Mabasi 750 ya mwendokasi kuanza kazi Mbagala Machi mwakani

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mabasi 750 Yaendayo Haraka yanatarajiwa kuanza kufanya kazi katika barabara ya Mbagala jijini Dar es Salaam, Machi 2023.

Mradi huo ambao ni awamu ya pili unatarajiwa kuanza na mabasi 750 kutokana na wingi wa watu katika eneo hilo.

Mradi wa mwendokasi Mbagala utasaidia kusafirisha abiria 600,000 mpaka 700,000 kwa siku kupitia barabara hiyo.

Mwendokasi.jpeg

Good kama siyo porojo za serikali za kiafrika hasa za kwetu hizi
 
Danganya toto.

Ya kivukoni mbezi-kibaha abiria wanajazwa kama nyanya kisa yapo machache ili kuongeza faida ndio iwe huko??

Huko watawajaza hadi juu ya basi.

Watanzania hatuwezi kusimamia chochote aisee.

Mradi mdogo tu kama huo unatushinda kuumanage.

Sasa hivi huko mbezi usafiri wa bajaji umeshika kasi baada ya mwendokasi kukosa ubora.

Abiria anaona bora apande bajaji kuliko kugombania mwendokasi akajiweke kwenye risk ya kupata magonjwa.

Ni aibu kubwa sana.
 
750 ama 75!? Kama tuliaminishwa uwepo wa viwanda 8,400 katika Tanzania mpya ya viwanda ambavyo havikuonekana, katika hili nalo itakuwa ni porojo kama zilezile.
 
Mabasi 750 Yaendayo Haraka yanatarajiwa kuanza kufanya kazi katika barabara ya Mbagala jijini Dar es Salaam, Machi 2023.

Mradi huo ambao ni awamu ya pili unatarajiwa kuanza na mabasi 750 kutokana na wingi wa watu katika eneo hilo.

Mradi wa mwendokasi Mbagala utasaidia kusafirisha abiria 600,000 mpaka 700,000 kwa siku kupitia barabara hiyo.

Hivi mleta mada unaelewa maana ya mabasi mia saba?
Achen utani, hicho kitu hakipo hapa bongo.

Huenda mleta mada unamaanisha mabasi 75, kitu ambacho kiuhalisia kinawezekana lakini huenda nacho kisiwezekane kwa Dar.
 
Ni ya gasi au tunaendelea na yale ya diesel au??
Maana nchi hii ni pana sana jaman
 
Hivi mleta mada unaelewa maana ya mabasi mia saba?
Achen utani, hicho kitu hakipo hapa bongo.

Huenda mleta mada unamaanisha mabasi 75, kitu ambacho kiuhalisia kinawezekana lakini huenda nacho kisiwezekane kwa Dar.
Pengine mtoa mada ana maanisha uwepo wa "bajaji" 750 zilizo maalumu zitakazo ruhusiwa kupita katika njia ya mabasi ya mwendokasi.
 
Back
Top Bottom