Mabasi ya 'Dar Express' yanahujumiwa?

hizi tabia dar express wameanza lini ?........au ndo mana watu wamekimbilia kilimanjaro siku hizi.
 
mdau wewe hupandi hili basi mara kwa mara! Shutuma zote ni ukweli mtupu mwenyewe yamenikuta, customercare 0000000000000!!!!! Bora mtu ujipandie kilimajaro express. Mwenye kampuni hana neno ila wahudumu wake ndo wamejisahau kabisa
 
Kulikoni mabasi haya siku hizi? huduma zimekuwa mbovu hawajali muda, kauli mbaya kwa wateja, hoteli yao pale korogwe imekuwa chafu, ofisi zao chafu basi tabu tupu.... SHABIBY, GREEN STAR, SUMRY tuokoeni ROUTE ya DAR ARUSHA

mkuu....hawa jamaa wameshakuwa kubafu....yote uliyosema ni kweli....watu tunasogea na metro....kili na mtei....stuka baba...
 
Kulikoni mabasi haya siku hizi? huduma zimekuwa mbovu hawajali muda, kauli mbaya kwa wateja, hoteli yao pale korogwe imekuwa chafu, ofisi zao chafu basi tabu tupu.... SHABIBY, GREEN STAR, SUMRY tuokoeni ROUTE ya DAR ARUSHA

Ni kweli Dar Express wamebweteka na kujisahau ila hayo mabasi uliyotaja hapo kama mbadala siyo kabisa

Kilimanjaro.. Mtei.. Metro
 
Ni kweli hawa wamebweteka, hili liko wazi hawako smart kama zamani. Juzi nimetoka Moshi na watoto kabla kidogo ya kufika Chalinze tukakuta wananchi wameweka barrier baada ya mtu kugongwa na gari.

Tulishuka na watoto tukawa tuko chini, ghafla konda katangaza gari inaondoka, si tukaanza kupanda, ghafla dereva akafunga mlango (automatic) wakati tunapanda, mwanangu akawa amebanwa na mlango. Mungu alisaidia hakuumia sana, akadondoka nje, kidogo tu angekanyagwa na tyre.

Nilimpomtaka dereva asimame akaendelea mbele na hakuonesha kujali hata kidogo. Niliudhika sana sana, akaenda kusimama kama mita 200 hivi baada ya kushindwa kuendelea mbele. Nliwajia juu sana, lkn tulikubaliana na wife huo ndo mwisho wa kupanda Dar Express.
 
Ni kweli Dar Express wamebweteka na kujisahau ila hayo mabasi uliyotaja hapo kama mbadala siyo kabisa

Kilimanjaro.. Mtei.. Metro

Hivi Royal coach bado wana-operate jamani? was my favourite but nina muda sijaenda pande hiyo
 
Hivi Royal coach bado wana-operate jamani? was my favourite but nina muda sijaenda pande hiyo
Hivi ni mabasi gani ambayo ni mazuri na yenye sifa za usalama ya kupanda route ya Arusha-Dar?
 
Kama lugha ni mbaya naamini watajisahihisha, kwa upande mwingine hii ndio kampuni pekee inayofunga tairi zinazotambuliwa kimataifa yaani Bridgestone na Michelin. Hizo nyingine ni Mchina, you can go and prove.
 
Hivi ni mabasi gani ambayo ni mazuri na yenye sifa za usalama ya kupanda route ya Arusha-Dar?

Royal coach ndo chaguo sahihi kama bado wana operate. Ni salama sana, yaani unalala tu bila wasiwasi wo wote, huduma A. Shida ni kwamba usiwe na haraka kwani utawachukia kupita maelezo manake mwendo wao ni wa jongoo kabisaa. Nauli yao pia ilikuwa juu sana by then (mara mbili ya zile za kawaida). Binafsi nilikuwa nawapenda sana kwavile sipendi kabisa mabus yanayokimbia hadi roho inakuwa juu juu.
 
Kama lugha ni mbaya naamini watajisahihisha, kwa upande mwingine hii ndio kampuni pekee inayofunga tairi zinazotambuliwa kimataifa yaani Bridgestone na Michelin. Hizo nyingine ni Mchina, you can go and prove.
pia ndio kampuni pekee yenye mabasi aina ya MERCEDES Benz, ghali kuliko Scania na Yutong aka mchina.
lakini kiukweli nikichunguza kwa umakini nimeona kuna tofauti ya rangi na maandishi kwenye mabasi ya hii kampuni, inaonekana kama yamebinafsishwa kwa uongozi/mmiliki mwingine
 
Royal yamechoka hivi sasa, nayaona yanaenda kusini mtwara na masasi.
 
Kiburi cha jina, watu hawajui biashara wanatafuta wateja kwa shida, wakiwapata wanaleta dharau, simple hawajui biashara, angulo Lao Laja na Ni kubwa.

Kulikoni mabasi haya siku hizi? huduma zimekuwa mbovu hawajali muda, kauli mbaya kwa wateja, hoteli yao pale korogwe imekuwa chafu, ofisi zao chafu basi tabu tupu.... SHABIBY, GREEN STAR, SUMRY tuokoeni ROUTE ya DAR ARUSHA
 
Sio siri Dar Express wanaboa sana siku hizi. Yapata kama mwezi mmoja nilisafiri nao kuelekea AR. Tulipofika hotelini kwao highway, tulisubirishwa pale kama masaa matatu. Kisa, eti gari yao nyingine iliyokuwa inaelekea AR iliharibika kabla hata ya kufika Mbezi. Walichofanya wakachukua Coster na kufaulisha abiria. Coster ikaanza kutimua mbio kufukuzia basi letu ili wale abiria waje kuchanganyanywa na sisi. Taarifa tulizopata baadae ni kwamba, wakati sisi tunaingia hotelini pale, coster ndo ilikuwa inashuka wami. Ndo kisa cha sisi kuwekwa korogwe three hrs ili tusubiri watu wanaotoka chalinze. Ilinikera sana. Mtu umepanda gari Dar saa kumi na mbili asubuhi, unaishia kuja kuingia AR saa nne usiku??? Bila hata kuombwa samahani! Why??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…