So longer bado anapangwa na anacheza pale mbele ya goli ipo siku atakutana na mpira umepotea njia atafunga tu. Na kwa jinsi baadhi ya viongozi, wanachama na msemaji wao wasivyojua mpira utasikia tambo zao. Kwa vyovyote vile Doumbia sio mshambuliaji sahihi wa kuivusha Simba kutoka hapa ilipokwama kwenye ligi na mashindano ya CAF
Watu wengi wanapenda mpira lakini sio wafuatlliaji. Huyo Doumbia kule kwao ana namba nzuri sana za magoli. Lakini idadi kubwa ya magoli yake kafunga kwa penati na vichwa. Lakini hayo ya vichwa ni "free header". Ndio maana anapata taabu sana kufunga hapa kwenye ligi yetu kwa sababu mabeki hata wa timu ndogo hawampi hiyo nafasi ya kuruka mwenyewe.
Namlaumu sana huyo aliyemsajili pale Simba. Kwani inaonekana aliaangalia zaidi namba hata "clipi" hakuangalia vizuri. Kwa uchezaji wa Doumbia hata ukiaangalia tu "clip" kwa mtu anayefahamu mpira vizuri aidha asingemsajili moja kwa moja kabisa au angesubiri kwanza amuone kwenye majaribio ajiridhishe ndio amsajili.
Ni mtizamo tu.