Mabando yanashusha muziki wetu, kwa sasa ni shughuli pevu kupata views milioni

Mabando yanashusha muziki wetu, kwa sasa ni shughuli pevu kupata views milioni

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Katika dunia ya sasa, views ni kipengere mojawapo muhimu sana cha kuitrendisha sanaa ya nchi fulani katika uso wa dunia.

Hali imekua tete baada ya mabando kupanda bei saizi youtube watu wanaingia kwa machale,

Views chache pia zinawapunguzia mapato wasanii, youtube wanalipa kwa kigezo kinachoitwa CPM (Cost Per Mile) kipimo chao ni malipo kwa kila views 1,000. kwa hapa kwetu wastani huwa ni wa dola 1 hadi dola 1.5 (shilingi elf 2,300 hadi shilingi 3,500) kwa views 1,000 na malipo huwa yanafanyika kila tarehe 22 au 23 kupitia western union ama kupitia bank (wire transfer)

Ilishazoeleka msanii kuandaa fungu la milioni 3 au zaidi kwajili ya video, hii yote ilitokana na uhakika wa kurudisha pesa hio kwa views , lakini kwa sasa kwa hii hali wasanii watakosa pesa za kurekodi videos zeye ubora wa hali ya juu na pia hata huko studio wataanza kujibana, hii kitu itakata mabawa wa sanaa yatu ambayo ilianza safari ya kusambaa nje ya nchi,

Video ya bia tamu iliyosubiriwa kwa hamu leo ni siku ya tatu haijapata views milioni

1635792928221.png



Ali kiba aliezoeleka kulaza views milioni ndani ya siku, nae kasota siku tatu leo ndio kapata views milioni

1635793076625.png


huku kwengine ni mtafutano tu

1635792961576.png


1635792981918.png


1635792943930.png
 
Wote walikuwa kwenye jukwaa la kijani wakituimbia mcc mbele kwa mbelee[emoji3]
 
Kwa hyo alikiba mpaka leo ameingiza

(1,000,000÷1000)×3000

Kaingiza tsh 3,000,000 sio mbaya lakini bado mwez haujafika jumlisha show

Kafaida kadooogo japo s haba nakaona
 
Kwa hyo alikiba mpaka leo ameingiza

(1,000,000÷1000)×3000

Kaingiza tsh 3,000,000 sio mbaya lakini bado mwez haujafika jumlisha show

Kafaida kadooogo japo s haba nakaona
Yaani views milion 1 uje upate tsh milion tatu?

Au umemaanisha nini mkuu?
 
Umeelewa swali?
Yes, views milioni 1 wastani ni shilingi elf 3, views milioni sawa milioni 3.

wengi huwa wanafikiri views ni ujivuni, la hasha!! views ni pesa zile, ukiwa nazo nyingi zinanunua hadi rolls royce matoleo ya mwaka huu huu 🙂 🙂
 
Hao wasanii so wapiga kampeni za CCM, acha waisome namba [emoji16][emoji16][emoji16]
Namba inasomeka kwakweli, Boa kina shilole kwa sasa wapo bize na migahawa, muziki wanafanya kama hobby tu, hata usipowalipa maisha yanaenda
 
Yes, views milioni 1 wastani ni shilingi elf 3, views milioni sawa milioni 3.

wengi huwa wanafikiri views ni ujivuni, la hasha!! views ni pesa zile, ukiwa nazo nyingi zinanunua hadi rolls royce matoleo ya mwaka huu huu 🙂 🙂
Ulicho kiandika nikikiwasilisha katima namba kinakuwa hivi:-

1,000,000 = tsh 3000
Na
1,000,000 = tsh 3,000,000
🥲🥲

Naomba unirekebishe kabla sijauliza swali zaidi
 
Ulicho kiandika nikikiwasilisha katima namba kinakuwa hivi:-

1,000,000 = tsh 3000
Na
1,000,000 = tsh 3,000,000
🥲🥲

Naomba unirekebishe kabla sijauliza swali zaidi
Yes, huo ndio wastani, malipo huwa ni 2,000 hadi 3,000 mara nyingi.

Kumbuka sio youtube mwenye hizo hela.

Vodacom, Tigo, Airtel, na makampuni mengine huwa wanawalipa youtube hizo hela, Youtube anaweka matangazo kabla video haijaanza kuchezwa (skip ads) vodacom anaweza akawa analipia dola 2 kwa kila watu elf 1 wataoona tangazo lake, youtube wanachukua asilimia 32, inayobaki 68 wanampa msanii ambae matangazo yalionyeshwa kwenye video zake.

dola 2 hapo asilimia 68 ni sawa na shilingi 3,100, unachobisha ni kipi?, unadhani youtube ni wezi wasimlipe msanii??

Mwengine atalipia hata dola 1, dola 1.5, dola 3, dola 4, n.k yeye youtube anapachika tangazo kwenye video, asimilia 32 anabaki nayo, 68 anamlipa msanii.
 
Back
Top Bottom