Viongozi wanatakiwa kuongoza kwa mfano.
Kama wananchi wanaweza kushitakiwa, viongozi, wote, waweze kushitakiwa.
Tena viongozi ndiyo wanatakiwa waweze kushitakuwa kirahisi zaidi ya wananchi wengine.
Noblesse oblige.
To whom much is given, much shall be required.
Ukimpa mtu A mtaji wa shilingi milioni mia moja, na mtu B mtaji wa shilingi milioni moja, kimantiki, utataka upate faida kubwa kwa mtu aliyepewa mtaji mkubwa.
Hata misahafu imeongelea suala hili.
The parable of talents talks about this. I am quoting this from a historical and philosophical context, not a religious one.
Matthew 25:14–30 Luke 19:11–27
Sasa, uongozi ni mtaji wa kijamii. Ni dhamana. Ukipewa uongozi, umepewa nguvu kubwa.
Kwa nini tunataka waliopewa nguvu kubwa wasidaiwe kuwajibika, na wale ambao hawajapewa nguvu ya uongozi wawajibike?
Yani ni kama tunasema mtu aliyepewa mtaji wa shilingi milioni mia moja akafanye biashara, tusimdai faida ya biashara, halafu mtu aliyepewa shilingi milioni moja tumdai faida ya 100% !
Huu ujinga wa kufanya mambo kinyumenyume tunauhalalisha vipi?