Tetesi: Mabasi ya Abood kuanza safari za Kampala na Karagwe

Tetesi: Mabasi ya Abood kuanza safari za Kampala na Karagwe

MBONA ABOOD ANA SAFARI MPKA BUKOBA

TRIP ANAYOANZA NI YA KAMPALA TU HYO KARAGWE NI NJIANI KUPITA TU
Kuna namna mbili kwenda Kampala ukitokea Kahama.
1. Kupitia Biharamulo, Bukoba, Kyaka hadi Mutukula.
2.Kupitia Nyakahura, Benako-Ngara, Karagwe, Kyaka hadi Mutukula.
Njia ipi inayoanzishwa?

Hivi sasa kuna mabasi yanayoishia Bkb kwa njia ya Biharamulo hadi Bukoba.
 
Itabidi waanze kubeba madumu ya dizeli kwenye buti. Maana hakuna namna nyingine.

Kuna siku nilipanda basi lao la Mbeya. Tulipofika Doma, mafuta yakakata. Tulilazimika kusubiri mpaka gari yao itoke Moro ituletee, ndiyo tukaondoka.
Daa!
Jirani na eneo hilo hakukuwapo kituo cha mafuta.
 
Atakuwa amefanya vyema sana kama anaongeza route ya kutokea karagwe kwenda Dar au popote TZ mpaka Uganda maana tayari anayo route ya Bukoba - Dar. Hii itasaidia sana huko Karagwe ambako kwasasa kuna mabasi ya Arusha to Karagwe, Mwanza to Karagwe na Musoma to Karagwe
Atuletee tu tunapata shida na gari mbovu za city boy...mi niko omurushaka naisubiri kwa hamu
 
Abood mwenye mabasi sio Abood mbunge hao ni watu wawili tofauti japo ni ndugu
Unaongea hili upate sifa au una uhakika na unachokiongea?? Mimi nimelelewa na Mzee Mohammed Abood na kucheza pamoja na Abdulazeez Abood na mdogo wetu alikuwa Majid..Kazi yangu ya kwanza nilifanya Abood bus soon after kumaliza form four mwaka 96..sasa ngoja nikwambie ambayo huyajui..

Ile kampuni inaitwa Mohammed Abood and sons company limited ikiwa na fleet ya mabasi,Malori, na biashara nyingine..
1) msimamizi wa biashara ya mabasi ni mbunge Abdulazeez Abood(ambaye wewe umeleta ujuaji wako kusema ni watu tofauti wakati hawa watu sisi tumekuwa nao na kusoma nao na kucheza nao mpira pale uwanja wa kiwanja cha ndege Morogoro,huyu mimi naweza kukutana nae muda wowote nnaotaka mimi nje na ofisi yake na wakati wewe na wenzio wanaoomba misaada mtatakiwa mkapange foleni pale ofisini kwake komoa,mjini kati pale kwenye nyumba yao au uende ofisi yake pale kwa mkuu wa wilaya na cha kukuongezea miezi kadhaa iliyopita nimetoka kumjulia hali mama yake kwenye nyumba yake ya Dar es salaam..

2.Msimamizi wa kampuni yao ya uwindaji ni kaka yake Tarari Abood pamoja na investment nyingine kama Vile viwanda ambavyo kwa sasa vimechukuliwa na serikali..
3.Msimamizi wa biashara ya duka la jumla(ambalo ndio kubwa pale Morogoro tangu miaka ya 1940 huko) ni majeed Abood,mdogo wetu huyu sisi tunamuita Majeed bonge...

Hawa ndio wasimamizi wa sasa wa mohamed Abood and sons co ltd ambayo ndani yake sasa ndio kuna hiyo Abood bus services..
Nimefanya kazi Abood nkahamia HOOD na kote huko nimeishi nao mabosi kama ndugu kutokana na influence aliyokuwa nayo mzee wangu enzi hizo,Nenda pale Msamvu kamuulize msimamiz wa mabasi ya Abood pale stendi anaitwa Morisi nampa code na weee nkupa code halafu nenda kamtajie hiyo code akupe wasifu wangu hili na relationship yangu na Abood halafu next time uje ufute comment yako hii!
 
Back
Top Bottom