mabadiliko ya sheria ya ndoa

mdome

Member
Joined
Jul 30, 2013
Posts
8
Reaction score
0
Habari zenu wadau msaada kwenye tuta katika mchakato wa kubadilisha au ku ammend baadhi ya vifungu katika sheria ya ndoa je mchakato huo umefikia wapi kwa sasa? Au ni mapendekezo gani yaliyotolewa?
 
Habari zenu wadau msaada kwenye tuta katika mchakato wa kubadilisha au ku ammend baadhi ya vifungu katika sheria ya ndoa je mchakato huo umefikia wapi kwa sasa? Au ni mapendekezo gani yaliyotolewa?
hakuna mchakato utakaokuwa mgumu kama huu hapa tz, kwasababu siku hizi kuna mwamko sana wa haki za binadamu na wapigania haki za wanawake ambao wengi wanapinga sheria ya ndoa kwa upande huu wakati wapo wengine wanaopinga kwa upande mwengine.

nitakupa mfano. mojawapo ya vifungu vinavyokwaza wengi kwenye sheria ya ndoa ni kwamba, mtoto wa miaka 14 anaweza kuolewa kwa ruhusa ya mahakama. yule wa miaka chini ya kumi na nane 18 lakini si chini zaidi ya 15 anaweza kuolewa kabisa kwa ruhusa ya wazazi/walezi wake. wanaharakati wanasema kuwa, kipengele hiki kinamnyima mtoto haki yake kisheria, haki ya kupata elimu na haki ya kufurahia maisha yake ya utoto (kuna mengi ndani yake) wakiwa na maana kuwa mtoto wa miaka 14 akiolewa atakosa elimu na mambo mengi ambayo watoto wenzie wanayapata.

wakati huohuo, kiimani, baadhi ya dini msimamo wao ni kwamba, hawatakiwi kupangiwa na sheria za kibinadabu ni wakati gani binti anatakiwa kuolewa, bali kile kilichoandikwa ndicho kinachotakiwa kufuatwa. kwa maana hiyo, mtoto akishavunja ungo tu kwa sheria za kiislam anaweza kuolewa (siku hizi kuna watoto wengine wanavunja ungo miaka hata 10). HOWEVER, ningependa kuongelea hili, pamoja na kwamba mimi sio muislam, neno "kuolewa" kwa waislam ninaamini kuwa halimaanishi kuwa mwanaume akishamchukua mwali tu anaanza kufanya naye tendo, nimeambiwa kuwa huwa wanasubiri hadi binti akue, hivyo unaweza kuoa lakini haufanyi naye ngono hadi akue. nadhani hilo si jambo baya kama linaendana na imani ya mtu, kila mtu afuate kama vile imani yake inavyosema....siwapingi hata kidogo. hivyo watu msije na maneno mabaya hapa mkifikiri kila anayeolewa umri mdogo huwa analalwa,,,hapana.

hivyo basi, kuna mkanganyiko kama huo, utalalia upande gani sasa hapa tz, upande wa wanaharakati hawa wa kimagaribi au ndugu zetu waislam tutakubaliana nao vipi, sheria iweje ili iwe katikati, isiwe upande wowote ili kila mtu asiwe na manung'uniko?...kuanzisha mchakato wa kurekebisha sheria hii haitakiwi kwenda haraka haraka, ni polepole ili tusijesababisha mvutano wa kidini. hayo ni mawazo yangu, kwasababu ninaamini kuwa ni haki yao kila raia wa tz kusikilizwa hisia zao hata kama ni za kidini, zipimwe halafu muafaka ufikiwe kwa mezani, then tunaendelea kuishi. nchi hii ni ya kwetu sote hata kama tunatofautiana imani hivyo lazima tuwe tunahakikisha kuwa chochote kinachofanyika kinakuwa kimewekwa mezani tukakijadili na kufikia muafaka. SHERIA KWA KISWAHILI
 
msaada!
Sheria ya ndoa inabainisha kuwa mume na mke mkika pamoja zaidi ya miezi mitatu tayari nyinyi ni mume na mke, sasa je! Mwanaume ukimtolea mwanamke mahali harafu hukuweza kukaa naye ndani ya mwaka mmoja yeye yupo kwao na mwanaume yupo kwao je! Hawa ni wanandoa au mume na mke?
 
Unachokisema wewe kinaitwa presumbition of marriage. Kwasheria za ndoa(nimesahau kifungu) presumbition ni miaka 2 na sio miez kma unsvosema,sio general rule kua ukikaa na mwamke kwa miaka miwili basi nyie mnakua pressumed kama mke na mme kuna vitu vngne vinaangaliwa.ndoa zip za aina mbili zinatambuliwa kisheria mbazo ukienda hata maakamani kuzivunja(divorce)zinaeleweka nazo ni ndao za kidini(kanisan na msikitini) na ndoa za kiserikali.(bomani)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…