SoC02 Mabadiliko chanya katika Sekta ya Afya kwa sasa Tanzania

SoC02 Mabadiliko chanya katika Sekta ya Afya kwa sasa Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Glady michael

Member
Joined
Aug 9, 2022
Posts
13
Reaction score
13
Huduma za afya ni zile huduma ambazo hutolewa kwa wananchi kupitia asasi za kiserikari na mashirika binafsi katika kurefusha maisha, kuzuia magonjwa na kusaidia watu kupata afya nzuri na bora.

Tanzania ni nchi ambayo ilikuwa dhaifu katika upatikanaji wa huduma za afya hii ni kutokana na changamoto mbalimbali zilizoikumba Tanzania. Hivyo katika karne hii ya 20 miaka ya sasa kuna mabadiliko kadhaa ambayo yamejitokeza kutokana na Maendeleo ya sayansi na Teknolojia. Mojawapo ya mabadiliko haya katika sekta ya afya ni:-

1. Kuimarika na kuongezeka kwa vituo vya kutolea huduma ya afya. Miaka ya nyuma kulikuwa na uhaba wa vituo vya afya sehemu mbalimbali hasa vijijini ambapo watu walilazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hata wagonjwa wengine kufia njiani. Na hata wajawazito walilazimika kujifungulia nyumbani badala ya hospitalini. Pia hata mijini kulikuwa na vituo vichache sana vinavyotoa huduma vizuri hasahasa hospitali binafsi. Lakini kwasasa tunaona mabadiliko katika sekta hii kwani kuna vituo vingi kuanzia zahanati ya kijiji, zahanati ya kata, hospitali ya wilaya, na hospitali za mkoa na taifa.

2. Kuimarika na kuongezeka kwa vifaa vya kisasa katika kutolea huduma hospitalini. Mabadiliko mengine ni kwenye vifaa vya kutolea huduma, ambapo miaka ya nyuma kulikuwa na uhaba wa vifaa kwenye hospitali za Serikali. Kwa mfano zamani wajawazito waliambiwa waje na vifaa vyao ili waweze kujifungua, au wagonjwa wengine hushindwa kupata huduma kutokana na vifaa kutokuwepo. Lakini kwasasa tunaona Serikali imejitahidi katika kuboresha vifaa na kuongeza zaidi ili watu wapate huduma kwa magonjwa mbalimbali. Kwa mfano kuna vifaa kama X-ray, ultrasounds, CT scan, MRI, colonoscopy, HBA 1C, ODG, USS, ECHO, na vifaa vingine vya kufanyia upasuaji wa magonjwa makubwa. Kwa mfano Muhimbili inajihusisha na upasuaji wa moyo kwasasa.

3. Upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya. Pia kwa sasa kuna mabadiliko katika upatikanaji wa dawa. Zamani vituo vingi vililazimika kuletewa dawa tu, na hii kusababisha kuwepo kwa uhaba wa dawa katika vituo vingi. Lakini kwasasa vituo vingi upatikanaji wake wa dawa ni mkubwa kwani wana uwezo wa kununua dawa wenyewe wanazoitaji pasipo kuletewa kama zamani na shirika la dawa (Medical Store Department).

4. Kuongezeka kwa wafanyakazi katika vituo vya afya kwa kuongeza kozi mbalimbali za afya vyuoni. Pia tunaona mabadiliko kati ngazi ya wafanyakazi. Miaka ya nyuma kulikuwa na wafanyakazi wachache sana ambao huchukua majukumu mengi kwa wakati mmoja na kusababisha ongezeko la watu na ucheleweshaji wa huduma kwa wananchi. Lakini kwa sasa Serikali imeongeza kozi mbalimbali vyuoni na watu kusoma katika ngazi hizo ili kupata wafanyakazi zaidi katika vituo vya afya. Tunaona kwasasa tukienda hospitali huduma zinafanyika kwa urahisi zaidi kutokana na wingi wa vyeo na kila mtu ana kazi yake. Chuoni kuna kozi kama vile BHRM( Bachelor Of Health System And Management) inayotolewa Mzumbe pamoja na BHIS ( Bachelor Of Health And Informations System) inayotolewa UDOM.

4. Kuwepo kwa mgawanyiko wa uongozi katika wizara ya afya. Pia kuna mabadiliko katika ngazi ya uongozi katika wizara ya afya kwani zamani hakukuwa na mgawanyo wowote na kusababisha kila kitengo kuwa na majukumu mengi au wizara kushikiria mambo mengi. Lakini kwa sasa Serikali imetoa mgawanyo wa uongozi ambapo kuna wizara ya afya, pia kuna mpya iliyoanzishwa kipindi hiki 2022 wizara ya ustawi wa jamii, pia hospitali za mikoa, kanda, na hospitali za Taifa zipo chini ya wizara. Pia hospitali za wilaya, kata, na zahanati za kijiji zipo chini ya TAMISEMI.

5. Kuwepo kwa matumizi ya Teknolojia katika utoaji wa huduma. Miaka ya nyuma kulikuwa hakuna Teknolojia katika utoaji wa huduma na wahudumu walilazimika kutumia nguvu zao katika kutoa huduma na wagonjwa kuzunguka mda mrefu hospitali ili kupata huduma. Lakini kwasasa Serikali imeleta mabadiliko katika utumiaji wa Teknolojia kwa kuweka mfumo wa GoT-HOMIS ambao ni mfumo wa kutumia komputa kuanzia mwanzo wa huduma hadi mwisho wa huduma na taarifa zake zikipitishwa kupitia komputa kutoka mapokezi hadi mwisho kuchukua dawa.

6. Kuwepo kwa mfumo wa afya wa kifedha na ushirikishwaji wa wananchi katika mfumo huo. Miaka ya nyuma hakukuwa na mfumo wa upatikanaji wa fedha katika vituo vya afya. Lakini kwasasa Serikali imeleta mfumo wa fedha ambapo mfumo huu kituo cha afya huingiziwa fedha moja kwa moja, mfumo huu unaitwa DHFF. Pia matumizi ya mfuko wa bima wa Taifa NHIF kwa wananchi ili kupunguza gharama kubwa na kuokoa muda hospitalini. Pia ushirikishwaji wa wananchi katika huduma ya afya kupitia HFGCs ( Health Facility Governing Committees) .

Hitimisho. Kwasasa Tanzania yetu ina mabadiliko kadhaa katika sekta ya afya tofauti na miaka ya nyuma na bado Serikali inazidi kuboresha miundombinu katika sekta ya afya na kila mwananchi kupata huduma bora zaidi. Tuwe na ushirikiano baina ya viongozi na wananchi kuboresha sekta ya afya.
 
Upvote 7
Back
Top Bottom