SoC02 Mabadiliko (change)

SoC02 Mabadiliko (change)

Stories of Change - 2022 Competition

Ibrahimeliza

Member
Joined
Nov 25, 2020
Posts
37
Reaction score
26
Habari za wakati huu msimamizi(moderator), habari za wakti huu washiriki na wanachama wenzangu wa jamii forum,Madada,Wakaka,Vijana,Wazee,Marafiki na Maadui.
Leo napenda kuzungumzia MABADILIKO kidogo sio sanaa kwa kadiri nilivyojaaliwa.

Mabadiliko hayakwepeki, mabadiliko ni sehemu au kitu ni muhimu katika maisha yetu. Hii namaanisha kila kitu katika maisha yetu kinapitia mabadiliko iwe kiumbe hai au sio kiumbe hai, mabadiliko ni kama KIFO lazima, hakuna anaeweza kuzuia mabadiliko au kupinga mabadiliko.

Namaanisha nini ninaposema mabadiliko, namaanisha kwamba kwenda kinyume na mfumo wako wa kawaida au kufanya tofauti na ulivyozea au namna ya mfumo wako ulivyo, mfano wewe ni kijana haujaoa au kuolewa kisha ukaamua kuoa au kuolewa hayo ni mabadiliko makubwa katika maisha yako kutoka kuishi peke yako kulala peke yako sasa unakula, kulala na kuishi na mtu, Mabadiliko yanatokea kila nyanja katika maisha yetu ; kazini, shuleni, vyuoni, serikalini, mtaani, katika kila taasisi kuna mabadiliko na sio hayo ya njee hadi katika miili yetu kunamabadiliko, namaanisha mabadiliko ya kifikra, mtazamo, kufikiria, lakini pia athari za moja kwa moja katika mwili kutoka kwenye kitambi mpaka (six pack) hayo ni mabadiliko, vipi kuhusu kubalehe...?? Sio mabadiliko...?? Jibu ni mabadiliko hauwezi ukawa kijana mpaka upite katika hatua ya kubalehe, kila mtu humu kapitia mabadiliko hayo ni lazima kupitia, embu ngoja kunamtu hajapitia humu ....??? Kama nilivyosema mabadiliko ni lazima, lakini changamoto za mabadiliko ya kubalehe kila mtu anazijua na huu ni mfano mdogo sanaaa wa mabadiliko, kupitia mabadiliko hayo kuna wanaojuta maisha yao yote na kuna walionufaika na mabadiliko hayo kwakujua au kwakutokujua mabadiliko lazima yatakuathiri.

Mabadiliko yanazalisha watu wa aina nne(4).

Kwanza;

Kuna watakao angalia TU mabadiliko yakitokea; hapa namaanisha kuna watu wasiojua wala kufuatilia chochote kile yani hajui chochote kuhusu jamii yake wakati mwingine hajui pia hata kuhusu familia yake, mpaka kitu kinampita hajui.

Pili;
Kuna wanaoshiriki kwa kuongea TU.

Hapa namaanisha hawa ni wale ambao wanajua na wanaona mabadiliko katika familia zao na jamii zao lakini hatua ya mwanzo na ya mwisho wanaochukua ni kuongea tu, kunapohitajika mabadaliko basi atatumia mdomo wake kurekebisha panapohitajika.

Tatu;
Kuna wanaoshiriki kwa vitendo.
Hawa ni wale wanaoshiriki moja kwa moja katika familia zao na jamii zao, yani wanatumia midomo na mikono yao, kitu cha msingi hapa "Kuongea sio ndo kutenda ila kutenda kunajumuisha na kuongea", unaweza kutumia mdomo kwakutenda.

Nne,.
Wafanya mabadiliko.

Hawa ni wale wanaona vitu vinatokea kisha wakashiriki kwa kuongea bali hawakuishia hapo wakafanya mabadiliko kwa mikono yao.

Sio kila mabadiliko ni mazuri au yanafaa katika familia yako au katika jamii yako, lakini tatizo ni kwamba bila mabadiliko watu hawakui na vitu vitabaki vilevile, bila mabadiliko hatutaweza kumudu changamoto, bila mabadiliko hatutakua kiuchumi, bila mabadiliko hakuna maisha, kama hakuna maisha ni nini tena....??

Tujaribu kujiuliza maswali haya, maswali ambayo yatajaribu kubalisha mitazamo yetu na fikra zetu kiujumla, kila mtu ajaribu kujiuliza haya maswali sio lazima uyajibu kwakuandika ukiwa na majibu kichwani mwako inatosha, huenda ndoikawa chanzo cha mafanikio yako binafsi na nchi kiujumla, lakini haya maswali yakijibiwa vibaya au kutumika vibaya ndo chanzo cha matatizo yote binafsi na ya nchi, ndo chanzo cha rushwa, ndo chanzo cha ubinafsi, ndo chanzo cha shida na malalamiko yote haya kiujumla sio hilo tu naamini upo jamii forum kwaajili ya maswali haya.....................!!
MASWALI

1) Mimi ni nani.....???

Watu wengi wanaogopa kujiuliza hili swali, ni swali linaloshtua mishipa na fahamu za kujitambua.

2)Natokea wapi....???
Ndiyo, unatokea wapi ukishajua ulipotokea utajua utakapokwenda.

3)Kwanini nipo hapa....???
Hili swali linamaanisha malengo yako, unataka nini..?? Unahitaji vitu gani...?? Unahitaji watu wa aina gani...??

4)Nifanye nini....???
Inatakiwa iwe hivi, ninauwezo wa kufanya nini...?? Au naweza kufanya kitu gani....??

5)Naelekea wapi....???
Unataka kwenda wapi ...??

Husipojua wewe ni nani hautojua umetoka wapi na husipojua umetoka wapi, Hautojua kwanini upo hapa na husipojua kwanini upo hapa hautajua cha kufanya, na husipo jua chakufanya hautajua pakuelekea.

Hauwezi kubadilisha kitu husichokielewa na hakuna jambo litakaloweza kubadilika bila kuamua katika akili yetu kama tunataka mabadiliko, tukishaamua tufanyie kazi vilivyopo kwenye fikra zetu. Haitakuwa rahisi ila utaweza kuvumilia maumivu ya mabadiliko ..??


Ahsanta🇹🇿✉💼
 
Upvote 0
Back
Top Bottom