Mabadiliko Katika Soko la Ajira la Wadada wa Nyumbani

Ukweli1

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
550
Reaction score
333
Watanzania tumefika mahali kazi za usafi wa nyumbani zinafanywa na foreigners, nimejiuliza yafuatayo:-

1) Inamaana watanzania wamejitosheleza hawahitaji kufanya kazi za nyumbani (kielimu na mengineyo)?

2) Au kilimo kimeajiri wengi?

3) Au inamaana watanzania ni wachaguzi wakazi, bora mtu akae bila kazi?

4) Au watanzania sio waaaminifu kwa kazi za nyumbani, tunaona bora tusiwaajiri?

Naomba mawazo yenu wadau.
 
Watanzania wanaogopa kuteswa na waajiri wao. Nafikiri umesikia vitendo vilivyotokea kwa wafanyakazi wa ndani miezi michache iliyopita!
 

inategemea huyo foreigner katoka nchi gani. maana kama burundi au ethiopia kuna wanaoomba kazi za ndani hawahitaji hata mshahara zaidi ya kupata msosi na malazi, sasa akitokea wa hivyo kwa nini hata wewe usimchukue. au mwezetu kuna foregner katoka amerika au ulaya umemuona anafanya kazi kwa mtu?
 
Foreigner maana yake ni mtu aliyetoka nje ya nchi inaweza kuwa nchi yoyote sio ulaya/amerika tu mkuu...it is as simple as that...post yangu ilitaka kujua kama hii movement inaoriginate from supply side or demand side.

Asante kwa mchango wako mkuu.
 
Watoto wa tz hawana malengo, unamwajiri msichana anakuja hana hata chupi, ukishamnunulia, akipata mafuta ya kupaka msosi mzuri miezi 2 anaanza, kuamshwa badala ya kuamka mwenyewe, atarundika nguo week nzima, ukiuliza utaambiwa nataka kwendanyumbani.anataka kuwa boss asiulizwe kwa kosa lolote.ni usumbufu mtupu. Wa nje mm binafsi nimeajiri mkenya ni miaka miwili imepita, ana malengo akitaka kwenda nyumbani anatoa taari 1 week kabla, akisema narudi lt say j3 atarudi kwa muda huo hutumii pesa kwa mambo yasiyo na manufaa. Kwa kweli sijawahi kukaa na msichana wa tz kwa muda hivi.
 

Dah mkuu juzi nimetimua mfanyakazi wa ndani, Yaani pamoja na hayo yako yeye alifikia hatua anaondoka theni ndiyo anani SMS kwamba sitokuwepo leo nimesafiri, akirudi ananuna, uliona wapi tajiri ananuniwa?
 
Hili nalo neno.... Sikuwahi kuwaza kuimport house manager. Dada wangu kila alipoomba nyongeza nilimsikiliza na kazi pia anajitahidi. Lakini mara ya mwisho ameomba nikampa masharti akifulu tuongeze mf chakula kiwe mezani 7pm sharp, b/fast nayo 7am sharp etc akashindwa... Mara na robo, mara na nusu etc.. Nikamjuza tu kwamba hapo bado itafaa avute nguvu akiweza namlipa retroactively na ya October. Dissapointingly, akaninunia... Blah! Nina miaka 2 naye lakini ikabidi nianze explore other options. Napata wapi mtu wa malengo? Inatia raha uwe natu halafu baadae naye unamkuta ana maisha yake mazuri sehemu...
 
Dah mkuu juzi nimetimua mfanyakazi wa ndani, Yaani pamoja na hayo yako yeye alifikia hatua anaondoka theni ndiyo anani SMS kwamba sitokuwepo leo nimesafiri, akirudi ananuna, uliona wapi tajiri ananuniwa?
hahhahaa huyo wako komesha kweli, ni shida hasaaa na hawa wa dada time to cross border, sijawahi kufikiria ilo maana uzalendo kwangu ni msingi ila wameshaniendesha vya kutosha.
 
Huyu niliye naye sasa ni wa pili, wakwanza alikaa miaka 2 na nusu sasa anafanya biashara ananunua culture huku moshi anauza kwao taveta, huwa nasikia raha sana
kila akija huwa ananitafuta tunaendelea kushauriana
. Watz niliyekaa naye sana ni miezi 7 tena kwa uvumilivu mkubwa, mara anune bila sababu, mara anipigie watoto, kikubwa zaidi akaanza kudeki na kanga moja bila hata kuvaa chupi mwee, ndiyo nikaona nijaribu kwengine
Nashukuru sijawa disapointed tena. Hwa wanakwambia kabisa nikifikishabkiasi fulani cha pesa naondoka, hawadai kuongezwa mishahara labda uamue mwenyewe.
 
Nina ubinaadam lakini huyu wa kuniandikia sms, akirudi atakutana na begi lake getini. Loo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…