Naomba niende kwenye mada husika kwa kuwaelekeza kwenye mifano halisi.
Nachukulia mfano Baraza la ardhi wilaya la Arusha ambapo migogoro ya ardhi imetamalaki na haiwezi kwisha kwa sababu migogoro mingi inachagizwa na wenyeviti wa mabaraza..
Majuzi kwenye pita pita zangu, nikitokea zilipo ofisi za RITA Arusha kufuatilia cheti zilizopo kwenye majengo yenye ofisi za mkuu wa wilaya Arusha mjini, lilipo baraza la ardhi la wilaya, nilikutana na wamama na kijana wao wakiwa wanalia sana na baadhi ya mawakili wakiwazunguka kuwapa ushauri...
Mwenyekiti wa miaka nenda rudi aitwae F.Mdac...alitoa maamuzi ya kushangaza eti wahanga wamevamiwa ardhi yao, wameenda barazani kufungua kesi, bahati mbaya wavamizi watu wa mjini na wana hela na influence...mwenyekiti akawa kwenye mapingamizi ya wavamizi wanashinda kwa gharama, kwenye mapingamizi ya wahanga wakishinda wanaambiwa gharama zitaangaliwa mwisho wa kesi...wale wavamizi wamepewa ushindi wa gharama kubwa kuzidi wanachoomba wahanga, na bado kesi ikiwa barazani, mwenyekiti anakubali wavamizi wakaze hukumu eneo ambalo Lina kesi mahakamani likamatwe liuzwe Ili wavamizi walipwe gharama walizoshinda kwenye mapingamizi...wahanga wakaomba mwenyekiti ajitoe na mwenyekiti akakataa kujitoa tena kwa gharama, aibu tupu, Yani mwenyekiti amekataa kujitoa kwenye kusikiliza shauri na kwa gharama..
Sasa unajiuliza je eneo ambalo lina mgogoro, na lina kesi barazani mbele yake mwenyekiti anapotaka likamatwe liuzwe kulipia gharama za mapingamizi madogo ndani ya kesi hiyohuyo je likiuzwa ni kesi gani itakuwa mezani kwake?? Kwahiyo hapo anamaanisha kwamba tayari atawapa ushindi wavamizi. Wakati huohuo wahanga wao wakishinda pingamizi wanaambiwa gharama zishughulikiwe mwisho wa kesi...
Haya ni madhara ya wenyeviti wa mabaraza kukaa sehemu moja muda mrefu na kujikuta wanashindwa kung'amua ama kuwa na jicho la kuona mwenye hatia ni yupi kwa sababu ya upendeleo ama rushwa.
Mamlaka za haki zinaingiliwa sana na yanahitajika maboresho makubwa na kuingiliwa kati kunusuru hali hii.
Sasa wakati wale mawakili wanawashauri wahanga wale nikaskia wakisema wakili mmoja ambae ni mwana wa judge mstaafu na ambae mdogo wake kwa sasa nae ni msaidizi wa judge Arusha hapo hapo alimlipia mwenyekiti ada ya wanae yote mwaka Jana...you can imagine hii inasababishwa na nini...ndo yale mazoea ya kuwaacha wenyeviti mahala pamoja muda mrefu.
Sasa mawakili na wenyewe walikuwa wanalalamika kuhusu maamuzi yasiyoeleweka yanayotolewa na mwenyekiti na waliwashauri waende mahakama kuu lakini waombe sana Mungu kwasababu wakili wa wavamizi ana influence kule mahakama kuu kwani mdogo wake ni msaidizi wa judge na baba yake ni judge mstaafu na kwa sasa ana ofisini ya SHERIA..huko mahakama inaweza kuwa vigumu sana kwao kutusua... Wakaendelea kuna wakati wakili huyo mtoto wa judge, alikamatwa karibia na kisongo airport akitoa rushwa kwa wakili wa takukuru lkn takukuru walimkamata...
Serikali ifanye tathmini kama haya mabaraza yana ulazma wa kuendelea kubaki MAANA yanachagiza migogoro lukuki.
Jaji mkuu pamoja na judge mfawidhi wasikubali watu kuingilia mifumo ya kimahakama.
Ombi langu enyi majaji wastaafu pumzikeni Ili mpate baraka msiingilie wala kuwashawishi majaji waliopo kazini kwani wanajua wajibu wao na huu ni wakati wao. Waacheni majaji watende haki.
Waziri wa ardhi naomba ulione hili.
Jaji mkuu naomba ulione hili