Hivi sasa abiria wa mabasi ya 'Dar Express' wanalazimishwa kulipia huduma za Choo katika stendi ya mabasi hayo mjini Moshi.
Hebu fikiria hata baada ya kulipa 30,000/- nauli, na kulazimishwa kula kwenye mgahawa wao pale Korogwe na halafu kuletwa kwa nguvu hadi stendi yao wenyewe pale Moshi ambako pia wengi hununua vinywaji au chakula kwenye mgahawa wao wa kituoni hapo. Bado sasa watu wanalazimika kulipa 200/- kuingia maliwatoni.
Huu sasa si ujambazi? Hata hivyo napenda kuamini kuwa uhuni huu pengine mhusika mkuu (Mzee Mremi) haujui na kwamba ni kazi ya watumishi wake wa hapo Moshi ambao baada ya kufuja hela wakati wa sikukuu wanalazimisha watu wawachangie.
Ila ikiwa itatokea kuwa mwenye mabasi pia amebariki nadhani ni wakati mwafaka wa kuya-boycott haya magari. Aliye na contact za Mremi (directly) ajaribu kumstua huyu mzee, asije akafa kwa presha siku biashara yake ikielekea njia ya Scandinavia Express!!!