Mabadiliko ya Katiba natamani hili lingezingatiwa pia

Mabadiliko ya Katiba natamani hili lingezingatiwa pia

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Wakati Katiba Mpya inaandikwa kama ningelikuwepo kwenye mazingira hayo, ningependekeza kuwepo na Mihimili minne katika Tz kwa jinsi mambo yanavyoenda tangu baada ya awamu ya kwanza ya uongozi wa nchi, yaani mitifuano ya kisiasa ambayo haina afya kwa ustawi wa taifa.

Mhimili wa nne ungekuwa ni Jeshi, kwa jinsi hiyo Jeshi lingeondoka kwenye siasa 100% kama Judiciary isivyokuwa kwenye siasa 100%. Hivi sasa Jeshi halipo kwenye siasa kinadharia tu.

Bora tukalipa Jeshi hadhi ya Mhimili wa nne kwasababu kwa mfumo uliopo hivi sasa ni kwamba linapopindua serikali kwa mfano, maana yake ni kuwa lina-control executive ambayo pia ni Mhimili wa kisiasa kama ilivyo Legislature kasoro Judiciary, hivyo basi kumbe Jeshi likichukuwa control ya executive kwa mapinduzi basi linakuwa limeingia kwenye siasa.

Ningependekeza Mhimili wa nne uwe ni Jeshi alafu rais apunguziwe mzigo wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu akabidhiwe CDF au ateuliwe mwingine (ambaye ni Mwanajeshi) juu ya CDF kuwa Amiri Jeshi Mkuu; ili CDF awe pia Ex-officio kwenye Legislature na Executive (Cabinet).

Hii ni kwasababu pia Jeshi ni taasisi kamili inayojitosheleza kwa kuwa na wataalam katika kila sekta/kada ya utumishi.

Majeshi hayo mengine yabakie kwenye Mhimili wa Executive kwa ajili ya enforcement ya sheria. Ila Rais aendelee kuwa ndiye Mkuu wa nchi.

Nadhani tungeenda vizuri zaidi ya tunavyong'ang'ania perspective ya dunia kwamba Jeshi lazima liwe kwenye Mhimili wa Executive.

Kwa staili hii hata Afrika ingepona na mapinduzi ya kila mara kwasababu hakuna Mhimili wa Jeshi ungeenda kupindua Mhimili mwingine ili kuchukuwa madaraka ya nchi kama ambavyo Legislature na Judiciary haziwezi kukalia nchi.

Natamani Tz tubadilike tuwe na mfumo wetu huru (siyo huu wa kikoloni)

“In politics if you want anything said, ask a man. If you want anything done, ask a woman.”
 
Wakati Katiba Mpya inaandikwa kama ningelikuwepo kwenye mazingira hayo, ningependekeza kuwepo na Mihimili minne katika Tz kwa jinsi mambo yanavyoenda tangu baada ya awamu ya kwanza ya uongozi wa nchi...
Jeshi ni serikali kwa maaana ya executive
 
Umelewa amani wewe.
Mkuu,

Mbona hata kwa mfumo huu ambao Jeshi liko chini ya Executive bado tunaona bara la Afrika pekee kwa mfano lina mapinduzi lukuki.

Empirical study by [McGowan, 2003] on Africa holds that, there were 145 plots that proceeded no further than the plot stage, 109 coup attempts that failed, and 82 successful coups from 1960 to 2005.

Olusegun Obasanjo once observed in one of his rhetoric that Africa in about 50 years has had 186 coups and 26 protracted expensive conflicts. It is believed that Comoro leads with 20 coup d’états since independence in 1975.


Tukifanya Jeshi kuwa Mhimili (wa nne) haliwezi kupindua serikali, kwasababu Katiba italizuia kupindua Mhimili mwenzake.
 
Jeshi ni serikali kwa maaana ya executive
Mkuu Yusufuj,

.....na serikali ni Mhimili wa kisiasa (kama Mhimili wa Bunge ulivyo pia) hivyo basi kama Jeshi likiwa ndani ya Mhimili wa serikali basi Jeshi linakuwa liko kwenye siasa pia.

Tusaidie kufafanua zaidi mkuu.
 
Umelewa amani wewe.
Mkuu,

Kazi ya Jeshi siyo kuua tu (kuondoa amani), kazi za Jeshi ziko kadhaa zikiwemo:
1. Kulinda mipaka ya nchi.
2. Kutoa huduma za jamii kama afya.
3. Ujenzi wa miundombinu.
4. Kubuni na kuendesha miradia ya maendeleo e.g. SUMA JKT kwa kesi kama ya Tz. US jeshi lina viwanda vya kuzalisha mali.
5. Uokozi kwenye mabalaa (Disaster Management)
6. Baada ya vita ya Kagera Amiri Jeshi Mkuu aliamuru Jeshi kubaki Kagera kulima mashamba ya maharagwe na mahindi ili kulisha taifa kufuatia njaa iliyokumba nchi na walizalisha kwa ziada.

NB. Kazi ya Jeshi siyo kuua tu (kuondoa amani), hiyo inawezakuwa ni dhana potofu.
 
Back
Top Bottom