MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 305
- 728
Mabadiliko madogo yaliyofanywa na Rais SAMIA SULUHU HASSAN katika Baraza la Mawaziri yanapaswa kupongezwa kwa kuwa yanalenga kuleta matokeo chanya kwa Taifa hususan katika: Kuendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Serikali ya Tanzania na mataifa mbalimbali duniani, Kuendelea kuimarisha ulinzi na hali ya amani nchini pamoja na Kuendelea kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kupata huduma mbalimbali za kijamii kwa ufanisi hasa ikizingatiwa weledi na utendaji kazi wakuridhisha walionao Mawaziri wateuliwa, STERGOMENA TAX, INNOCENT BASHUNGWA na ANGELLA KAIRUKI.
STERGOMENA TAX kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni jambo sahihi kwa kuwa mtajwa ana uzoefu katika masuala ya diplomasia (Mwanadiplomasia mbobezi) aliyehudumu katika Jumuiya ya Maendeleo Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa miaka tisa (2013-2021) kama Katibu Mtendaji (Excetuvie Secretary).
Pia, amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa miaka sita (2008-2013). Kwa uzoefu huu ni hakika TAX anakwenda kuitendea haki Wizara yake mpya kwa kuwa amerudi katika uwanja wake wa nyumbani, hivyo pasi na shaka tuna Imani kuwa diplomasia ya Tanzania ina kwenda kung’ara zaidi.
INNOCENT BASHUNGWA msomi na mwenye weledi na uzoefu wa kutosha katika nafasi ya uwaziri: 2019- 2020 alihudumu kama Waziri wa Viwanda na Biashara, 2020-2021 kama Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, 2022 mpaka uteuzi huu mpya alihudumu kama Waziri wa TAMISEMI.
Hivyo kutokana na uzoefu huo BASHUNGWA ana kwenda kuwajibika ipasavyo kama Waziri mpya wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
ANGELLA KAIRUKI, pia ana uzoefu wa kutosha katika Wizara zenye dhamana ya kutoa huduma moja kwa moja kwa wananchi. Mwaka 2012 hadi 2015 alikuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, mwaka 2015 alihudumu kama Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Baada ya Uchaguzi wa mwaka 2015 alikuwa miongoni mwa Mawaziri Wawili waliohudumu katika Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo, KAIRUKI kuteuliwa kuwa Waziri wa TAMISEMI, Wizara ambayo pia inahusika katika kutoa huduma za moja kwa moja kwa wananchi.
Hivyo, kutokana uzoefu alionao katika masuala hayo KAIRUKI anakwenda kuitendea haki Wizara hiyo.
Wito kwa Watanzania wenzangu tuwaunge mkono Mawaziri hawa katika utendaji kazi wao pamoja na Serikali kwa ujumla ili kuendelea kujipatia maendeleo.