Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Mabalozi wapya wanolewa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amefungua rasmi mafunzo kwa mabalozi wapya yenye kuwaongezea uelewa na ujuzi kabla ya kuelekea katika vituo vyao nje ya nchi.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam Mhe. Waziri Kombo amewaasa mabalozi hao kutambua kuwa nafasi waliyopata inawafanya wao kuwa wawakilishi wa kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika nchi wanazoenda na hivyo wawe mstari wa mbele kukuza ushirikiano kati ya nchi yao na nchi mwenyeji kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.
Waziri Kombo amewataka mabalozi hao kutambua kuwa zipo changamoto katika vituo wanavyoenda na wahakikishe wanaziondoa au kuzipunguza kwa kiwango kikubwa changamoto hizo.
Aidha, Mhe. Waziri Kombo amewahimiza mabalozi hao kuwa wabunifu katika kutekeleza majukumu yao na kuiagiza Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Wizarani kuhakikisha mafunzo hayo yanakuwa ya kina na yagusie intelijensia ya uchumi, diplomasia ya umma na mfumo wa PEPMIS.
Kwa upande wake mtoa mafunzo, Balozi Charles Sanga amewaeleza Mabalozi hao wapya kufanya rejea katika nyaraka zote muhimu ikiwemo Waraka wa Rais wa mwaka 1964 ili kuelewa namna ya kuwasiliana na mabalozi wengine.
Pia amewasisitiza wenza wa mabalozi wakawe washauri wazuri kwa wenza wao wanapotekeleza majukumu yao katika vituo walivyopangiwa.

Attachments
-
FB_IMG_1741626299930.jpg21.1 KB · Views: 2 -
FB_IMG_1741626295171.jpg33.7 KB · Views: 1 -
FB_IMG_1741626297747.jpg32.5 KB · Views: 1 -
FB_IMG_1741626308370.jpg28.6 KB · Views: 1 -
FB_IMG_1741626310735.jpg23 KB · Views: 2 -
FB_IMG_1741626320790.jpg24.7 KB · Views: 1 -
FB_IMG_1741626318577.jpg37 KB · Views: 1 -
FB_IMG_1741626315949.jpg15.9 KB · Views: 1 -
FB_IMG_1741626304688.jpg29.1 KB · Views: 1 -
FB_IMG_1741626302157.jpg36.2 KB · Views: 1 -
FB_IMG_1741626313392.jpg27.2 KB · Views: 1 -
FB_IMG_1741626322760.jpg50.7 KB · Views: 1