Poppy Hatonn
JF-Expert Member
- Apr 9, 2021
- 3,095
- 4,632
Afande Awadhi Hajji ( Mkuu wa Operesheni na Mafunzo)alikuwa anasema jana amefika Mbeya kutazama kama matayarisho ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa yanaendeles vizuri na pia kutazama suala la usalama barabarani lakini ajali imetokea kule leo.
Mabasi mawili, moja likiwa mali ya Kampuni ya Kapricon na jingine la Premier Line, yamegongana uso kwa uso katika eneo la Sae, Jijini Mbeya, leo Oktoba 7, 2024. Ajali hiyo imeleta taharuki kubwa kwa wakazi wa eneo hilo, huku jitihada za uokoaji zikiendelea.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limefika eneo la tukio kwa haraka na linaendelea na shughuli za kuwaokoa abiria waliokwama ndani ya mabasi hayo. Hata hivyo, hadi sasa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na Jeshi la Polisi kuhusu idadi ya majeruhi au vifo vinavyoweza kuwa vimetokana na ajali hiyo.
Inadaiwa kuwa mabasi hayo yalikuwa yakielekea maeneo tofauti, ambapo basi la Kapricon lilikuwa likitoka Mbeya kuelekea Tunduma, huku basi la Premier Line likielekea Mbeya kutoka Dar es Salaam. Chanzo halisi cha ajali bado hakijabainika, ingawa inaaminika kuwa mwendo kasi wa mabasi hayo huenda ulichangia.
Shughuli za uokoaji zinaendelea huku mamlaka zikitoa wito kwa madereva kuwa waangalifu zaidi barabarani ili kuepusha ajali kama hizi.Ripoti zaidi kuhusu hali ya abiria waliokuwamo zinasubiriwa kutoka kwa mamlaka husika.
PIA SOMA
- Poleni sana wote mliopata majanga kwenye ajali ya mabasi ya Premier na Kapricon