uchumi wa mwandishi mmoja mmoja na wa vyombo vya habari.
Kongamano limezimia kuundwa kwa tume/kikosi ama kuwepo na mjadala utakaoangazia maudhui ya tamthilia na michezo ya kuigiza za ndani na nje ili kulinda maadili kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Kongamano limekubali kwa pamoja kuunga mkono ombi la kampeni ya Umoja wa Mataifa kuchukua hatua dhidi ya ndoa za utotoni na kumtetea binti ili aweza kutimiza ndoto zake.
Kongamano limeazimia vyombo vya habari kuwekeza katika habari zenye tija na kuleta suluhu kwa matatizo ya wananchi ili kuwa na matokeo chanya kwa taifa.
Katika kuondokana na ‘fake news’ serikali ihusishe na kushirikisha vyombo vya habari kufika katika vyanzo halisi vya habari.