Mabadiliko ya wakuu wa mikoa na dhana ya kuchochea uwajibikaji

Mabadiliko ya wakuu wa mikoa na dhana ya kuchochea uwajibikaji

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2019
Posts
305
Reaction score
728
Kwa mara nyingine Rais Samia Suluhu anaendelea kuonyesha aina ya uongozi unaojali uwajibikaji na usio toa nafasi ya kufanya kazi kwa mazoea. Falsafa hii ni muhimu kwa Taifa linalohitaji matokeo ya haraka na linalojali uwazi na uwajibikaji.

Kwasasa kila atakaye pewa nafasi kwa kuteuliwa katika Uongozi atalazimika kuwa na uhakika kuwa dhamana aliyopewa ni kuwatumikia watanzania sawa sawa na kiapo chake na asipofanya hivyo atawajibishwa. Taswira pana ya uteuzi uliofanywa;

1. Uteuzi kuzingatia taaluma, uzoefu wa kiuongozi unaohitajika kusimamia serikali ya Mkoa husika.

2. Uteuzi kuzingatia rekodi ya uadilifu na uchapakazi usio tia shaka, hususani katika majukumu ya utumishi wa umma.

3. Uteuzi kuzingatia mahitaji ya sasa ya nchi katika nyanja za uwekezaji na mapinduzi ya kilimo, ufugaji na uvuvi kulingana na Mkoa husika.

4. Uteuzi kuzingatia ujumuishi na usawa wa kijinsia hususani katika kuwawezesha wananchi kutoka katika makundi rika yote.

5. Uteuzi kuzingatia mahitaji ya Mkoa husika na fursa zilizopo katika nyanja za uwekezaji.

6. Uteuzi kuzingatia uwakilishi wa viongozi kutoka maeneo yote nchini bila upendeleo wa udini au ukabila na badala yake sifa zinazohitajika.

Utamaduni huu wa kupokezana vijiti ndio falsafa kubwa inayosadifu mabadiliko yanayolenga kuleta ustawi katika Taifa letu, shime tuwape ushirikiano wateule katika majukumu yao.

#MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Back
Top Bottom