Nchi zenye uchumi mkubwa duniani kama Marekani na China zinapiga hatua kubwa katika Nyanja mbalimbali za teknologia wakati sisi Tanzania(Africa kwa ujumla ) tukiwa bado tuko nyuma. Mifano mizuri tumekuwa tukiona mapinduzi yanayozidi kufanywa katika utengenezaji wa magari, kampuni moja ya hukou China inayoitwa Baidu imepata leseni ya kwanza kabisa katika jiji la Shenzhen ya kuweka barabarani gari ndogo ambazo zinajiendesha zenyewe(robotaxi) bila kuongozwa na abiria na zikiwa zinatumia nishati safi ili kuweza kujiendesha.
Mfano mwingine wa aina hii ni magari mbalimbali yanayotengenezwa na kampuni ya Tesla yenye uwezo wa kujiendesha na yanayotumia nishati ya umeme katika uendeshaji wake. Mbali na teknologia hii ya magari lakini pia tumekuwa tukishuhudia mapinduzi makubwa katika mambo mengine mengi kama usalama katika matumizi wa mitandao(Cybersecurity)
Leo hii sisi kama Taifa hatujawa na ujuzi wa kuratibu usalama wa taarifa za watumiaji wa mitandao kitu ambacho kinatuweka katika hatari kama Taifa, pengine tunaona tunaona kama taarifa zetu binafsi zinazowekwa mitandaoni haziwezi vibaya lakini si hivyo. Kuna haja kubwa kuja na njia sahihi za kufanaya uratibu(regulation) katika suala zima la mitandao ili kulinda usalama wa watumiaji wa hii mitandao
Siku chache zilizopita kitengo cha ujasusi cha Marekani kilifanya utafiti katika vifaa vya mtandao vya kampuni ya Huawei vilivyokuwa karibu na eneo lenye silaha za kijeshi na kugundua kuwa vifaa hivo vinaweza kuchukua taarifa za kijeshi na kuzitunza(chanzo: Reuters). Swali ni je sisi kama taifa tuna ujuzi wowote unaoweza kutusaidia kujua hatari katika vifaa tunavyotumia kama ni salama kwa Taifa letu? Au kuna hatua zozote zinachukuliwa kuhakikisha matumizi yetu ya teknologia tunazotoa nchi za nje ni salama kwetu?.
Basi kwa kuwa maswali haya hatuwezi kuyajibu basi kuna haja kubwa sana ya kuongeza nguvu kubwa katika teknologia ili kuweza kuendana na mazingira halisi ya Dunia ya sasa na kuweza kuimarisha usalama wetu kama taifa.
Dunia yetu kwa sasa imebadilika sana kiasi kwamba tunaambiwa tu angani angani kuna satelaiti nyingi mithiri ya kukaribia kugongana lakini katika idadi iyo kubwa ya satelaiti katika anga za juu hakuna hata moja kwa teknolojia ya Afrika, ni baadhi ya nchi chache ambazo zimeweza kutuma vyombo hivyo katika anga na hizo nchi zimesaidiwa nan a nchi za ulaya na Asia katika utengenezaji na utumaji wa vifaa hivi.
Katika tathmini inayofanywa na chi zilizoendelea ni kwamba kuna uwezekano mkubwa satelaiti zikatumika vema kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika siku zijazo, mapema mwaka huu shirika la habari la Global Times la huko Uchina liliripoti kwamba nchi hiyo ina mipango ya kuweka teknologia inayoweza kuzuia mawe makubwa(meteorites) yasiweze kugonga uso wa dunia.
Lengo la mifano yote ni kuonesha jinsi gani sisi kama Taifa bado tuko nyuma katika mambo mbalimbali yahusuyo teknologia na jinsi gani tunaweza kujipanga ili kuweza kupiga hatua katika jambo hilo.
Hizi nchi zote wakati zinaanza lazima zilianzia chini na taratibu zikaweza kupiga hatua katika mapinduzi hayo, hivyo basi hata sisi kama Taifa tunaweza kuanzia chini kabisa na tukaweza kusonga mbele kama ambavyo wenzetu wamefanya, pengine tunaweza kupiga hatua kubwa zaidi kuzidi hata hizi nchi kubwa baada ya muda fulani. Imefika wakati nchi nyingine zinapambana kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi sisi bado hatua na uwezo wa kuzalisha umeme wa makaa ya mawe kwa kutumia ujuzi wetu mbali na kusaidiwa na mataifa ya nje katika kila hatua.
Hivyo ni lazima tukubali kuwekeza sana katika sayansi na teknologia au tukubali kutawaliwa katika mifumo yetu yote kama tutachagua kuendelea kutumia teknologia ya nchi nyinginezo katika mifumo yetu jambo ambalo si zuri kwa ustwahi wetu kama Taifa.
Kwa kuwa tayari tumeona jinsi gani nchi nyinginezo zilizoendelea zilivyoweza kufanya mapinduzi haya basi hata kwetu sisi tukiamua ni jambo ambalo linawezekana, tukiweka misingi mizuri katika elimu yetu kuanzia katika ngazi za awali ili kuweza kutengeneza mazingira ya kuwa na wahitimu wenye weledi katika nyanja ya teknologia.
Mitaala yetu ya elimu ikifanyiwa marekebisho tukatoa kipaumbele katika ufanisi ni dhahiri shairi tunaweza tukapiga hatua kubwa sana katika hili.
Tunaweza tusifuate njia zilezile walizotumia wenzetu wa Ulaya na Marekani lakini bila shaka tunaweza kujifunza kutoka Uchina, nchi ya China ilikuwa na uchumi sawa na wa kwetu miaka sitini iliyopita lakin leo hii ni nchi ya pili kwa uchumi mkubwa zaidi duniani na imepiga hatua kubwa zaidi katika teknologia ambacho ndio kichocheo kikubwa zaidi cha uchumi wake.
Mapinduzi makubwa yaliyofanywa na China katika teknologia yamelifanya taifa hilo kufikia uchumi wenye thamani ya dola za kimarekani trilioni kumi na tisa wakati nchi inayofuatia ya Japan ikiwa na uchumi wenye uchumi wa thamani ya dola za kimarekani trilioni tano.
Kitu kikubwa walichofanya nchini China ilikuwa ni kujifunza kwa nchi nyingine ambazo zilikuwa bora zaidi katika suala la uzalishaji mali na kuyakaribisha makampuni mbalimbali ya kigeni kwenda kufanya uwekezaji nchini humo na walihakikisha uzalishaji unafanyika kwa gharama nafuu zaidi ili kuweza kupata masoko nje ya nchi yao kwa bidhaa wanazo zalisha katika viwanda vyao.
Hivyo basi kwa mifano hiyo iliyotolewa katika Makala hii na ushauri ulioambatanishwa tuna mengi ya kufanya kama kweli tunataka tusibaki nyuma katika swala zima la mapinduzi ya teknologia

Upvote
0