gongolamboto
JF-Expert Member
- Feb 21, 2011
- 1,185
- 570
Asee wewe ni bingwa wa kuraramika.....kwani ulisafili mala ngapi?
Ukweli ni Kwamba tangu mmiliki wa Dar Express (Mr. Mremi) afiwe na mke wake... biashara zake zimeanza kwenda kombo!! wafanyakazi wanajibu wateja wanavyotaka, madereva wanaendesha gari vibaya...wanavyotaka....abiria wakilalamika wanasimamisha gari au wanaendesha gari mwendo wa kwenda kwa miguu...(taratibu sana) madereva hawajali muda!! yaani ni utumbo mtupiu......yaelekea wafanyakazi walikuwa wanamwogopa Mke wa Mremi mbaya kabisa......
Tafadhali sana andika kiswahili. Kuraramika maana yake nini? Ulisafili mala ngapi ina maana gani kwa kiswahili? Acheni kuandika lugha za kijijini kwenu
Hivi sasa abiria wa mabasi ya 'Dar Express' wanalazimishwa kulipia huduma za Choo katika stendi ya mabasi hayo mjini Moshi.
Hebu fikiria hata baada ya kulipa 30,000/- nauli, na kulazimishwa kula kwenye mgahawa wao pale Korogwe na halafu kuletwa kwa nguvu hadi stendi yao wenyewe pale Moshi ambako pia wengi hununua vinywaji au chakula kwenye mgahawa wao wa kituoni hapo. Bado sasa watu wanalazimika kulipa 200/- kuingia maliwatoni.
Huu sasa si ujambazi? Hata hivyo napenda kuamini kuwa uhuni huu pengine mhusika mkuu (Mzee Mremi) haujui na kwamba ni kazi ya watumishi wake wa hapo Moshi ambao baada ya kufuja hela wakati wa sikukuu wanalazimisha watu wawachangie.
Ila ikiwa itatokea kuwa mwenye mabasi pia amebariki nadhani ni wakati mwafaka wa kuya-boycott haya magari. Aliye na contact za Mremi (directly) ajaribu kumstua huyu mzee, asije akafa kwa presha siku biashara yake ikielekea njia ya Scandinavia Express!!!
unasema choo kinamilikiwa na DAR EXPRESS AU NI CHOO CHA STENDI?
mkuu hizi ni zama za kibiashara(no free lunch) hata DE anaweza kuwa amempa mtu kazi ya ku-run hiyo maliwato...ina umeme,maji,sabuni,toilet paper nk hivyo ni huduma tu kama nyinginePale Moshi Dar Express wana stendi yao wenyewe hawashirikiani na mabasi mengine isipokuwa ya kwao. Pia wana mgahawa pale. Sasa nashangaa kwa nini wawatoze watu kutumia choo kwani migahawa ya mjini yote si inastahili kuwa na choo cha wateja?
Hivi naweza kukupeleka nyumbani kwangu, kwa gari langu mwenyewe amabalo nimekutoza nauli halafu nikuchaji kutumia choo. Tena baada ya wewe kununua chakula nilichopika mwenyewe? Kuna wengine humu nadhani hawaelewi