Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar, 1984: Kipi Hasa Kilichobadilika?

Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar, 1984: Kipi Hasa Kilichobadilika?

Kelele za SJMTZ hazitukoseshi usingizi wa karafuu huko visiwani!Katiba ni yetu wenyewe na tumeibadili wenyewe...nawashangaa ndugu zetu bado ati anaita Tanzania Bara badala ya Tanganyika!

This was suppose to be a wake up call!:smile-big:

Kwani Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ilienda wapi baada ya Muungano? Kumbuka kifungu cha 3 cha Sheria ya Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 yanasema kwamba:

Zanzibar ni nchi ambayo mipaka yake ni eneo la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogovidogo ambavyo vinaizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
 
Unauliza au unajibu ? Nilifikiri jawabu ndio hayo mabadiliko....Anyways, on our side we're pretty satisfied with the new change in our constitution.All we need now is 2nd referendum on this crap!
 
Buchanan kama ukiiosoma katiba ya Muungano vizuri baadhi ya mabadiliko hayo yatahusisha mabadiliko ya katiba ya Muungano na hili haliwezi kufanyika mpaka bunge la muungano likae. Pia mabadiliko hayo lazima yaidhinishwe na theluthi mbili yawabunge wa zanzibar na theluthi 2 ya wabunge wa Tanzania Bara.

Kwa hiyo mchakato bado unaendelea.

Baadhi ya mambo sidhani kama yatapita katiaka bunge la Muungano (Ingawa nina wasiwasi sana na wabunge wa CCM kama watachaguliwa kwa wingi) kwa hiyo tutarajie mgogoro mkubwa zaidi wa kimuungano.

By the way ulipata nafasi ya kuhudhuria Mjadala wa mabadiliko haya uliofanyika jana Diamond Jubilee? Ulikuwa ni njadala wa wazi na haya mambo yalijadiliwa kwa kina. Tulikubaliana kuendeleza mjadala na kuhamasisha ufufuaji wa serikali ya Tanganyika. Nitakujuza kama kuna mjadala mwingine maana tulikubaliana iwepo ili kujenga hamasa.

Naona hujatoa hoja zenye data. Unapodai baadhi ya mambo, yapi? Mchakato upi? Baadhi ya mabadiliko hayo, yapi? Na mnapojadili kuwa Serikali ya Tanganyika irudishwe, mmetumia vigezo gani kwa hilo? Mnafikiri umaskini wa Tanzania unasababishwa na kutokuwepo kwa Serikali ya Tanganyika au namna gani?
 
kwani kifungu cha zamani kilikuwa kinasemaje? si kilikuwa kinawapa huo uwezo wa kujitoa?sasa haya mabadiliko yanaonyesha kuwa sio mtiririko mmoja wa kutaka kuwa nchi. Maana kwa upande mmoja wamedai kuwa nchi, na upande mwingine wamekubali kushiriki katika vita pamoja. Umenipata hapo? Just a point of note.

Nimekupata, ila mtiririko wa Zanzibar ni wa taratibu, sio ghafla. Tumeshaona sasa hivi suala la Elimu ya Juu nako limeshaanza kuleta mzozo, keshokutwa wataanza kuzungumzia juu ya ulinzi na usalama, mafuta ndio hayo walishayatoa kinyemela kwenye mambo ya Muungano, nk. Kama unafuatilia mambo hata katika kauli zao Wazanzibari utajua tu mwelekeo ni upi!
 
hili suala limejadiliwa kwa upana wake na gazeti la Raia mwema katika matoleo 3 na wameonyesha vifungu vya mkataba wa muungano ambavyo vinathibitisha serikali zote mbili hazikufutwa na ni Rais mstaafu aliyekuja kutoa decree ya kufuta Tanganyika na katiba ya mwaka 1977 haikuzingatia ipasavyo mkataba wa muungann unaotambua nchi ya zanzibar na Tanganyika kuwa zitaendelea kuwepo ndani ya muungano na pia maneno ya Tanzania bara na Tanzania visiwani hayakuwepo katika mkataba husika wa muungano
 
zanzibar hoyee sasa hivi CUF na CCM lao moja wanajiandaa kula kodi zanzibar so its better tukaimarisha vyama vingine, Zanzibar kwishinei
 
hili suala limejadiliwa kwa upana wake na gazeti la Raia mwema katika matoleo 3 na wameonyesha vifungu vya mkataba wa muungano ambavyo vinathibitisha serikali zote mbili hazikufutwa na ni Rais mstaafu aliyekuja kutoa decree ya kufuta Tanganyika na katiba ya mwaka 1977 haikuzingatia ipasavyo mkataba wa muungann unaotambua nchi ya zanzibar na Tanganyika kuwa zitaendelea kuwepo ndani ya muungano na pia maneno ya Tanzania bara na Tanzania visiwani hayakuwepo katika mkataba husika wa muungano

cha msingi nchi ya tanganyika irudi na zanzibar irudi ikisha tuustructure muungano

maana mie hucheka ati kuna tume ya kushughulikia kero za muungano, inaundwa na waziri wa muungano (ambaye ni mzanzibari), makamo wa rais (ambaye ni mzanzibari) na waziri kiongozi wa zanzibar (ambaye ni mzanzibari) na waziri mkuu wa muungano(ambaye ni mtanzania mwenye asili ya bara) hapa pana kasoro

zirejeshwe mamlaka zote wazanzibari na watanganyika wakae kuujadili muungano.
 
Hao wazanzibari wanoshangilia mabadiliko ya katiba wanaufinyu wa mawazo, ili kura ya maoni ifanye kazi yake ilitakiwa wananchi wapewe muda wayasome na wayapitie kabla hawajayapigia kura, je hicho kilifanyika? lugha iliyotumika kwenye marekebisho ni kisanii kitupu, hiyo ilikuwa lugha ya kuwalainisha wazanzibari kwani CCM ilishaweka mikakati ya kuweka raisi mpemba Zanzibar, tangu kipindi marehemu Dr. Omar Ally Juma ( mungu amlaze mahali pema), lengo la CCM ni kuweka uwiano wa madaraka kwani viongozi BMZ waliiapa mpemba hatatawala Zanzibar, wazinzibar katiba ya awali iliwanyima kitu gani cha msingi na hii mpya itawapa kitu gani? Tatizo lenu wengi wenu bado mna mawazo ya kitumwa ndio maana tunasema mtumwa hana asili, mmekimbilia kuutukuza uarabu na kuacha asili zenu za kimakonde na kinyamwezi, tafuteni historia za kwenu ili mmjue mnapotoka, siku mtakapojua asili zenu basi hamtaubeza muungano kwani umewaokoa na mengi.
 
Wanajamvi/Wanasheria naomba Soft Copy ya katiba Mpya ya Zanzibar ambayo ina yale maridhiano ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa
 
Nami naishubiri Kwa hamu: utakua umefanya la maana sana. Ahsante kwa wazo lako.
 
Wanajamvi/Wanasheria naomba Soft Copy ya katiba Mpya ya Zanzibar ambayo ina yale maridhiano ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa

Kimsingi, hakuna katiba mpya ya Zanzibar. Katiba bado ni ile ile ya mwaka 1984. Kilichofanyika ni marekebisho ya 10 (Na. 9/2010) ya katiba ya Zanzibar yaliyofanywa na kikao cha Baraza la Wawakilishi mwaka huu na kuingiza muundo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa kwenye katiba. Chini ya marekebisho hayo, Zanzibar sasa inajulikana kwa jina la Serikali ya Mapinduzi ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ambayo inaundwa baada ya uchaguzi mkuu.

Pia marekebisho hayo yameondoa kipengele kilichokuwa kikieleza kuwa "kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za serikali, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atashauriana na Rais (wa Zanzibar) kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi". Badala yake marekebisho hayo yanaeleza kuwa "kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za serikali, Rais aweza kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi". Chini ya mabadiliko hayo, rais wa Zanzibar hatakuwa na ulazima wa kushauriana na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya maamuzi ya kugawa mipaka ya nchi yake.
 
Kimsingi, hakuna katiba mpya ya Zanzibar. Katiba bado ni ile ile ya mwaka 1984. Kilichofanyika ni marekebisho ya 10 (Na. 9/2010) ya katiba ya Zanzibar yaliyofanywa na kikao cha Baraza la Wawakilishi mwaka huu na kuingiza muundo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa kwenye katiba. Chini ya marekebisho hayo, Zanzibar sasa inajulikana kwa jina la Serikali ya Mapinduzi ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ambayo inaundwa baada ya uchaguzi mkuu.

Pia marekebisho hayo yameondoa kipengele kilichokuwa kikieleza kuwa “kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za serikali, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atashauriana na Rais (wa Zanzibar) kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi”. Badala yake marekebisho hayo yanaeleza kuwa “kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za serikali, Rais aweza kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi”. Chini ya mabadiliko hayo, rais wa Zanzibar hatakuwa na ulazima wa kushauriana na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya maamuzi ya kugawa mipaka ya nchi yake.

See attachment! Msisahau kuweka "senksi!"
 
Attachments

Mkuu Buchanan nilikuwa najiuliza umepotelea wapi, hili Jukwaa la Sheria lilidorora kidogo. Thanx God y`re Back.

Nilikuwa overtaken na mambo ya uchaguzi mzee, nafikiri sasa nitarudi kwenye Jukwaa letu la Sheria! Thanks kwa kunikumbuka!
 
Back
Top Bottom