SoC02 Mabadiliko ya Kiuchumi

SoC02 Mabadiliko ya Kiuchumi

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 11, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Uchumi:Serikali iangalie swala La maeneo yaliyo wazi mjini haswa Dar es salaam wamilikishwe watu binafsi kwa mkataba ambao utakua wa kudumu ambapo atakayemilikishwa atapaswa kuanzisha mradi mfano apartments ambapo baada ya mradi kukamilika kutakua kugawanya faida Kati ya serikali na huo aliyemilikishwa hii itasaidia serikali kujipunguzia mzigo wa matarajio na kuhamisha kwa watu binafsi ambao Wana Nia na uwezo na serikali itanuafaika kwa kupata mapato na sio kutoa mapato kwa ajili ya uwekezeji

Mfano:Kuna maeneo mengi ya halmashauri ya jiji na mengine ya serikali kuu ambayo yapo hapa Dar es Salam ambapo yangeweza kumilikishwa watu binafsi wakaweka miradi ambayo itachochea ajira kwa watu wengi na kusaidia taifa kupata mapato kutokana na faida itakayopatikana na pia purchasing power itaongezeka hatimaye mzunguko wa biashara utakua ni mkubwa na mapato yatakua makubwa pia


Uchumi(misitu) :Kwa kua Tanzania Ina uzalishaji mkubwa wa mbao inastahili serikali kupitia mamlaka husika izuie au kupunguza uingizwaji wa bidhaa zitokanazo na miti kama vile toothpick ambazo nyingi hutoka China madaftari kutoka India na viberiti kutoka Kenya. Serikali itapaswa kuweka nguvu za mikopo ya kifedha na mashine ili kusaidia watu ambao watakua na uwezo wa kuzalisha hatimaye kundi kubwa la wasomi wa juu wakati na hata ambao si wasomi wataweza kupata ajira na soko tegemezi litakua la ndani maana serikali itafanya quota control au kuzuia kabisa kuingizwa

Lakini pia serikali kupitia bodi ya mikopo ya wanafunzi wa ngazi ya juu kutoka na kiasi ambacho wanafunzi wanapewa kama books and stationary kuwe na kiasi kitakachoelekezwa kwa wazalishaji ambapo wanafunzi hawatapata Tena fedha kamili Bali watapata fedha na vifaa vya kusomea kama madaftari penseli nakadhalika. Kwa mfano kama mwanafunzi mmoja alikua anapata 200 000 itapaswa itolewe asilimia kadhaa kama vile asilimia 40% ambayo itaelekezwa kwa wazalishaji kama mikopo na pia wazalishaji watawasilisha vifaa kwa wanafunzi husika na baada ya hapo riba itakayopatikana itakua faida ya bodi ya mikopo hapo bodi yenyewe itaweza kuongeza uwezo wa kukopesha wanafunzi wengi kwa mwaka mmoja


Teknolojia: Kuanzishe mfumo ambao utawasaidia wamiliki wa magari ya mizigo kuweza kupata mizigo yaani (go and return) kwa kua Kuna desturi gari ya mizigo inatoka mfano dar kwenda mkoani ila inarudi ikiwa tupu. Hii inapelekea garama ya usafiri kuongezeka na hatimaye bei za bidhaa kupanda kwa kasi kubwa.
Kwa hiyo bhasi mfumo huo utasaidia wamiliki wa mabasi kua na uhakika kua gari inatoka dar kwenda mkoani Lakini mkoani Kuna mteja Ana mizigo inastahili Kuja dar hivyo mmiliki huyo atasafirisha mizigo kwa bei nafuu na ya kiuchumi. Mfumo huo unaeza kua kama aplikesheni(app) mfano Tz cargo requesting app
Faida ya mfumo huo kwa mmiliki binafsi ni kua itamsaidia kupata mizigo ya kusafirisha atokapo na aendapo

Pia mfumo huo utasaidia kampuni za Bima kwa kua ili mzigo usafirishwe kwa njia itakayokua salama mmiliki wa mizigo atapaswa kukata Bima ya mizigo ili ikitokea ajali iwe salama na rahisi kwa mmiliki wa mizigo kutoka Pata hasara

serikali itanuafaika na mapato yatokanayo na Bima, wamiliki wa mfumo, na wamiliki wa mizigo hii itachochea sekta ya usafirishaji na pia itasaidia bidhaa kushuka bei na hivyo garama ya maisha itapungua
 
Upvote 0
Back
Top Bottom