Elimu ni sekta umuhimu ya kijamii katika kuchochea maendeleo ya ukuaji wa jamii ambapo inahusisha utoaji wa maarifa,ujuzi na mafunzo mbalimbali kuhusu maadili na stadi za maisha, sasa na utawala bora, ufundi na shughuli mbalimbali za kiuchumi Kama vile kilimo, ufugaji, uvuvi na biashara kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utendaji kazi pili kukuza pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alikuwa mtetezi mkubwa Sana wa elimu nchini Tanzania na alitambua umuhimu wa elimu kwa maendeleo ya nchi. Alisisitiza juu ya elimu jumuishi ya haki na usawa kwa wote,alitambua kwamba elimu ni umuhimu katika kujenga Taifa lenye maendeleo na maadili mema.
Kulikuwa na jitihada kubwa za kuanzisha elimu ya msingi kote nchini lakini pia alisisitza umuhimu wa kutoa elimu kwa watu wazima. Mwalimu Nyerere aliendeleza falsasa ya"Ujamaa na Kujitegemea",ambayo iliongoza Sera ya elimu nchini Tanzania.
Wizara ya elimu,utamaduni,sayansi na teknolojia ni chombo maalumu nchini Tanzania ambacho kina majukumu na dhamana ya kuratibu na kusimamia shughuli zote za elimu nchini katika kuhakikisha huduma bora ya elimu inapatikana kwa watu wote, miongoni mwa majukumu ya wizara ni kufanya mabadiliko ya mitaala ya elimu nchini, mfano mwaka 1974 wizara ya elimu ilianza maboresho na mabadiliko katika kuongeza muda wa elimu ya msingi kwa miaka 7 ,serikali iliamua kutoa elimu ya msingi kwa miaka 11 badala ya miaka 7 iliyokuwa swali.
Hii imesaidia kupunguza kiwango cha watoto wanaoacha shule kabla ya kumaliza elimu ya msingi,pia kuanzisha mpango wa elimu bure,serikali ilianzisha Sera ya elimu kwa wanafunzi wa msingi lakini sasa hivi hadi kidato cha sita.
Kutokana na mabadiliko ya elimu yaliyofanywa lakini elimu ya Tanzania inapoteza ubora wake kila siku kutokana na Changamoto mbalimbali za sekta ya elimu, miongoni mwa changamoto changamoto hizo ni kama vile
Mitaala ya elimu iliyopitwa na wakati ambayo haikizi mahitaji ya sasa katika ushindani wa solo la ajira na maisha ya sasa kwa sababu mfumo wa elimu wa elimu unazingatia zaidi katika kumkaririsha mwanafunzi afaulu mitihani na kusahau ufundishaji wa ujuzi wa stadi umuhimu za kazi na maisha katika jamii,pia upatikanaji mdogo wa vifaa vya kufundishia
Shule nyingi nchini Tanzania hazina vifaa vya kisasa vya kufundishia Kama vile kompyuta, maabara, vitabu na vifaa vya kufundishia sayansi, vile vile miundombinu duni ya shule pamoja madarasa, viti, meza na madawati yaliyoharibika,ukosefu wa maji safi na salama,uhaba wa matundu ya vyoo na nyenzo mbalimbali za kufundishia.
Katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za elimu nchini, serikali ya Tanzania kupitia wizara yake ya imekuwa ikishirikiana kwa ukaribu katika kufanya mapendekezo ya maboresho na marekebisho mbalimbali kwa kuratibu sheria, kanuni na taratibu mbalimbali za kuendesha elimu nchini sambasamba na mabadiliko chanya yanayotakiwa kufanyika katika elimu.
Maana halisi ya mabadiliko chanya katika elimu ni kuwa na marekebisho na maboresho katika mfum wa elimu,l engo la mabadiliko haya ni kuongeza ubora na ufanisi wa hali ya juu katika sekta ya elimu nchini,kwa mfano mabadiliko chanya ya katika elimu yanaweza kujumuisha upatikanaji wa vifaa bora vya kufundishia na teknolojia ya kisasa, maboresho katika mitaala ya masomo,kuongeza ushirikiano Kati ya walimu na mwanafunzi na kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu bora.
Katika kusisitiza mabadiliko chanya kwenye sekta ya elimu ,serikali haina budi kusimamia uwajibikaji na utawala bora katika elimu katika kuwa na mfumo na utaratibu unaohakikisha uwajibikaji na utawala bora kwa kila mshiriki katika sekta ya elimu. Hii ni pamoja na watendaji wa serikali;walimu,wafanyakazi wa shule, wanafunzi, wazazi na jamii kwa ujumla.
Lengo kuu la uwajibikaji na utawala bora ni kuhakikisha elimu inayotolewa ni bora na inakidhi mahitaji ya mwanafunzi na jamii kwa ujumla,Mifano ya taratibu za uwajibikaji na utawala bora zinaweza kujumuisha mambo Kama vile;-
(i) Kusimamia vizuri ufadhiri na matumizi ya fedha za elimu ilikuhakikisha uwajibikaji,uwazi na utawala bora.
(ii) Kuimarisha utaratibu wa kufuatilia matokeo ya kidato cha pili hadi cha sita katika ngazi ya shule, kata,wilaya,mkoa na Taifa kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora.
(iii) Kusimamia na na kuhakikisha utekelezaji wa Sera na mikakati mbalimbali ya elimu kwa ajili ya kufikia malengo ya elimu ya Taifa.
(iv) Kupitia na kuboresha utawala wa shule na kuhakikisha madarasa,vifaa vya kufundishia na rasilimali zinapatikana na kutumika vizuri.
(v) Kuweka mifumo ya uwajibikaji kwa walimu na wafanyakazi wengine wa elimu ili kuhakikisha kuwa wanatekeleza kikamilifu majukumu yako.
(vi) Kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa elimu na kushirikisha wazazi,walezi na jamii nzima katika kujenga mazingira mazuri ya elimu.
(vii) Kusaidia na kusimamia mafunzo na maendeleo ya walimu ili kuwawezesha kufundisha kwa ufanisi zaidi na kubaki katika kiwango cha ubora wa elimu.
(viii) Kuweka na Kusimamia utaratibu wa tathmini ya ubora wa elimu na ufuatiliaji wa matokeo ya wanafunzi na kuchukua hata za kuboresha pale inapobidi.
(ix) KuKukuza na kusimamia teknolojia ya habari na mawasiliano(TEHAMA) katika elimu ili kuboresha mchakato wa kufundisha,ujifunzaji na utawala wa elimu.
(x) Kuendeleza na kutekeleza Sera na na mikakati ya kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora kwa watoto wote,wakiwemo wale wa makundi maalumu Kama vile watoto wanaoishi katika mazingira magumu,wenye mahitaji maalumu na watoto wa kike.
(xi) Kusimamia vyanzo vya fedha za elimu na kuhakikisha matumizi ya fedha hizo yanafanyika kwa uwazi na ufanisi.
(xii) Kukuza na kusimamia ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika kuboresha elimu,ikiwemo wazazi,jamii,na mshirika ya kiraia na sekta binafsi.
(xiii) Kuendeleza na kusimamia utafiti na tafiti za elimu na kiufundi kwa lengo la kuboresha elimu na kukabiliana na changamoto zinazijitokeza katika sekta ya elimu.
(xiv) Kusimamia ubora wa elimu kwa kuhakikisha viwango vya ufundishaji vinazingatiwa na kutekelezwa kwa ufanisi .
(xv) Kupitia na kuhakikisha ubora wa vyuo vya elimu ya juu na taasisi zinatoa mafunzo ya kiufundi na ufundi(VETA).
(xvi) Kuendeleza na kusimamia mifumo ya upimaji na tathmini ya wanafunzi katika ngazi ya mbalimbali za elimu ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu inayofaa au kukidhi viwangi vya kitaifa na kimataifa.
(xvii) Kutoa semina,warsha na mafunzo kwa walimu,wakufunzi na wadau wengine wa elimu ili kuboresha mbinu za ufundishaji na ujifunzaji.
(xviii) Kushirikisha wadau wa elimu Kama vile wazazi,jamii na sekta binafsi katika kuboresha elimu na kutoa mwongozo na ushauri kwa wadau mbalimbali.
(xix) Kufuatilia mwenendo wa elimu kwa kutumia takwimu na taarifa zinazotolewa na taasisi zinazohusika na elimu, na kutumia taarifa hizo kufanya maamuzi.
Mwisho
Kutokana na jitihada mbalimbali zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano katika sekta ya elimu kumesaidia Sana katika kuboresha mifumo mbalimbali ya elimu kupitia programu za ufadhiri wa masomo nchini za nje Kama vile China, Canada, Marekani,India na Uturuki, serikali imekuwa na mahusiano mazuri na nchini mbalimbali duniani katika kuunganisha nguvu kwenye upatikanaji wa huduma za elimu hususani maeneo ya vijijini na mijini lakini has a vijijini kwa sababu kuna changamoto Sana za elimu.
Kupitia jitihada hizi serikali ya Tanzania imepata fedha kutoka benki ya maendeleo ya dunia (World bank)kupitia mradi mkubwa wa maendeleo ya jamii (MDP).
Kupitia msaada wa fedha serikali ya Tanzania imeweza kuboresha miundombinu ya shule kongwe nchini Kama vile Kibasila, ujenzi wa shule mpya katika kila wilaya,kununua magari ya afisa elimu wa shule za msingi ili kufuatilia maendeleo ya elimu katika vituo vyao vya kazi, kusimamia na kuratibu mpango wa elimu bure na kuboresha miundombinu ya ujifunzaji wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari nchini.
Haya ni matokeo makubwa Sana yaliyofanywa katika awmu ya tano kutokana na kusimamia misingi imara ya utawala bora na uwajibikaji kwa watendaji wakuu na wasaidizi wa elimu nchini ili kutimiza maagizo na sera ya Baba wa Taifa katika kupambana vita dhidi ya ujinga kwa kusimia Sera za Serikali ya kufuta ujinga na kutaka kila mtanzania awe anajua kusoma na kuandika.
Katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la wasomi na wataalamu mbalimbali waliobobea katika masuala mbalimbali ya afya,mafuta na gesi, uhandishi, habari na teknolojia sasa na utawala bora, hali hii imechochea ukuaji wa haraka wa maendeleo ya Tanzania ukilinganilisha na awamu zilizopita, hivyo basi kumesaidia sana kuwepo kwa ushondani mkubwa Sana katika solo la ajira nchini.

Upvote
1