uteuzi wa balozi hutegemea masuala mengi ambayo nchi zote husika zinabidi kuangalia. kabla balozi hajatangazwa lazima jina la balozi mtarajiwa liwe limekubaliwa na nchi atakayopelekwa. aidha nchi inayofanya uteuzi inabidi kujaribu kuangalia ni vitu gani vinaweza kukwaza ufanisi wa balozi anayeteuliwa.
sasa kama dini itaonekana inaweza kuwa kikwazo kwa mtazamo wa mamlaka ifanyayo uteuzi basi mamlaka hiyo itazingatia hali hiyo katika uteuzi wake. kama mamlaka itaona dini sio kikwazo basi vigezo vingine vitapewa kipaumbele.
siamini kama suala la dini ndilo limesababisha balozi wetu italy asituwakilishe
vatican bali ni kama mdau alivyoeleza hapo juu kwamba ni makubaliano yaliyopo kwamba nchi kama haiwezi kuwa na ofisi mbili za ubalozi italy (moja kwa italy na nyingine kwa vatican) basi itabidi nchi hiyo itumie ubalozi wake uliopo nje ya italy.
tovuti ya ubalozi wetu ujerumani inaonyesha kwamba ubalozi huo pia unatuwakilisha huko uswiss, austria, poland, jamhuri czech, slovakia, rumania, bulgaria, na hungary. haionyeshi vatican (sasa sijui kama wamekosea au vipi ila pia bado inamuonyesha chenge kwenye baraza la mawaziri)