Mabalaa humuandama mtoto wa kike tangu akiwa tumboni…………

Mabalaa humuandama mtoto wa kike tangu akiwa tumboni…………

mtambuzi umenigusa sanaaaa...kwanza ni wanaume wachache wanaochukulia sawa mtoto wa kike na wa kiume.mwanamke anapozaa watoto wa kike mfululizo anajisikia vibaya moyoni kama yeye ndo kasababisha.jaman kwani watoto wote si ni sawa?kwanini wa kiume ndo aonekane wa maana wa kike ni mkosi?jaman tubadilike,mtoto ni mtoto,kuna wengine wanakesha kuomba hawapati.afterall utafiti unaonyesha ukimuendeleza mtoto wa kike atakuja kukusaidia sana mbeleni
 
Watoto wa kike, haswa wale wanaozaliwa nje ya ndoa wametelekezwa kirahisi, wamekataliwa na baba zao kirahisi, ukilinganisha na watoto wa kiume. Idadi ya watoto wa kike wanaokufa kutokana na kutelekezwa na kukataliwa na baba zao ni kubwa kuliko ya watoto wa kiume. Hata zile kesi nyingi za watoto kukataliwa na baba zao zinahusisha watoto wa kike zaidi. Ni jambo la kushangaza kwamba ndoa ambayo ina watoto wa kike watupu hutazamwa kwa bezo na dharau ukilinganisha na ile yenye watoto wa kiume watupu. Hata wale wanawake wanaozaa watoto wa kike watupu hujihisi vibaya na kuamini kwamba walistahili kuzaa watoto wa kiume pia.Kwa maeneo ya vijijini na katika familia masikini, watoto wa kike hutazamwa kama, ‘biashara ya kesho' ambapo watauzwa kwa njia ya mahari.

Kwa hiyo thamani yao ni kuolewa, ni ile ya kibidhaa na sio kibinadamu. Na ndio maana mtoto wa kike anaposhindwa kuolewa huanza kuonekana kama mzigo usio na thamani, na hata kuzongwa hutokea. Ili kujinasua na tatizo hili, msichana huenda kwa mwanaume yeyote kama kwa kujilazimisha. Kila mtu anajua kuhusu wazazi hapa nchini, ambao wamekuwa wakiwalazimisha binti zao kurudi kwenye ndoa za mateso kwa hofu ya kurejesha mahari. Kinachotokea ni binti hao kuuawa na waume zao. Ni wazi hii ni njia ya makusudi ya kuwapunguza wanawake, bila kujali mtu ataieleza vipi……………….

Umemaliza kaka, nimewahi kushuhudia ndoa iliyovunjika kwa sababu tu mke amezaa watoto wa KIKE WATUPU, si hivyo tu, bali pia wanume wengi wanweza kupata kisingizio cha kutoka nje ya ndoa ili kutafuta mtoto wa kiume, wao wanaamini kama mkewe ameshindwa kumpatia mtoto wa kiume, ambaye ndiye anayechukuliwa kama mrithi, basi mke huyo anakuwa hafai.

Mtoto wa kike ameanza kubagukiwa kuanzia katika familia, jamii, mila na desturi zetu, na hata DINI zetu hizi za mapokeo, nazo pia zimemuweka mwanamke chini sana. lakini tumeona mifano mingi ya jinsi wanawake wanavyomudu majukumu yao, tukiachili mbali wale wachache walioboronga kwa hapa nchini, lakini ukitazama zile wizara zilizoshikwa na wanwake waliojitambua na wenye uwezo wa kuongoza tumeona matunda yake.......... angalia nchi zilizoongozwa na zila zinazoongozwa na wanawake, zimepiga hatua kubwa sana........... namkumbuka sana hayati Quarazon Aquino aliyewahi kuwa Rais wa Philipines, aliitoa nchi ile katika hali ya ulitima na kuiwezesha kumudu kusimama tena. licha ya kuandamwa na wapinzani wake...........................

Lipo jambo moja, wanawake kutopendana, hili kw akiasi kikubwa linawaangusha mama na dada zetu..............ukiangalia waliofungua madanguro ya kuwafanyisha wanawake biashara ya ngono ni wanwake hao hao, wanaofuata watoto wa kike vijijini na kuwaleta mijini na kuwauza kwa ajili ya kufanyishwa kazi za majumbani ni wanawake, wanaopenda kusengenyana na kufanyiana fitina ni wanawake................

Niliwahi kumsoma mwana JF mmoja hapa nadhani ni PRETA, aliwahi kusema ni bora uwe na rafiki wa kiume kuliko wa kike, akimaanisha platonic friend.
Kwa nini? ni kwa sababu wanawake hawaaminiani, wanachukuliana hata wanaume........................ nilimsikia mmoja akisema, 'kama ukimsifia mumeo au mpenzi wako kwa mashoga zako, ni rahisi kuporwa'
 
vipi wa kiume unaye?? tusaidiane kumpata wa kike basi
Ninae wa kiume ndio. Tusaidiane basi ndugu yangu!

MJ1 si uzae na we ujilelee kabinti kako! Au nisubiri mi nikizaa nikuletee.......lol! Yaani article ya mtambuzi imejaa ukweli alafu imegusia kwa kiasi kikubwa halisi ya maisha ya mtoto wa kike!

Hahahha kipipi mpenzi haya ngoja niongeze bidii katika nyanja hii maana naona nimekuwa mvivu kidogo kwani huyu nnliyenaye naona ashaanza kuniletea kibesi flan hivi na vijipele vya ndevu vinaanza kutoka hahahahahaha

Unaweza kuasili pia.............

Niko kwenye mchakato Mtambuzi, yule wa Morogoro namtamani kweli!
 
Niko kwenye mchakato Mtambuzi, yule wa Morogoro namtamani kweli!

Ni jambo jema, lakini Je unazijua taratibu za kuasili hapa nchini? maana usidhani unakwenda kuchukua kama vile mtoto wa nduguyo, kuna taratibu za kisheria lazima usifuate...............
 
Mtambuzi aksante sana. I wish ningewezakuishi na Binti yangu wa kufikia............... !

Ila natafuta jamani Binti!!

vipi wa kiume unaye?? tusaidiane kumpata wa kike basi

Ninae wa kiume ndio. Tusaidiane basi ndugu yangu!

Hahahha kipipi mpenzi haya ngoja niongeze bidii katika nyanja hii maana naona nimekuwa mvivu kidogo kwani huyu nnliyenaye naona ashaanza kuniletea kibesi flan hivi na vijipele vya ndevu vinaanza kutoka hahahahahaha

Niko kwenye mchakato Mtambuzi, yule wa Morogoro namtamani kweli!

...ongezeni imani, kwa mwenyezi mungu hakuna linaloshindikana, ....hata nami mbu baada ya miaka ya kuomba na imani
hatimaye nimejaaliwa mtoto wa kike.... mungu ni mkubwa....saidianeni nami nawaweka kwenye maombi.
 
Hii sredi imenifanya nirudi tena kwenye kale kautafiti kangu...........

Subiri...!
 
...ongezeni imani, kwa mwenyezi mungu hakuna linaloshindikana, ....hata nami mbu baada ya miaka ya kuomba na imani
hatimaye nimejaaliwa mtoto wa kike.... mungu ni mkubwa....saidianeni nami nawaweka kwenye maombi.
Hebu weka maombi na mie nipate toto la kiume.

Mi nadhani nimeumbwa kwa ajili ya kuongeza mabinti duniani aisee.
 
mungi,to some of us women, the power lies in proving our oppressors wrong! when no one believes in u,u just look inside and see all the motivation u need! and in the end u ralise there is a here inside u and the sky is nt even the limit anymore coz u can go beyond!
big up to all my opressors, i lov u more than u can imagine,hahaha!
I don't see the women empowerment here, post nyingi zina discuss wanawake tu!
 
vipi wa kiume unaye?? tusaidiane kumpata wa kike basi

MJ1 si uzae na we ujilelee kabinti kako! Au nisubiri mi nikizaa nikuletee.......lol! Yaani article ya mtambuzi imejaa ukweli alafu imegusia kwa kiasi kikubwa halisi ya maisha ya mtoto wa kike!

...ongezeni imani, kwa mwenyezi mungu hakuna linaloshindikana, ....hata nami mbu baada ya miaka ya kuomba na imani
hatimaye nimejaaliwa mtoto wa kike.... mungu ni mkubwa....
saidianeni nami nawaweka kwenye maombi.
Mbu hujambo?
 
Hebu weka maombi na mie nipate toto la kiume.

Mi nadhani nimeumbwa kwa ajili ya kuongeza mabinti duniani aisee.

...amini mw'mungu nae atakuaminisha kwa uaminifu wako. Dua yako inajibiwa kwamba kila jambo linasababu na utukufu wake, furahia majaaliwa yako, Amen
 
Back
Top Bottom