brazaj labda inawezekana umechoka kuona tunaendelea tu na mijadala na "kulalamika" bila ya kuwepo Kwa Suluhu la jambo lenyewe.
Mkuu imebidi nikujibu kwa urefu kama ulivyokuja:
Kuchoka si mimi tu bali pamoja na watanzania wengi, bila shaka wasiokuwa CCM au vibaraka wao (kwa kujua au kutokujua).
Lakini hali hiyo imetokana na msingi uliowekwa na TANU na ASP na baadae CCM, msingi ulioweka kanuni ya kuamini zaidi mawazo na maoni ya viongozi dhidi ya watu wa kawaida.
Ninadhani hata hao CCM wanafurahi sana tunapolitafuta tatizo letu kwao (au hata TANU) tukiliacha likiendelea kutula nguoni mwetu.
"Ukweli mchungu matatizo yetu tunayo sisi wenyewe."
Kwamba tumekuwa wagumu wa kutumia akili zetu kuchambua mambo? Kwamba tunataka nani kutuamulia sisi lililo jema au baya au nini tufanye?
Hapa ndipo umuhimu wa demokrasia unapokuja, tena across the board hadi vyamani huko. Kungeharibika vipi jambo penye wengi?
"Kwani beberu hadi akawa na primaries hakuyaona haya?"
Mpaka sasa watanzania wengi wanaamini kuwa suala la Katiba mpya ni suala la viongozi wa CHADEMA dhidi ya viongozi wa CCM.
Hili si kweli hata kidogo. Tatizo letu ni ubinafsi. Vingine ni visingizio. Tumeshindwa kujifunza kote, hata ambako harakati kama hizi zimefanikiwa au zinashika kazi.
"Kutokuwa na maadui wa kudumu wala marafiki wa kudumu bali agenda, kumeshindwa kueleweka."
Agenda inaweza kuizidi mashiko agenda ya kupata katiba mpya kiasi hata cha kutaka kuiweka rehani, kwa mfano?
Unapoona msomi kama Pasco anaongea mambo ya kuwa na shukrani kwa marekebisho ya Sheria za uchaguzi yatakayofanyika, jiulize watu wa mitaani wanawazaje??
Binafsi nina matatizo na bwana
Pasckali kwenye kuuma na kupulizia tu. Japo kiutu uzima ninadhani anafanya hivi kutokana na kuwa ameng'amua kwa mwendo huu, hatutoboi leo.
"Kwamba labda kaamua kumtumikia kafiri apate mradi wake (angalau kwa muda)."
Ni mawazo yangu kuwa bila shaka kukitokea serious movement yenye kuonyesha uelekeo ulio bayana kabisa, anaweza kuwa siyo huyu tunayemwona.
Pia kwenye struggle tusipende kusikia tunayopenda tu. Wakosoaji ndiyo wanao shape uelekeo.
Kumsoma
Paskali, ukae uvute fundo kama wala muwa, yakhe. Vinginevyo utamtakia heri na teuzi ambazo kwa hakika akitunukiwa hatakataa na pia labda hatakuwa kama kina nani hii ..
Tatizo kuu ninaliliona mimi ni uwezo mdogo wa watu wenye mawazo mbadala katika kubadili mawazo na mitizamo ya watanzania wengi kuhusu uwezo wao binafsi katika kuchagiza mabadiliko chanya kwa mustakabli wao na vizazi vijavyo.
Sidhani ndugu. Nionavyo tatizo hapa ni kukosekana kwa demokrasia ya kutosha kuhakikisha mawazo na watu walio bora kabisa tunaoweza kuwa nao, wako pote panapostahili.
"Dhana ya kuwa vyama hivi ni vya wanachama haiwezi kupuuzwa."
Lugha inayotumika kuwasilisha hoja Kwa watanzania wa kawaida mara nyingi inaleta mikanganyiko isiyo na sababu na hakuna muendelezo wa hoja kwenye hiyo Agenda ya kulenda mabadiliko.
Mkuu si lugha. Bali Kwa maoni yangu:
"Maneno matupu hayavunji mfupa."
Ni lazima uelekeo uwe ni vitendo:
Habari ndiyo hiyo.