Kweni kufanya kwanza marekebisho madogo ya Katiba ya 77 kunahitaji Bilioni ngapi na Miaka mingapi?.Lakini kufanya mabadiliko ya sheria zilizotokana na katiba, bila kutanguliwa na mabadiliko ya katiba, ni superficial changes
Kila jambo linajadilwa kwa wakati wake. Nini Sasa kifanyike na kifanyike vipi ni mjadala mwingine kabisa.Kumkumbusha hilo CCM ni sawa na Mimi hapa kukumbusha wewe kuwa:
"CCM inajifanya kama vile hakujawahi kuwapo kwa mchakato wa kupata Katiba mpya, wakati siyo kweli."
Unadhani wanahitaji kukumbushwa jambo wanalolijua na ambalo kwa hakika wamedhamiria kutoriridhia (kirahisi)?
Kwangu mm nikiona kitu fulani kinafanyika hua nawaza hatua 3 Miele,hii ninayoiona nimaanisha nini huko mbeleni.
Kwa mtazamo wangu ukiona kunabadiliko la jambo la kisheria kazini kwako or serikalini jua kuna jambo wanatakakulifanya na hio sheria ndio itawalinda/kinga kwao soma vzr sana hayo mabadiliko uyaelewe nakuyafanyia kazi otherwise kuna siku yatakudhuru.
In short hio ni kinga Kwa wakubwa kaka Pascal Mayalla
Wanabodi
Hii ni makala ya Jumapili ya leo.
Hili ni bandiko mwendelezo wa bandiko hili Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
View attachment 2775208
Kufanya mabadiliko yoyote ya sheria iliyotokana na vifungu vya katiba, bila ya kufanya kwanza mabadiliko ya katiba, no sawa na kula bila kunawa!. Je Watanzania tuna njaa sana, na tuna haraka sana na uchaguzi ujao, hadi tukimbilie kula bila kunawa?
Dini zote zinatufunza kuwa na shukrani kwa yote, hivyo kikao cha Bunge kijacho, kitapokea miswada kadhaa ya mabadiliko ya sheria za Uchaguzi, Tume ya uchaguzi na Ofisi ya Msajili wa vyama, japo bado sijajua ni sheria zipi zitafanyiwa mabadiliko, hivyo hatua ya kwanza ni kushukuru kwa mabadiliko hayo.
Lakini kufanya mabadiliko ya sheria zilizotokana na katiba, bila kutanguliwa na mabadiliko ya katiba, ni superficial changes!.
Kwa muda mrefu, tumepigia sana sheria kandamizi za uchaguzi na sheria batili zilizochomelewa kiubatili ndani ya katiba yetu!, maadam sasa something is going to be done, let's be appreciative for whatever is going to be done regardless how little it is.
Hapa ni baadhi ya sheria hizo
- Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?
- Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
- Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
- Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza?
- Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
- Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
- Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
- Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
- Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
- Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?
- Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa
- Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
- Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!
Paskali
Mkuu soma andiko vizuriUondoe unafiki wako, chawa wahedi.
Haki haitolewi....tumefanyiwa manipulation....right is what that is due to somebody....Greens 🐍 wanaogopa kutoa HAKI kwa Mpigakura.
Ndeeeeeefuuuuu! Ukifika mwisho unajikuta yale uliyoaanza nayo yote yamefutwa hapo katikati, a maze of contradictions. Mgombea binafsi anabebweaaaa halafu katikati anatupwa pale inspokataza udikteta, I mean Rais binafsi atadhibitiwa na nani? Inakuja dhana ya kuwa lengo la Katiba ni haki na maendeleo, sawa, gafula unakuja ule ugoro wa TLS eti bandari isiendelezwe. Hamna kitu hapa, Ndg Njaa nadhani alikuwa anawahi deadline ya article kabla gazeti kwenda kwa Printer.Wanabodi
Hii ni makala ya Jumapili ya leo.
Hili ni bandiko mwendelezo wa bandiko hili Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
View attachment 2775208
Kufanya mabadiliko yoyote ya sheria iliyotokana na vifungu vya katiba, bila ya kufanya kwanza mabadiliko ya katiba, no sawa na kula bila kunawa!. Je Watanzania tuna njaa sana, na tuna haraka sana na uchaguzi ujao, hadi tukimbilie kula bila kunawa?
Dini zote zinatufunza kuwa na shukrani kwa yote, hivyo kikao cha Bunge kijacho, kitapokea miswada kadhaa ya mabadiliko ya sheria za Uchaguzi, Tume ya uchaguzi na Ofisi ya Msajili wa vyama, japo bado sijajua ni sheria zipi zitafanyiwa mabadiliko, hivyo hatua ya kwanza ni kushukuru kwa mabadiliko hayo.
Lakini kufanya mabadiliko ya sheria zilizotokana na katiba, bila kutanguliwa na mabadiliko ya katiba, ni superficial changes!.
Kwa muda mrefu, tumepigia sana sheria kandamizi za uchaguzi na sheria batili zilizochomelewa kiubatili ndani ya katiba yetu!, maadam sasa something is going to be done, let's be appreciative for whatever is going to be done regardless how little it is.
Hapa ni baadhi ya sheria hizo
- Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?
- Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
- Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
- Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza?
- Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
- Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
- Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?
- Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
- Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
- Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?
- Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa
- Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
- Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!
Paskali
Kila jambo linajadilwa kwa wakati wake. Nini Sasa kifanyike na kifanyike vipi ni mjadala mwingine kabisa.
kuchanganya hoja ni kuuparaganyisha mjadala wenyewe!!
Hoja ya Mayalla inahitaji tafakuri jadidi hasa kwenye kuwaza watu wa kuibeba hiyo dhima ya marekebisho ya Katiba kabla ya uchaguzi wa 2025.
What? Wewe siyo mtanzania? Una-play part gani kwenye kupinga? Au unadhani kuna watu watakutafunia kila kitu? Watanzania bado kabisa. Tunadhani sisi hatuna mchango wowote kwenye mwelekeo wa siasa zetu.Na hao wapinzani watakaokubali utahira huo ndio viini macho vya vyama mbadala... Wtz tunapaswa kupima nafasi ya vyama Kama chadema kupitia hili Jambo!. Kuna kila dalalili ya chadema kuwa "CCM B"
Mkuu soma andiko vizuri
brazaj sasa nimeilewa hoja yako.
Unajua maana ya kuwa kiongozi?What? Wewe siyo mtanzania? Una-play part gani kwenye kupinga? Au unadhani kuna watu watakutafunia kila kitu? Watanzania bado kabisa. Tunadhani sisi hatuna mchango wowote kwenye mwelekeo wa siasa zetu.
brazaj labda inawezekana umechoka kuona tunaendelea tu na mijadala na "kulalamika" bila ya kuwepo Kwa Suluhu la jambo lenyewe.
Lakini hali hiyo imetokana na msingi uliowekwa na TANU na ASP na baadae CCM, msingi ulioweka kanuni ya kuamini zaidi mawazo na maoni ya viongozi dhidi ya watu wa kawaida.
Mpaka sasa watanzania wengi wanaamini kuwa suala la Katiba mpya ni suala la viongozi wa CHADEMA dhidi ya viongozi wa CCM.
Unapoona msomi kama Pasco anaongea mambo ya kuwa na shukrani kwa marekebisho ya Sheria za uchaguzi yatakayofanyika, jiulize watu wa mitaani wanawazaje??
Tatizo kuu ninaliliona mimi ni uwezo mdogo wa watu wenye mawazo mbadala katika kubadili mawazo na mitizamo ya watanzania wengi kuhusu uwezo wao binafsi katika kuchagiza mabadiliko chanya kwa mustakabli wao na vizazi vijavyo.
Lugha inayotumika kuwasilisha hoja Kwa watanzania wa kawaida mara nyingi inaleta mikanganyiko isiyo na sababu na hakuna muendelezo wa hoja kwenye hiyo Agenda ya kulenda mabadiliko.
brazaj huwezi kuweka pembeni ufukarishaji mawazo uliofanywa na CCM kufikia hapa tulipo.
Ni kwa vipi hiyo "movement" mpya itakavyoweza kuzaliwa nje ya tamaduni zetu za kisiasa bila ya uwepo wa uasi wa kifikra??
Hawa kina Pasco wanaouma na kupuliza siyo watu wa kutegemeka hata kidogo.
Misimamo thabiti haijengwi na watu wenye hasira peke yake, bali na watu wenye uthubutu wenye malengo bayana na watu jasiri.
Bahati mbaya hatuwezi kufikia viwango hivyo bila ya kuwa na falsafa tunayoisimamia na kuipigania.
Kuchukia matendo ya CCM pekee hakutoi fursa ya kuwepo kwa hiyo "movement" unayoitamani.
Lakini pia tuna upungufu wa watu wa kuaminiwa uadilfu wao na wenye dhamira zisizotiliwa shaka kuwa wana malengo binafsi.