Mabachela wenzangu, mnapika vyakula gani vya haraka haraka?

Uzi wa vyakula we unatuletelea stori za kufua! Umevurugwa?
 
Mbiga usioshe baada ya kuikatakata, unaondoa viinilishe. Ioshwe kabla
 
nunua box la tambi, weka getto.

kutoka mishe, chap chemsha maji toa hapo vikombe viwili vya chai

then tia chumvi kijiko cha chai nusu, weka tambi kiasi chako, dak 5 toka chuja maji kama yamepaki.

then weka mafuta kidogo kwa sufuri then unga tambi zako kwa suka au nyanya na kitungu (utakavyo penda siku io)

and that's it.

#chai na tambi
 
Vyakula visivyo na mlolongo mrefu wa kuandaa na vyombo vichache sana vitumike. Nimechoka ubwabwa (wa rice kuka)/tambi/ugali na nyama au mainiau mchemsho. Vitu gani vingine huwa mnapika?

Asanteni
Bamia ,unachukua nyanya na kitunguu ,unakaanga kama dakika tano hivi unalumangia na sembe lako na samaki wa gengeni kama kilainishi
 
Nachemsha ndizi, napitia na samaki kwa mama Nyemo, mchana umepita.
 
Dah.... Utakuwa unakula viporo maisha yako Yote. Hatari Sana πŸ˜€
 
Ugali na mayai..
Unapiga ugali, unapika mayai. Ugali unalia kwenye sufulia na mayai unachanganya umo umo.. Flampeni kwa mwezi inaoshwa mara moja sababu huwa haichafuki.
Unakuwa na kazi ya kuosha sufulia tu
Tabia yangu hii[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…