Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Kuna utitiri wa kozi zinafundishwa vyuoni zinazosababisha unemployment rate katika taifa letu kukua kwa kasi.
Nabadala yake watoto wanahitimu hizo kozi wanabaki hawana ajira lawama zote zinabaki kwa serikali.
Tupo kwenye mchakato wa kubadili mtaala wetu ili uendane na mazingira yetu. Basi tusisahau kuzifuta kozi hizo. Na kozi zote ambazo hazitoi ajira zinajulikana. Wenzangu watazitaja hapa na hata sekretarieti ya ajira inazifahamu kozi hizo.
Kama kuzivuta haiwezekani tunaweza kuziunganisha na kozi nyingine.
Na bila kusahau udhibiti wa idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa kila mwaka. Kuna baadhi ya vyuo vinachukua idadi kubwa ya wanafunzi kwenye kozi zao. Hili nalo ni tatizo tunakua na idadi kubwa ya wahitimu kuliko uhitaji.
Naomba huu uzi usiondolewe kwenye jukwaa hili la siasa ili tupate kuujadili.