KERO Mabadiliko ya ghafla ya kiingilio HIFADHINI bila notisi kwa wadau wa UTALII

KERO Mabadiliko ya ghafla ya kiingilio HIFADHINI bila notisi kwa wadau wa UTALII

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari za muda huu kiongozi wa Jamii Forums,

Nikiwa kama Mtalii na mdau wa Utalii wa Nyanda za Juu kusini mwa Tanzania, nipende kuwasilisha kero yangu Kubwa na kwa watalii wengine.

- Ikumbukwe tokea Bei za mafuta zipande April Mosi, kuna baadhi ya Hifadhi ya Taifa nayo imepandisha bei ya kiingilio Hifadhini ambapo hapo awali Hifadhi hiyo ya Mpanga Kipengere ilikuwa ikitoza Tsh 5,900/=.kama kiingilio ila kwa sasa imepanda mpaka kufikia Tsh 10,620/=.

- Inatufanya kujihuliza Sisi kama wadau wa Utalii kusema kuwa Hifadhi inaongozwa na Mafuta,, maana hiyo Tozo imekuja ghafla ukifananisha na Hifadhi nyingine za Taifa kama Kitulo, Ruaha, Katavi na Mikumi ambazo zenyewe zikitozwa Tsh 5,900/=. Kama kiingilio cha watanzania Hifadhini.

- Tunaomba wizara ya Maliasili na Utalii itusaidie kwa hilo, kwasababu katika Sera ya Utalii inataka kuongeza motisha na Idadi kubwa ya watalii wa Ndani kupenda na kuyatalii maeneo. Kwa Gharama hizo kubwa na za ghafla zinatupa ugumu wa kufanya Utalii.

NB: Tozo hiyo ya kiingilio Hifadhini ipo juu Sana ukilinganisha na Hifadhi nyingine zinazopatikana Nyanda za Juu Kusini.

Naomba kuwasilisha.🙏
 
Back
Top Bottom