Elections 2015 Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,


Kama ilivyo kawaida yetu jf, wewe kama mwana JF, una pata ile kitu inaitwa the jf advantage to "be the first to know" kuwa ujio wa Lawassa kujiunga Chadema, sio tuu utakipaisha Chadema to unimaginable dimentions kutokana na ufuasi mkubwa wa watu walio nyuma yake, bali ujio huo, unaandamana na neema kubwa na neema tele za mambo mengine mengi makubwa na mazuri kwa Chadema, na moja kubwa ni kwa Chadema kuhama kwa Makao Makuu yake toka kwenye kale kajumba kalichopo Mtaa wa Ufipa, Kinondoni Dar es Salaam, ambako hakuna hadhi ya makao makuu ya chama kikuu cha upinzani, yatahama kutoka hapo Mtaa wa Ufipa hadi kwenye eneo jingine lenye hadhi na nafasi zaidi ili angalau kufanania!.

Hii ni kufuatia idadi kubwa ya watu wanaotarajiwa kujiunga na Chedema kufutia ujio wa Edward Lowassa kwenye chama hicho.

Hali hii ni kufuatia hali iliyojitokeza jana, wakati Edward Lowassa alipofika Makao Makuu ya Chadema, mtaa wa Ufipa, kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea urais kupitia Chadema, kufuatia umati mkubwa wa wafuasi wa Chadema kufurika kwa wingi hali iliyoleta shida na kero kwa majirani mtaa mzima, kutokana na location ya ofisi hizo zilipo eneo lililozunguka ofisi hizo ni eneo dogo kufuatia ofisi hizo kuwepo kwenye eneo la makazi ya watu. Na hapo hao waliojitokeza ni wafuasi tuu wa Chadema, bado tsunami ya wafuasi wa Lowassa hawajatia timu!, wakitia timu kama hali ilivyokuwa uwanja wa Sheikh Amri Abedi, then Mtaa wa Ufipa, unahatari ya kudidimia na kuzama, huku nyumba zikipata nyufa hivyo sio tuu kuleta bughudha ya umati mkubwa wa watu bali pia ni hatari kwa maisha ya watu kuweza kusababisha janga la kitu kinachoitwa stampede!.

Ukipiga hesabu ya jumla ya ruzuku yote ambayo Chadema imekuwa ikipokea, ukajumlisha na zile fedha za Sabodo alizoipa Chadema kujenga ofisi za makao makuu zenye hadhi, na kulinganisha ruzuku hiyo imekuwa ikifanyia nini, utakubaliana na mimi, kuwa fedha hiyo, ingetosha kabisa kujenga jengo jingine la maana na lenye hadhi kwenye eneo la kutosha. Hali hii imetokana na upangaji mbovu wa vipaumbele vyake, hali iliyopelekea matumizi mabovu ya ruzuku, kama yalivyofafanuliwa kwenye ripoti ya CAG.

Mabadiliko hayo chanya ya ujio wa Lowassa sio tuu kwa Chadema kumiliki jengo lake lenyewe, bali pia Chadema itamiliki media zake yenyewe kikiwepo kituo chake cha Redio na Televisheni pamoja na magazeti yake yenyewe, kwa sababu Lawassa hapo alipo tayari anamiliki by proxy, familia kubwa ya media, yenye vituo vya Redio, TV na magazeti lukuki!, hivyo sasa pia vitatumiwa kuisupport Chadema kwa kuanzia tuu, wakati mchakato wa umiliki rasmi wa vyombo vyake yenyewe ukiendelea!.

Ama kweli mgeni njoo, mwenyeji apone!.

Hongera sana Lowassa!.

Hongera Chadema.

Ikulu 2015 ni ya UKAWA!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali

Source ya Taarifa hii ni observation yangu binafsi.

NB. Japo Pakali ni mwanachama wa chama cha siasa, na ni kada wa Chama cha Mapinduzi CCM, huyu ni kada mzalendo wa kweli wa taifa hili kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa, kazi yangu ni to tell nothing but the truth, with objectivity, impartiality and balance from all sides!.
 
Pasco

Mkuu Pasco unataka niamini kwamba ulikuwa hujui kuwa CHADEMA wanapanga pale ufipa au ndio michimbezo ya kumpata mgeni?
 
Last edited by a moderator:
Lowassa....Chademaaa, Ukawaaaaa....yaani tunabadili gia juu kwa juu...yaani Ukawa wamecheza game hili kama MESSI VILE... maana ushindi wa kishindo ni saa 2 asubuhii...

Maskini CCM hawa hawajui nn kinaendelea, wako ktk coma...butwaa...wanakanana wenyewe kwa wenyewe...daahh..!!
 
Pasco bhana,
Anyway,hata ukiongea common sense tu,nitakuheshimu,regardless ni fact or not. Kwamaana uyanenayo mengi huwa. Hivyo tutegemee jumba la HQ lenye hadhi ya El-premier!
 
Last edited by a moderator:
Pasco

Wakinamama na wanafunzi wanavujiwa kwenye hospital na shuleni halafu wewe unaleta mambo ya anasa mpumbavu kweli ofisi zitakuwa mioyoni mwa watanzania
 
Last edited by a moderator:
Chadema kilikuwa chama cha Ukombozi mpaka alipoingia Lowasa sasa kimekuwa Chama cha Matumaini! Kwa chama cha matumaini, ni vizuri wahamie kwenye magorofa marefu kule Samora ndo kwao. Wawaachie wakombozi ufipa yao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…