Uchaguzi 2020 Mabadiliko katika siasa za Tanzania yamejengwa sana na kauli ya kuunga mkono Juhudi

Uchaguzi 2020 Mabadiliko katika siasa za Tanzania yamejengwa sana na kauli ya kuunga mkono Juhudi

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Bishara ya kununua watu kwa ahadi ya madaraka au nguvu ya fedha itabaki kuitwa biashara ya utumwa siku zote.

Waasisi wa biashara ya utumwa awamu ya tano Wana kila sababu yakulaumiwa na kukifanya chama kitumie muda na rasilimali nyingi kusaka watu ambao hawana mchango chanya kwenye mustakabali wa nchi na chama bali familia zao.

Tulipowanunua na kuwapa nafasi kugombea ndani ya chama tulikigawa chama kwa sababu hatukuruhusu wapite kwenye mchujo wa ndani, wanachama wakaumia na hasira zao tumeziona kwenye kura za maoni

Lakini wapo waliotegemea watateuliwa ndani ya chama hawakuteuliwa bali wageni walifika nakukaribishwa chumbani. Alaaniwe aliyeleta mradi huu ndani ya chama.

Wakati tunakusanya mamluki upinzani wao walijijenga wakitathimini nani mpinzani wa kweli nani yupo upinzani kwa maslahi ya cheo.

Wananchi nao waliona uonevu na utumwa uliokuwa unafanyika wakanyamaza, ila Leo hii wanaonyesha wazi wazi kuukataa utumwa. Waliwakataa kupitia wajumbe na wanawakataa kqenye kampeni.

Mbinu zakuwarejesha wabunge zilikuwa na baraka ya tume zikiitwa huru na haki hazitatumika 2020?
 
Back
Top Bottom