Mabasi 38 ya kampuni ya New Force yapigwa stop na LATRA kusafiri usiku, kuanza huduma saa 12 asubuhi

Hatua nzuri,hata hivyo wamechelewa sana,hii kitu inahusu uhai wa watu,mmesubiri mpaka afanye ajali 5 ndio mchukue hatua,inasikitisha sana kwa kweli...
 
New force mwamba wa Kusini ngoja kampuni zingine zipate abiria nazo
 
Hatua nzuri,hata hivyo wamechelewa sana,hii kitu inahusu uhai wa watu,mmesubiri mpaka afanye ajali 5 ndio mchukue hatua,inasikitisdha sana kwa kweli...
Ya kwanza Huwa ni kosa zaidi ya hapo Huwa ni makusudi
 
Ukipigwa stop inatakiwa usimamishiwe Kila kitu kuanzia marejesho ya Kodi,nssf nk
 
Wanyang'anywe leseni kabisa
 
Basi ilo ambalo kwasasa ni kinara wa ajali limefungiwa kutoa huduma kuanzia saa 9-11 alfajiri badala yake litakua linatoka saa 12 asbh kwa uangalizi na wamepewa onyo la mwisho kabla hawajafungiwa leseni zao
 
Hivi serikali wakati inaruhusu hizi safari za usiku hawakujua kama yatatokea haya,mwanzo kilichosababisha kupiga marufuku safari za usiku zilikuwa ajari ni miaka ya tisini kabla ya elfu mbili,nashangaa wanajitoa ufahamu wanaruhusu tena wakati madreva ni hawa wenye kuendesha hovyo Kwa Kasi kama wanavuta bangi,na usiku wanaijua hakuna trafiki wa kuwauliza,kifupi ngozi nyeusi haiwezi kujiendesha mpaka isimamiwe,utashangaa watu wanagongwa magari tena kwenye zebra mchana kweupe sembuse usiku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…