Mabasi mapya ya DART yaliyokuwa yamezuiliwa sasa yameruhusiwa na kuanza kufanya kazi

Mabasi mapya ya DART yaliyokuwa yamezuiliwa sasa yameruhusiwa na kuanza kufanya kazi

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Toka mradi hui wa mabasi ya mwendo kasi, hivi sasa ni zaidi ya miaka 4 na hatujaona mabasi mengine mapya yakiingizwa Barabarani.

Takribani miaka 2 iliyopita tulisikia "tetesi" kuwa DART walikuwa wameagiza magari mapya, lakini yalikuwa yamezuiliwa bandarini kutokana na kudaiwa kodi!

Kwa kweli hali ilikuwa mbaya sana kwenye mabasi hayo, kwa namna ya abiria walivyokuwa "wanashonana"

Ukizingatia kipindi hiki ni cha ugonjwa hatari wa corona, kwa namna mabasi hayo yalivyokuwa yanajaza abiria wake, ilikuwa ni hatari Sana kwa usalama wa abiria hao

Tunaamini kutokana na DART kuyaingiza Barabarani hayo mabasi, basi ile hali ya kuyajaza abiria kupita kiasi, itaisha Katika kipindi kijacho
 
Ni kweli, ni mapya, nimeyapanda juzi kati nilivyokuja mjini kushangaa maghorofa.
 
Toka mradi hui wa mabasi ya mwendo kasi, hivi sasa ni zaidi ya miaka 4 na hatujaona mabasi mengine mapya yakiingizwa Barabarani.

Takribani miaka 2 iliyopita tulisikia "tetesi" kuwa DART walikuwa wameagiza magari mapya, lakini yalikuwa yamezuiliwa bandarini kutokana na kudaiwa
Kwa Dar, hususani kwenye usafiri wa jumuia, ni Mungu tu ndio anasaidia, hata leo nenda sehemu kama mbagala, tandika, tegeta, bado ujazaji wa abiria uko pale pale tu!!na no barakoa!!
 
Ni kweli,ni mapya,nimeyapanda juzi kati nilivyokuja mjini kushangaa maghorofa
Je ni yale tuliyosikia kuwa yalikuwa yamezuiliwa bandarini kwa kutolipiwa kodi?
 
Kwa kweli hali ilikuwa mbaya sana kwenye mabasi hayo, kwa namna ya abiria walivyokuwa "wanashonana"
unadhani kushonana kutaisha? let us wait and see. Hii ni Africa bwana.... naishi Kimara, ngoja nione
 
Vibaka walikuwa wanaipenda mwendo kasi, simu zimepigwa sana, labda nafuu itapatikana.
 
Back
Top Bottom