Mabadiliko ya Elimu Yetu Hayaepukiki. Ila ni lazima tuwe Makini kwenye Utekelezaji wa Mabadiliko ya Mtaala Mpya wa Elimu

the power

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
407
Reaction score
799
Kuna msemo unasema "Umeruka Vumbi Ukakanyaga Matope". Hakuna ubishi elimu yetu inahitaji over-hall, ni kweli kabisa kama tunataka kusonga mbele kielimu kuendana na ulimwengu wa sasa wa sayansi na tekinologia lazima tufanye mabadiliko kwenye mfumo wetu wa elimu.

Tumeupitia mtaala mpya wa elimu, tumeambiwa steps zilizopitiwa kwenye kuuandaa, tumeelezwa situation analysis ilivyofanyika; kweli na ni vyema na haki. Kizuri juzi juzi tumeelezwa na mkurugenzi wa elimu pamoja na Waziri wetu professor Mkenda hatua za utekelezaji hasa kwa upande wa walimu.

Naunga mkono asilimia 100 kwamba lazima mabadiliko ya walimu yawepo, ila nisingependa tuconcentrate kwenye walimu tu, ukiusoma huu mtaala unahitaji maadalizi kwenye sector nyingi, nilitegemea wasomi watudadavulie mbali ya walimu wamejipanga vipi kwenye sector nyingine?

Kwenye programming kuna msemo wa kimombo unasema "How do you Introduce new Changes in a Country's Development Sector" , kibaya hizi si changes tu ni changes kubwa balaa (Huge changes) na zaidi ndani ya sekta kubwa (big and impactful developmental sector); Yaani, namna ambavyo unaintroduce major changes kwenye sector kubwa ya maendeleo. Kumbuka kukamilisha kuandika secural ni one thing, ofcourse ni good step lakini; a)kufanya maandalizi (strategic planning) ya kuanza kuimplement changes is another thing na, b) Kujiandaa namna ya kuintroduce changes (operationalize) is another important and separate dimension.

Sasa ni kipindi cha maandalizi ya kuanza kuimplement hii secural mpya ya elimu, kumbuka maandalizi sio kitu cha kukurupuka, inabidi tujue na lazima viwekwe kwenye hiyo secural: ni maandalizi yapi? yatahusu maeneo yapi? na yatafanyika kwa mda gani? na cha muhimu zaidi kwa kila andalizi kipi kinahitajika; yaani the why, the how and when are critical questions to ask ourself and systematically document in our secural. Sasa twende kazi!

1) Mabadiliko Sekta ya Walimu
Tumesema watapewa muda kujiendeleza, ni kwa muda gani? je kuna utaratibu wa kuwasaidia? je kama 50 percent wakikosa pesa za kujisomesha tutawafukuza?, lazima tu-adress potential barriers kabla ya kuanza na tuwe na plan A,B,C n.k

2) Mabadiliko ya Mitaala na Vitabu rejea
Je tutabadilisha mitaala na vitabu rejea? Ofcourse yes kwani secural imetamka vitu vipya vingi sana, Je tutaiandaa vipi mitaala na hivyo vitabu rejea? je tunauwezo kifedha na kiutaalamu kuandaa vitu hivi kabla ya kuoperationalize huu mtaala,itachukua muda gani?

3) Mabadiliko ya Kuboresha Mazingira ya Ufundishaji ;majengo, mahabara n.k
Sasa unataka mtoto aende mahabara kujifunza steps fulani baada ya topic, unataka mtoto afanye kwa vitendo sehemu ya sylabus, unataka mtoto afanye practical sessions kwa kutumia reagents au vifaa fulani, unataka kila manafunzi a-demonstrate kitu fulani; swali tumejiandaa vipi kuboresha mazingira mabaya na hafifu ya kufundishia ya shule zetu za sasa; kumbuka changes are good but expensive.

Kwenye epidermiology kuna philosopy inasema "in order to quickly realize your intended outcome in a developmental program, you need to ensure each projects/major interventions within the program produce an additive effect to each other. Hizo sekta tajwa lazima zifanyike kwa pamoja (concurrently or by phases), kutengeneza walimu competent kuende sambamba na mabadiliko /uboreshaji wa mitaala na vitabu rejea, lakini lazima vyote hivyo tajwa viwe supported na uboreshaji wamazingira ya ufundishaji . Otherwise tutakuwa tunacheza makida makida.

Angalizo hapa ni lazima tukumbuke Kila badiliko katika sekta husika litatakiwa kuwa na steps zake na muda wake na ghalama zake, otherwise tukikurupuka tu yatakuwa mahafa.

Mwisho, nachelea kusema nina wasiwasi kama wenzetu wamejiandaa kiprogramming na kisystem kuoperationalize mtaala huu mpya ili ulete matunda tarajiwa na si matunda hasi; matunda mabaya zaidi ya tunayokula sasa, Hili la system nitaliongelea siku nyingine kwani ni topic inayojitegemea, inaitwa "System Thinking in Programming".

Ukioona viongozi wakuu wanaongelea kipengele kimoja tu kwenye system nzima ya mtaala mpya mfano walimu kama jibu kamili kuhusu overall preparation (maandalizi) ya program kubwa kama hii, ujue kuna tatizo. Lakini hatujachelewa muda, nafasi, watu tunavyo ni suala la tunavitumia vipi?
 
Umeongea kitu cha msingi sana lakini wachangiaji mada hawaonekani kama ungeandika umbea wa daimond na zuchu au mobeto na azizi ki maoni yangejaa kurasa na kurasa
 
Umeongea kitu cha msingi sana lakini wachangiaji mada hawaonekani kama ungeandika umbea wa daimond na zuchu au mobeto na azizi ki maoni yangejaa kurasa na kurasa
Aksante sana na mimi nafahamu topics za kuandika ili watu wachangie ila hiyo hainizuii kudadavua mada nyingine muhimu hata nikijua sitapata mchangiaji. Kwangu hii ni kama reserve kumbukumbu yangu kuna siku na saa hizi mada zangu zote nitazitwist na kuziongelea katika panel kubwa na za maana. Nimezihifadhi humu kama archieves .Ukisoma flow of idea and thoughts ya hili andiko pamoja na ushauri ni vitu ambavyo nilitegemea sisi kama wasomi tuvizungumze. Huwezi kujenga nyumba huku ukiongelea matofari tu,nyumba mpaka hisimame inahitaji vitu lukuki na vingine visivyokuwepo hakuna nyumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…