100 others
JF-Expert Member
- Aug 5, 2017
- 10,825
- 38,702
Kuna hivi vyombo vya habari vya machawa navyo siku hizi wanazungumza siasa, wasafi tv, clouds media na vyombo vingine vya habari zikiwemo youtube channel za machawa, nao siku hizi wanachambua siasa na matukio ya MO29.
Ila naona serikali inaendelea kutumia hivi vyombo na lengo kuu lao si kwa faida na maslahi ya wananchi. Ni mkakati wa kutengeneza picha ya kufikirika kwamba nchini kuna uhuru wa habari, demokrasia, na uhuru wa kujieleza.
Hatua hii inalenga kujisafisha mbele ya Umoja wa Ulaya na jumuiya za kimataifa. Mashirika haya yanafuatilia kwa karibu mienendo ya nchi, hali inayopelekea hata mikutano ya CHADEMA kutozuiwa kwa sasa ili kulinda taswira hiyo. Maana kuna malalamiko huko kwamba vyombo vya habari Tanzania havina uhuru na uhuru wa kijieleza haupo.
Na hio taasisi zinafuatilia, kwa kufanya hivyo wanaonyesha si kweli kinachosemwa.
Soma Pia: Msigwa: Nchi yetu imetoa uhuru wa kutosha wa kujieleza na kutoa maoni, Vyombo vya habari vipo huru kuandika chochote ambacho ni sahihi
Kingine naona ni mikakati ya kupunguza hasira kwa wananchi na kuna uwezekano mkubwa viongozi wakuu walishauriwa na wazee wenye busara ama watu wenye akili kuruhusu watu waseme na kutoa hasira zao. Maana kuwadhibiti ingeleta hasira zaidi na kungetokea vurugu zaidi.
Kiuhalisia, mifumo na tabia halisi ya serikali hii haijawahi kuwa hivi.. hii ni miendendo fake...
Au wenzangu mnaonaje? Lakini yote na yote naona its too late