Mabaki ya ‘jitu’ la ajabu yafukuliwa, yana vidole 6

Mabaki ya ‘jitu’ la ajabu yafukuliwa, yana vidole 6

Inafahamika kwamba binadamu wa kawaida, akizidi sana basi anakuwa na urefu wa futi 7 na hapo kila mtu anamshangaa! Hashim Thabeet, mcheza kikapu wa nchini Marekani mwenye asili ya Tanzania, ana urefu wa futi 7.2 na kila mtu anamshangaa, sasa vuta picha, jitu lenye urefu wa futi 12 litakuwaje?

Desemba 1895, ulikuwa ni mwezi wa kipekee baada kutokea tukio la ajabu nchini Ireland kwenye eneo la machimbo la Antrim. Inaelezwa kwamba wakati mchimbaji mmoja wa madini ya chuma aitwaye Dyer, akiwa kwenye kazi yake aligundua kitu ambacho mpaka leo hakuna anayeweza kukitolea majibu ya kueleweka.

Yalikuwa ni mabaki ya binadamu anayetajwa kuwa mkubwa zaidi kuwahi kugundulika, akiwa na urefu wa futi 12, upana wa kifua wa futi 6, mikono yenye urefu wa futi 4.6 kila mmoja na vidole sita kwenye mguu wa kulia na kwenye mikono yote miwili.


Yote tisa, kumi ni kwamba jitu hilo lilikuwa na uzito unaokadiriwa kuwa tani 2, jambo lililowalazimu mgunduzi na watu waliokuwa wa kwanza kuyaona mabaki hayo, kutumia ‘winchi’ kulitoa eneo lilipokutwa.

Baadaye jitu hilo lilipigwa picha iliyotoka kwa mara ya kwanza kwenye Gazeti la The British Strand mwezi huohuo na kuzua gumzo kubwa dunia nzima, wengi wakiwa hawaiamini habari hiyo huku wengine wakiamini na kuihusisha na maandiko katika Biblia Takatifu, Kitabu cha 2 Samuel 21:20

Baada ya hapo, jitu hilo lilisafirishwa kwa treni mpaka jijini Dublin lilikowekwa kwenye makumbusho kabla ya kuhamishiwa katika Miji ya Liverpool na Manchester na baadaye kuishi jijini London kwenye Makumbusho maalum ambapo maelfu ya watu walianza kufurika kwenda kuliona jitu hilo la ajabu, kila mmoja akilazimika kulipia kiwango fulani cha pesa ili kujionea maajabu hayo.

Hata wale ambao awali hawakuwa wakiamini, baada ya kujionea wenyewe mabaki hayo walianza kuamini, swali likabaki kuwa jitu hilo ni nani, liliishi miaka gani, nini kilichosababisha likafa na lilikuwa likiishi vipi maisha yake ya kawaida?


Watu wakawa wanaumiza sana vichwa kutaka kujua kwamba lilitokea wapi na uzao wake umeishia wapi? Limewahi kupata watoto? Hao watoto wako wapi? Kwa nini lilikuwa kubwa kiasi hicho? Hayo ni miongoni mwa maswali mengi ambayo mpaka leo hayajapatiwa majibu.

Utata mwingine ulikuja kuibuka kuhusu mtu ambaye ndiye aliyekuwa anatakiwa hasa kufaidika na fedha zilizokuwa zinalipwa na maelfu ya watu kutaka kuona mabaki ya jitu hilo, mgogoro ukawa mkubwa na baadaye, haikujulikana nini kilitokea lakini mabaki ya jitu hilo yalitoweka na mpaka leo, uthibitisho pekee ambao unaweza kupatikana ni picha tu lakini mabaki yake yamebaki kuwa historia!
Huyo ndiye aliyeuawa na waisrael kule agano la kale kwani alikuwa na vidole sita mkononi na mguuni.
Mungu anaendelea kufunua neno lake.
Imani yangu ni hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona hata mimi nilizaliwa na vidole sita
Ni sawa wala si ajabu but chromosomal DNA zako uko connected na hawa watu wa kale ''Giant of the old'' hili ni somo kabisaa linajitegemea, kwa wakristo si mnajua Goriath, mfalme ogu wa Bashan, Samson, Pharaoh lamseh haya yalikuwa ni majitu hasa.yaani watu wa leo ni km panzi tu!

Kila kabila au jamii Duniani kote kuna hadithi ya mijitu mikubwa ya kale, mfano kabila la Wajita au waruli kama mko humu ndani waliliita ''Wesumwa Amakaka'' kuna kale ka wimbo wanaimbaga .... 'Kagoma lila lila dondori! nibirikile wesumwa dondori! ....... ila yaliondolewa kutoka uso wa dunia na deluge kwa sababu ya ubabe wao! kwa mujibu wa Sumerian cuneiform.

unaendaga kutambikia?
 
Back
Top Bottom