Mabadiliko ya Katiba ya TFF

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Tarehe 18/07/2013 Uongozi wa Rais Leodegar Tenga na Katibu Mkuu Angetile Osiah kwenye Kanuni za Uchaguzi za 2013 waliongeza kipengele cha sifa za Mgombea Urais na Makamu wake kuwa na elimu ya angalau Degree ua Chuo Kikuu (University Degree) Kipengele cha 9(8).

Kwenye mabadiliko ya Katiba iliyosajiliwa tarehe 12/06/2015 na Uongozi wa Rais Jamal Malinzi na Katibu wake Mwesigwa Selestine, sifa hizi ziliainishwa kwenye katiba ya TFF ya mwaka 2015 ibara ya 29(7) kuwa Mgombea Urais lazima awe na angalau elimu ya Degree ya Chuo Kikuu (University Degree).

Ukaja Uongozi wa Rais Wellace Karia na Katibu wake Wilfred Kidao kwenye mabadiliko ya katiba ya tarehe 02/02/2019 kipengele hiki hakikutolewa kiliendelea kubaki kwenye ibara ya 29(7).

Katika Mabadiliko ya tarehe 21/12/2019 ya Uongozi huo huo wa Rais Wellace Karia na Katibu wake Wilfred Kidao, kipengele cha sifa za mgombea Urais kilitolewa, hivyo Katiba ya sasa inayotumika kwenye uchaguzi wa mwaka huu haijaainisha sifa za mgombea Urais, japo sifa hizo zimebaki kwenye kanuni za uchaguzi za mwaka 2013, hii inakinzana na Katiba.

Katiba hii mpya imeweka mchakato wa mgombea Urais kupata udhamini wa Wanachama wasiopungua watano (5) kutoka kwa viongozi wawakilishi wa mkutano mkuu wa Kanda 6 na Mikoa 26 kwa mujibu wa ibara ya 84.

Hii inamaana kwamba mgombea mmoja akishapata udhamini kutoka mkoa fulani, mgombea mwingine hawezi kudhaminiwa na mkoa au kanda husika. Kwa lugha rahisi ni kwamba kwakuwa Katiba kwenye ibara ya 30(5) haijaweka kikomo cha idadi ya juu ya udhamini, Mimi Union kama nina ushawishi naweza kuomba udhamini (endorsement) kutoka kwa Kanda zote 6 na Mikoa yote 26 au nikabakisha mikoa miwili, kusababisha wagombea wengine wakose udhamini (endorsement) hivyo kukosa sifa ya kugombea nafasi ya Urais.

Kwa hoja hii naweza kusema kwamba Ibara ya 30(4) ya katiba ya sasa imewekwa kumpendelea Rais aliyeko madarakani na kupunguza nguvu kwa wagombea wengine.

Ushauri wangu, Viongozi wa mpira mnaopewa dhamana na Watanzania, muongoze mpira wetu kwa weledi na kuruhusu ushindani wa uwezo, hii itasaidia mpira wetu.

Niwatakie heri wagombea wote.
 
Uchaguzi wenyewe si unafanyikia Tanga? Ni Nyumbani kwa Rais anaetetea kiti chake ni wazi ameshajipanga vya kutosha.

Mbali na kujipanga pia kuna maendeleo makubwa ameyafanya yanayoonekana hata kwa macho tu. Apewe tu mitano mingine.

Hizo kanuni tutakuja kuzirekebisha tena baada ya uchaguzi kuisha..
 
Uchaguzi hakuna, kuna endorsement tu ya Msomali kuendelea kuwa Rais wa TFF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…