Tanzania hakuna udini ila kuna kujuana.Sioni sehemu yeyote udini umetumika kwenye hii nchi ya kifisadi ila je wewe ni mwanamtandao, na mtandao wako ni wa nani. haijalishi kabila, rangi, dini, elimu, wala lugha kama wewe ni fisadi mambo kanyaga twende utapelekwa kokote na utakuwa yeyote. kama wewe unamsujudia mkulu mambo ni vilevile. Kikwete na lowasa hawakuwa dini moja. Wala kikwete na membe sio dini moja wala kabila moja.kikwete na Karamag sio kabila moja, Hivyo mimi sioni kama kuna udini kama washika dau wengi wanavyotaka kuleta ila wakati wa kampeni wanatumia vigezo vya dini kupigia kampeni misikitini na makanisani kwa sababu zao na ujinga wetu sisi wapiga kura.
Tusiogope vivuli vyetu bali fikra zetu.