SoC03 Mabadiliko baadhi ya Sekta

SoC03 Mabadiliko baadhi ya Sekta

Stories of Change - 2023 Competition

Mwelekete

New Member
Joined
Jul 23, 2023
Posts
1
Reaction score
0
Kwenye nchi Kuna baadhi sekta inatakiwa zibadilike kimuundo na uendeshaji, na viongozi wetu hususani watunga sheria hawako tayari kuunda mifumo inayochochea uwajibikaji (viongozi wengine siyo wawajibikaji kama wanavyodai). Kuna baadhi ya sekta zikiundwa zitaleta utawala bora na uwajibikaji.

Mawaziri wasiwe wanasiasa yaani wasitokane na ubunge badala yake watokane na waombaji kama ajira nyingine zinavyoombwa kuzingatia taaluma na ujuzi wa mambo ya wizara husika. Kwa mfumo wa sasa waziri anateuliwa kwa ajili ya kusimamia wizara ambayo hana uzoefu na pengine hasomea kabisa kile anachosimamia yaani hajui chochote, yeye ndiyo anaanza kujifunza badala ya kwamba alete ujuzi. Kwa mfano waziri wa kilimo atokane na wataalam wa kilimo na ikiwezekana awe mbobevu kwenye kilimo.

Mtumishi akipatikana na hatia awajibishwe kisheria na siyo kumhamisha kituo, hali hii inadumaza sana maendeleo ya nchi na uwajibikaji. Hapa serikali haiwajibiki sana na inaonekana watumishi wanalindana na wanachi hawana sehemu ya kuaminika kwa ajili ya kutatua changamoto hii. Na bila shaka kuna sheria ambazo zipo kwa ajili ya uwajibikaji kwa watumishi na wananchi ziangaliwe upya.

Wakurugenzi wa wilaya na mikoa wasiwe wateule wa Rais,Kuna baadhi ya miladi mingi inakwama kwa sababu ya hao wakurugenzi hawana uwajibikaji ndani yao au hawana taaluma/uzoefu na kila wanachotakiwa kukifanya. Pia hawana mtu wa kuwawajibisha isipokuwa tu aliyemteuwa yaani Rais. Ikiwezekana Rais apunguziwe mamlaka ya kuteua waajiriwe kwa kuzingatia taaluma na uwezo wao.

Serikali au nchi iandae mpango kazi wa kudumu na siyo kufuata mtazamo wa Rais anayekuwepo madarakani. Hili mara nyingi linazungumzwa sana na baadhi ya viongozi mojawapo ni Mheshimiwa Josephat Ngwajima mbunge wa Kawe na sina uhakika kama kweli viongozi wengine mamlaka wanamuelewa vizuri, na kama wanamuelewa wana mpuuzia. Suala hili linakwamisha nchi kuendelea kwa sababu kila kiongozi anayekuja anakuja na mtazamo wake.

Kwenye teuzi mbalimbali zizingatiwe sifa au taaluma ya atakaye teuliwa. Mtu ana teuliwa ili kumsaidia kiongozi na kumuwakilisha kwa niaba yake kwenye mambo mbalimbali yanayohusu utawala bora, maendeleo na uwajibikaji. Wengine wanateuliwa ni kwa ajili ya kuwepo pale na siyo kuwajibika, kwa mtazamo wangu naona vigezo vizingatiwe ili kupata utawala bora na uwajibikaji. Kwa mtu anateuliwa akasimamie michezo na yeye siyo mwanamichezo inawezekanaje?

"Vijana taifa la kesho" kauli hii isitumike tena, kauli hii husemwa sana na baadhi ya viongozi wetu kitu ambacho ni kuwapumbaza vijana wajione muda wao bado na kuwadumaza kifikra na uwajibikaji. Pia kauli hii ina uchoyo wa madaraka na fulsa mbalimbali kwa vijana. Vijana tuwajibike tusikubali kutumika vibaya na viongozi wetu hususani wanasiasa.

Pia kauli hii inakaukatili kwa vijana ndani yake inatakiwa tuikatae kwa nguvu zetu zote kwani ikitokea nchi imevamiwa ni vijana watakuwa msitari wa mbele kuilinda na kuipambania na siyo wazee. Pia hata vyombo vya habari vihamasishe vijana kujitambua na kuwajibika bila kusahau kupambana na kauli kama hizi ambazo zinadumaza fikra za vijana kwenye dhana ya uwajibikaji.

Kila kampuni au taasisi ichukue na iwajibike kisheria kuwapa uzoefu wahitimu mbalimbali wanaohimu vyuo kwani mwishowa siku wanaulizwa uzoefu pindi wanaomba kazi. Imekuwa ni kawaida sana kijana au mtu yeyote anapoomba kazi kuulizwa uzoefu na mara nyingi kama una taaluma na huna uzoefu kazi hupati na kazi hupati utapataje uzoefu? Ikiundwa sheria ya kuzibana taasisi au makampuni itachochea uwajibikaji kwa taasisi na wahitimu wa vyuo mbalimbali.

Mitaala ya elimu yetu iundwe upya, kwa sasa elimu yetu imejikita zaidi kuajiriwa na siyo kujiajiri. Kwa mfano ukiachana na ufundi stadi, mtu anasomea biashara (business administration) lakin hayupo tayari kuanzisha au kusimamia biashara yake badala yake analenga kuajiriwa na kampuni au taasisi ili apate mshahara. Si vibaya kuiga kwenye nchi ambazo tunaweza kujifunza kwenye jinsi ya kuunda mitaala itakayofanya muhitimu kuwajibika kwa kuzingatia mazingira yetu. Kuna baadhi ya nchi kama Japan, China nakadhalika kuna uwajibikaji mkubwa wa wanachi na viongozi wao.

Jaji mkuu asiwe mteule wa Rais badala yake atokana na wanasheria au chama cha wanasheria, kwa sasa jaji hana uhuru wa kumuwajibisha kisheria endapo kiongozi atafanya kosa lolote kwa kuwa ni mteule wake. Kwa hiyo inagekuwa vema sana kama jaji angepatikana kama anavyopatikana spika kwa kupigiwa kura ili aongoze bunge. Hili litachochea uwajibikaji na uzalendo ndani yake.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom