Mabasi ya Happy Nation ni Mabasi mabovu ya kihuni

Mabasi ya Happy Nation ni Mabasi mabovu ya kihuni

Minjingu Jingu

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2023
Posts
1,072
Reaction score
2,384
Haya mabasi yamekuwa yakilalamikiwa kuwa kuna uhuni mwingi unafanyika kwa abiria. Unapoenda kukata ticket wanakukatia bus jipya kwa nauli kubwa.

Ukija kupanda unakutana na ngarangara na ukiwauliza wanakuambia hilo ndo bus lililopo so uamue kusuka ama kunyoa.sasa hapo kama una dread unaona bora usuke tu maana umetoka mbali nazo.

Hapa bus tyre imeisha upepo.ikajazwa ikaisha tena. Halafu spare kumbe nalo bovu lipo tu kama pambo. Kuanza kwenyewe safari badala ya saa 2 kama wanavyosema mnaanza saa tatu kasoro.

Jamaa ni wahuni basi kama daladala. Linasimama kila kituo kuokoteza abiria.humo ndani sasa dereva amefanya ni disco.music anafungulia kama wote.ukimwambia apunguze sauti anakuwa mkali.

Gari ipo Singida tyre la mbele bovu na spare yake nayo bovu.

IMG_20240718_094147.jpg
IMG_20240718_094144.jpg
IMG_20240718_094140.jpg
IMG_20240718_094137.jpg
 
Tangu nitoke Mbeya saa 12 asbh na kufika Dar saa 7 usiku sina hamu nao. Basi bovu sana.
 
Changamoto za kawaida hizo ukiwa na usafiri..
Tusipende kulalamika tu tuwapongeze wenzetu waliojaribu...
Huko Musoma gari nzuri ni hiyo inayokuja Dar
 
Which happy nation they mean? Bora wajiite BORED KINGDOM 👑
 
Back
Top Bottom