Mabaraza ya rasimu ya katiba

Meshack E

Member
Joined
Jul 12, 2013
Posts
5
Reaction score
1
Mimi ni mmoja kati ya wajumbe wa mabaraza ya katiba. Rejea tamko la m/kiti wa tume ya mabadiliko ya katiba,
"Tume ya Mabadiliko ya Katiba imesema vikao vya mabaraza ya Katiba ya Wilaya sasa vitaanza tarehe 12 Julai – 2 Septemba, 2013"
na kwmba vitatumia siku 54
Mimi kama mjumbe sina taarifa yeyote na hata mtendaji wa kata naye kadai hana taarifa yeyote.
Swali ni je lengo la kutumia siku 54 litatimia?
Pili ni nini kinaendelea, je kuna maeneo vikao vimeanza?
Je, unataarifa gani juu ya hili?
 
vikao vinafanyika kwa siku tatu tu ktk kila wilaya husika, hizo siku 54 ni kipindi chote ambacho hayo mabaraza yatakua yanakaa kwa nchi nzima, mabaraza ya katiba mkoa wa dar es salaam yanaanza kukaa mapema mwezi ujao wa 8.
 

Huku kwetu wamemaliza.

Walikaa siku tatu tu. Huku kuna watu waloijidanganya kwamba ni ajira ya muda mrefu mpaka Katiba ipatikane wakiwa wanalipwa mishahara. Wakahonga ni mwisho mpaka wengine wakauza mifugo ili wapate hizo nafasi. Sasa juzi wameenda wakakaa siku 3 huku wakilipwa 65,000/= kwa siku. Imekula kwao!!

Isije ikawa na wewe mkuu ulitoa rushwa ili upitishwe!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…