Mabaki ya ‘jitu’ la ajabu yafukuliwa, yana vidole 6

Mabaki ya ‘jitu’ la ajabu yafukuliwa, yana vidole 6

Hashpower7113

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
1,353
Reaction score
2,142
Inafahamika kwamba binadamu wa kawaida, akizidi sana basi anakuwa na urefu wa futi 7 na hapo kila mtu anamshangaa! Hashim Thabeet, mcheza kikapu wa nchini Marekani mwenye asili ya Tanzania, ana urefu wa futi 7.2 na kila mtu anamshangaa, sasa vuta picha, jitu lenye urefu wa futi 12 litakuwaje?

Desemba 1895, ulikuwa ni mwezi wa kipekee baada kutokea tukio la ajabu nchini Ireland kwenye eneo la machimbo la Antrim. Inaelezwa kwamba wakati mchimbaji mmoja wa madini ya chuma aitwaye Dyer, akiwa kwenye kazi yake aligundua kitu ambacho mpaka leo hakuna anayeweza kukitolea majibu ya kueleweka.

Yalikuwa ni mabaki ya binadamu anayetajwa kuwa mkubwa zaidi kuwahi kugundulika, akiwa na urefu wa futi 12, upana wa kifua wa futi 6, mikono yenye urefu wa futi 4.6 kila mmoja na vidole sita kwenye mguu wa kulia na kwenye mikono yote miwili.

5660010_orig.jpg

Yote tisa, kumi ni kwamba jitu hilo lilikuwa na uzito unaokadiriwa kuwa tani 2, jambo lililowalazimu mgunduzi na watu waliokuwa wa kwanza kuyaona mabaki hayo, kutumia ‘winchi’ kulitoa eneo lilipokutwa.

Baadaye jitu hilo lilipigwa picha iliyotoka kwa mara ya kwanza kwenye Gazeti la The British Strand mwezi huohuo na kuzua gumzo kubwa dunia nzima, wengi wakiwa hawaiamini habari hiyo huku wengine wakiamini na kuihusisha na maandiko katika Biblia Takatifu, Kitabu cha 2 Samuel 21:20

Baada ya hapo, jitu hilo lilisafirishwa kwa treni mpaka jijini Dublin lilikowekwa kwenye makumbusho kabla ya kuhamishiwa katika Miji ya Liverpool na Manchester na baadaye kuishi jijini London kwenye Makumbusho maalum ambapo maelfu ya watu walianza kufurika kwenda kuliona jitu hilo la ajabu, kila mmoja akilazimika kulipia kiwango fulani cha pesa ili kujionea maajabu hayo.

Hata wale ambao awali hawakuwa wakiamini, baada ya kujionea wenyewe mabaki hayo walianza kuamini, swali likabaki kuwa jitu hilo ni nani, liliishi miaka gani, nini kilichosababisha likafa na lilikuwa likiishi vipi maisha yake ya kawaida?

irish-giant.jpg

Watu wakawa wanaumiza sana vichwa kutaka kujua kwamba lilitokea wapi na uzao wake umeishia wapi? Limewahi kupata watoto? Hao watoto wako wapi? Kwa nini lilikuwa kubwa kiasi hicho? Hayo ni miongoni mwa maswali mengi ambayo mpaka leo hayajapatiwa majibu.

Utata mwingine ulikuja kuibuka kuhusu mtu ambaye ndiye aliyekuwa anatakiwa hasa kufaidika na fedha zilizokuwa zinalipwa na maelfu ya watu kutaka kuona mabaki ya jitu hilo, mgogoro ukawa mkubwa na baadaye, haikujulikana nini kilitokea lakini mabaki ya jitu hilo yalitoweka na mpaka leo, uthibitisho pekee ambao unaweza kupatikana ni picha tu lakini mabaki yake yamebaki kuwa historia!
 
Duniani kuna mambo na tulikotoka Mbali....tuendako mbali

Kokote Kule hatujuwi vema hasa tulikotoka nakule tuendako.

Historia inajitahidi kutukumbusha walau kwa uchache tulikotoka.
 
Kwa ushahidi wa picha pekee? tena picha zenyewe za 1800 kweusi... ina maana kina Livingstone na mwanahistoria maarufu Dr. Leakey hawakupata kujua uwepo wa jitu hilo? Nimejaribu kulinganisha ukubwa wa kichwa na hao wachimbuzi naona ni zaidi ya futi kumi na mbili zilizoandikwa kwenye "heading!" mwisho wa siku naiona ni habari ya kubuni tu afadhali za wanefili na Unju zina mashiko kwani masalia ya majengo yao yanapatikana Sham na Yemen...

Yawezekana mkuu, sema hii inaenda mbele zaidi kwa kuwa na ushahidi unaoweza kukufanya ukaamini tofauti na zile hekaya za mwanzo.

Mbona hata mimi nilizaliwa na vidole sita
Mkuu usiseme na urefu wako hapo 😉😎😁 ....lingekuwa la ajabu kama lingekuwa na vidole kama mbuni... 😀
 
Siwezi kupingana na ulichokiandika, kwa sababu hapo zamani matumizi ya nguvu yalikuwa makubwa kuliko akili.Ndio maana ubongo wa binadamu wazamani ulikuwa mdogo kulinganisha na body ratio yake, tofauti na binadamu wasasa ambao ubongo wao ni mkubwa ukilinganisha na body ratio yao kuliko ule wakina Zinjanthropus. Ndio maana ukisoma vitabu vingi vya historia vinaelezea sana hii issue ya Giantism na kufika kuelezea kwamba hili uweze kufit katika mazingira ya zamani ulitakiwa uwe na nguvu ndio inakuja issue ya (survival of the fittest) only the strong survive.
 
Siwezi kupingana na ulichokiandika, kwa sababu hapo zamani matumizi ya nguvu yalikuwa makubwa kuliko akili.Ndio maana ubongo wa binadamu wazamani ulikuwa mdogo kulinganisha na body ratio yake, tofauti na binadamu wasasa ambao ubongo wao ni mkubwa ukilinganisha na body ratio yao kuliko ule wakina Zinjanthhropus . Ndio maana ukisoma vitabu vingi vya historia vinaelezea sana hii issue ya Giantism na kufika kuelezea kwamba hili uweze kufit katika mazingira ya zamani ulitakiwa uwe na nguvu ndio inakuja issue ya (survival of the fittest) only the strong survive.
Umeeleza vyema mkuu! Na hata maandiko matakatifu (Biblia) yanawataja sana hawa Giants. Soma 2 Samuel 21:20
 
Ukubwa wa fuvu ambalo jamaa wawili wameliinamia hauendani na fuvu la kwenye casket pia fuvu la kwanza ni Kama kichwa na kiwiliwili vimeshaachana wakati fuvu la kwenye kasket lipo intact hii nadhani Ni chai Kama ya mwalimu kashasha
 
Hayo katika picha ni masanamu yaliyochongwa au kufinyangwa kwa udongo tu, hakuna uhalisia. Mabaki halisi yako wapi? Tukio kubwa kama hili, mabaki yake hayawezi kutoweka kirahisirahisi tu hivi hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo kama si Awafu nwenye nguvu basi ni zimwi danta (rejea hadithi ya danta na halifa kwa wahenga)
 
Back
Top Bottom