SoC02 Mabadiliko ya fikra za Vijana katika kujishughulisha na kilimo

SoC02 Mabadiliko ya fikra za Vijana katika kujishughulisha na kilimo

Stories of Change - 2022 Competition

Mabula marko

Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
44
Reaction score
38
yesa-wide-landscape.jpg


Picha na farming Africa.


UTANGULIZI
Nchi nyingi katika dunia ya leo hasa zile zinazoendelea zikiwemo nchi za AfriKa hasa katika ukanda wa Sahara ikiwemo Tanzania watu wake hutegemea sana kilimo kama uti wa mgongo wa uchumi wao kutokana na ukweli kwamba watu wake wanakaa katika maeneo ya vijijini ,ikikadiliwa kuwa alimia 75 %ya watanzania wanaishi vijijini na asilimia 25% ni wakazi wa mijini huku katika wakazi wa vijijini zaidi ya asilimia 85% wanajishughulisha na kilimo kama sehemu ya kujipatia kipato na kuendeshea maisha yao ya kila siku(farming first2013)

Katika siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa vijana wengi katika maeneo haya kutokupenda kabisa kujishughulisha na kilimo kutokana na kutokuwa na Imani kama kilimo kinaweza kuwafanya waweze kuwa na maisha mazuri kama ambavyo wasanii , wafanyabiashara na watu wengingine walio katika ajira walivyo na maisha mazuri au ya wastani ukilinganisha na watu wengi wanaojishughulisha na kilimo hali ambayo imekuwa ikiwasukuma vijana wengi kuhama vijijini na kukimbilia mijini kwenda kutafuta shughuli nyingine ili waweze kujipatia kipato hali ambayo imepelekea kuwa na msongamano mkubwa wa watu

WHO wanakadilia kufikia 2030 kati ya watu 6 kati 10 hukaa mjini na mpaka kufikia mwaka 2050 kati ya watu 10 watu 7 watakuwa wakikaa mjini hali hii imesababisha kuongezeka kwa matukio ya kikatiri, wizi, ukahaba na mambo mengine yasiyopendeza kijamii

Kubadili mitazamo ya vijana ili waweze kukiona kilimo kama sehemu ya shughuli zinazoweza kuwaingizia kipato hata kuwapatia fedha nyingi na kuwafanya wakawa watu maarufu kunahitaji kwani mitazamo yetu mingi haioni kama tunaweza kufanya kilimo kama kazi ktupa maisha mazuri na kupunguza ukosefu wa ajira na utegemezi kwa serikali


NAMNA YA KUBADILISHA FIKIRA NA MITAZAMO YA VIJANA ILI KUPENDA KILIMO

Nikinukuu kutoka katika sera ya taifa kuhusu ushirikishwaji wa vijana katika kilimo ya mwaka 2016-2021, Serikali iliona haja ya kutoa kipaumbele kwa vijana kwa kuwawezesha katika Nyanja mbalimbali ili waweze kujishughulisha na kilimo kama sehemu ya kazi na kuweza kujipatia kipato chao

Kuna njia zilizoainishwa kama kutoa mikopo nafuu, kuwawezesha ardhi, kupunguza ushuru wa zana za kilimo na kuwezeshwa mbegu na huduma za ugani na zinginezo ,sambamba na hizo kuna nyingine kama zikizingatiwa zitaongeza hamasa kwa kundi kubwa la vijana wakitanzania na Afrika kwa ujumla

Kilimo kuwa sehemu ya mitaala ya elimu. Kilimo kinapaswa kuwa sehemu ya mitaala ya elimu kuanzia shule za misingi ili kuweze kuondoa zana za vijana wengi kuamini kuwa kazi za ndoto zao ni udaktari, polisi, jeshi, urubani na uinjinia kumbe kama mtu huyu akifundishwa umuhimu wa kilimo na faida zake tangu akiwa mtoto mdogo kuanzia la kwanza ipo siku utamuuliza mtoto unataka kuwa na nani atakwambia nataka kuwa mkulima na hapo tutakuwa tumeondoa dhana ya kukiweka kilimo kama mbadala wa kazi nyingine kwamba iwapo mtu atashindwa kupata kazi ndipo atafanya kilimo

Kuwapa sauti wakulima vijana (kuwepo kwa majukwaa ya kilimo). Hapa vijana wengi wanaojishughulisha na kilimo ikiwemo huduma za kilimo mfano Malembo farm na watu wengine kusimama na kupaza sauti zao na kuwahamasisha vijana kujishughulisha na kilimo, midahalo iandaliwe ya wakulima wasimame wazungumze. Kumekuwa na midahalo ya mingi ya ujasiriamali na biashara inayoandaliwa na vyombo vya habari kina Mohamed Dewji wanasimama na kuongea basi tuwape pia vijana wale wachache waliosimama katika kilimo waweze kuwapa hamasa wengine ili wawezi kuingia katika kilimo vituo vya habari vianzishe vipindi vinavyohusu wakulima na majukwaa ili watu waweze kusimama na kutoa elimu hii ya kilimo

Kuongeza ubunifu katika kilimo. Vijana wengi wanakimibia kilimo kwa kuogopa changamoto mbalimbali zinazoweza kuwakuta na kupoteza mitaji yao, changamoto kama ukosefu wa mvua za uhakika, wadudu na gharama kubwa za zana za kilimo, ukosefu wa ardhi yenye kukidhi mahitaji ya kilimo zimekuwa changamoto kubwa kumbe kunahitajika ubunifu wa teknolojia zitakazopunguza ukosefu wa maji katika kilimo, pia kuleta unafuu wa gharama za zana za kilimo na kufanya matumizi mazuri ya ardhi kidogo inayopatikana na kufanya uzalishaji wenye tija kwa jamii hali ambayo itaongeza chachu kwa vijana kuingia katika kilimo , teknolojia ya kutoa huduma za ugani kwa njia ya simu, kurasa za mitandao , matumizi ya mbolea asilia , kutumia kilimo cha kizimba haya yote na mengine yataleta haueni na kuvutia vijana kushiriki katika kilimo

Kuwapa nafasi vijana katika uandaaji wa sera za vijana hususani katika kilimo. Siku nilivojua kuwa Wizara ya Kilimo imewahi kuandaa sera ya ushirikishwaji wa vijana nilijaribu kuwaulizia wanafunzi wenzangu kama walau hata wanajua tu kama kuna sera hii katika nchi yetu katika watu 10 ni mtu 1 tu ndo alionekana kufahamu kidogo na saa nyingine katika 10 wote hakuna anayejuwa hata wale wanaosoma masomo ya kilimo. Kumbe kuna haja ya sera hizi kuandaliwa katika hali ya ushirikishwaji mkubwa wa vijana iliwaweze kuwa na sera zitakazoweza wavutia vijana katika kujishughulisha na kilimo na kisha kutangazwa kwa vijana katika hali ya ukubwa ili vijana waweze kuzielewa na kuzifuata sera hizo lengo ni kutia chachu ya ushiriki katika kilimo na kuondoa visingizio na hatimae kuendesha maisha yao kwa kutegemea kilimo chenye tija katika maisha yao.

Kukifanya kilimo kuwa biashara. Namna nyingine inayoweza kuwavutia vijana kushiriki katika kilimo ni kukifanya kilimo kuwa biashara kwa maana ya kilimo-biashara kila mahali hali ambayo itawavutia vijana kushiriki katika kilimo hata katika mnyororo wa uongezaji thamani mazao yatokanayo na kilimo kumbe elimu izidi kutolewa nyingi katika kilimo – biashara hali itayaoleta tija kwa vijana kukiona kilimo kama mkombozi na ni furusa kwao


UMUHIMU WA VIJANA KUSHIRIKI KATIKA KILIMO
vijana wana umhimu mkubwa katika kilimo hivo ushiriki wao ni mhimu katika kukinyanyua kilimo kwani wanao ubunifu Zaidi katika kutatatua changamoto zitokanazo na kilimo, vijana pia wanaweza kuleta mabadiliko yenye tija katika kukifanya kilimo kiwe endelevu na kisiwe sehemu ya uharibifu wa mazingira na sekta nyingi zitegemeazo mazao shamba kuendelea na kukua


HITIMISHO

Kilimo kikifanyika vizuri siku zote huwa ni sehemu ya kutoa mabadiliko chanya kwa vijana na vizazi vyake , kilimo kinafanya vijana kukuwa kiuchumi, kifikira na kina namna ya utafutaji furusa kiasi cha kuweza kuondoa tatizo na njaa katika nchi na katika taifa kama tu wakepewa elimu , kupewa sauti katika se
 
Upvote 6
Back
Top Bottom